Mkuu ukichukua ela ya safari hata kama umeenda safari mwisho wa siku unatakiwa kufanya retirement ya namna gani umetumia hela kwani unaweza ukawa umepewa dola 200 kwa ajili ya Hotel hivyo lazima uje na viambatanisho vya hotel uliyolala maana inawezekana ukawa umelala hotel ya dola 150 hivyo hiyo 50 ni change inabidi irudi (ela za safari huwa hazitolewi kama unavyotoka mshahara kwamba mwajiri wako hakufuatilii kwenye matumizi but kwenye posho za safari lazima mwisho wa siku ulete viambatanisho) nadhani wanajua taratibu unless kama alitaka mwongozo wa either azitumie ili safari nyingine ikitokea hatapewa posho ya safari atazitumia hizo hizo.
Naelewa jinsi ya kufanya retirement ila swali langu ni kuwa kila taasisi ina sheria za fedha (financial policy) hivyo si lazima iwe hivyo unavyosema kuwa kufanya retirement ni lazima. Na kama policy iko kimya (silent) inapaswa uulize kwa nia njema (in good faith). Kuna taasisi ambazo watu wenye vyeo fulani (executives) hawaulizwi kwa maana marejesho ya posho kinachotakiwa ni ripoti ya lengo analokusudiwa kulifanyia kazi; kaenda - hajaenda, kala - hajala, katuma mtu au kafanya mwenyewe. Na ndio maana swali langu la msingi ni kua sheria/kanuni zinasemaje hapa? Tuna miaka hamsini na mbili na bunge letu hili, je Nassari ni wa kwanza? Kuna wangapi huko nyuma walirudisha na kama hawakurudisha walifanya/walifanywa nini? Kwa nini ishu isiwe sheria/kanuni na usimamizi wake bali ishu inakua watu?