Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,022
- 10,190
Naelewa jinsi ya kufanya retirement ila swali langu ni kuwa kila taasisi ina sheria za fedha (financial policy) hivyo si lazima iwe hivyo unavyosema kuwa kufanya retirement ni lazima. Na kama policy iko kimya (silent) inapaswa uulize kwa nia njema (in good faith). Kuna taasisi ambazo watu wenye vyeo fulani (executives) hawaulizwi kwa maana marejesho ya posho kinachotakiwa ni ripoti ya lengo analokusudiwa kulifanyia kazi; kaenda - hajaenda, kala - hajala, katuma mtu au kafanya mwenyewe. Na ndio maana swali langu la msingi ni kua sheria/kanuni zinasemaje hapa? Tuna miaka hamsini na mbili na bunge letu hili, je Nassari ni wa kwanza? Kuna wangapi huko nyuma walirudisha na kama hawakurudisha walifanya/walifanywa nini? Kwa nini ishu isiwe sheria/kanuni na usimamizi wake bali ishu inakua watu?
Nimekupata mkuu, inaonyesha hawa jamaa huwa wanazitafuna si unaona Zambi kuna ambazo alisema kuna ugeni wa katibu mkuu na kumbe kuna zingine za nyuma alipiga kimya. Ila speaker jana alisema waliochukua warudishe taratibu zinaeleweka. Nilichojifunza hapa kuna mazoea flani ambayo yamezoeleka kuhusu hizi posho za safari na hata za wakati wa bungeni mtu anasaini tu hata kama hayupo analamba mzigo iwe kwa viongozi wakuu au wa chini, yaani ni sawa na huku uswahilini uwe na boss anapenda fedha anaweza akasaini akasepa siku nyingine na wewe unalamba hela unasepa mwisho wa siku imekuwa mazoea