Giving back to the community

Pinacoladee

JF-Expert Member
May 22, 2023
653
760
Habari zenu, Giving back to the community ni program moja nzuri sana ya kuirudishia jamii au kuwafanyia jambo jamii kwa kujitolea, tumekua tukiona baadhi ya makampuni wakifanya donation au charity events, sio makampuni au taasis zote zinafanya ili jambo, Kuna baadhi ya viwanda vilivyopo Tanzania vimekua vinafanya kazi karibu na mazingira au makazi ya watu lakini maeneo hayo hayanufaiki na chochote ukiachana na viajira viwili vitatu wanavyotoa ao wakazi wa apo wananufaika na nini au mnawapa nini? Nitolee mfano

Viwanda vilivyopo kuanzia kizuiani mpka rangitatu hata barabara za apo nje kwenu na za mitaa mmeshindwa kutengeneza,mnapata shida wenyewe na magari yenu lakini pia njia hasa mvua ikinyesha hazipitiki tunashangaa serikali inashindwa kutoa order kwa hivi viwanda vilivyopo karibu na makazi ya watu angalau ifanye kitu au jambo kwa ajili ya wananchi.

Giving back to the community inayofanywa na taasisi au wabunge ni kutembelea vituo vya watoto yatima, hii sio mbaya lakini unakuta wanataka sifa unakuta wamepelekea vijuice vya u fresh na vipipi vya ivory na wanapiga nao picha na kuwapost mitandaoni, kama mna nia kweli ya kusaidia kwanini msiwalipe ada watoto yatims? watoto yatima wanahitaji sana elimu kuliko pipi ivory.

Wabunge na nyie mnairudishia nini jamii pamoja na mishahara yenu au posho zenu? Wengi wenu ni mshajijenga na mna mabiashara makubwa,lakini na nyie mmekua wale wale wa kwenda vituo vya watoto yatima na kupiga picha nao kwa kuwapa vijuice vya azam. Aibu naona mimi uku iki kitu kinaniuma sana wale watoto wakikua wanakuta mmewapost mitandaoni wamepewa vipipi ivory badala mngejitoa mkawasomesha shule nzuri.

Mbunge mmoja aliropoka eti boom lifutwe ili watoto wa maskini wasome kwa tabu, na sisi tunaomba angalau mkatwe mishahara na posho zenu kwa ajili ya kuisadia jamii,mkikatwa angalau asilimia fulani ipatikane,labda mkusanye million 100 kila baada ya miezi sita kwa mwaka mara mbili naamini izo million 100 zitafanya jambo fulani.

Unakuta baadhi ya viwanda au taasisi badala ya kuisadia jamii ni imekua chanzo cha uharibifu wa mazingira,wametoboa adi mashimo maji yanatiririka kwenye makazi ya watu,mvua ikinyesha tu na wenyewe wanamwaga mimaji yao, Kama wabunge mpo na mmeshindwa kusimamia na kutengeneza sheria kali Juu ya ili swala mnafanya nini sasa apo kwenye viti.
 
Back
Top Bottom