Wabunge watafuna Posho hovyo! CCM, CHADEMA wote washiriki mchezo mchafu

Mkuu ukichukua ela ya safari hata kama umeenda safari mwisho wa siku unatakiwa kufanya retirement ya namna gani umetumia hela kwani unaweza ukawa umepewa dola 200 kwa ajili ya Hotel hivyo lazima uje na viambatanisho vya hotel uliyolala maana inawezekana ukawa umelala hotel ya dola 150 hivyo hiyo 50 ni change inabidi irudi (ela za safari huwa hazitolewi kama unavyotoka mshahara kwamba mwajiri wako hakufuatilii kwenye matumizi but kwenye posho za safari lazima mwisho wa siku ulete viambatanisho) nadhani wanajua taratibu unless kama alitaka mwongozo wa either azitumie ili safari nyingine ikitokea hatapewa posho ya safari atazitumia hizo hizo.

Naelewa jinsi ya kufanya retirement ila swali langu ni kuwa kila taasisi ina sheria za fedha (financial policy) hivyo si lazima iwe hivyo unavyosema kuwa kufanya retirement ni lazima. Na kama policy iko kimya (silent) inapaswa uulize kwa nia njema (in good faith). Kuna taasisi ambazo watu wenye vyeo fulani (executives) hawaulizwi kwa maana marejesho ya posho kinachotakiwa ni ripoti ya lengo analokusudiwa kulifanyia kazi; kaenda - hajaenda, kala - hajala, katuma mtu au kafanya mwenyewe. Na ndio maana swali langu la msingi ni kua sheria/kanuni zinasemaje hapa? Tuna miaka hamsini na mbili na bunge letu hili, je Nassari ni wa kwanza? Kuna wangapi huko nyuma walirudisha na kama hawakurudisha walifanya/walifanywa nini? Kwa nini ishu isiwe sheria/kanuni na usimamizi wake bali ishu inakua watu?
 
Nasari hakuwa na harambee yoyote jimboni mie naishi arumeru mash,niko karibu na chama ninajua ratiba zote ni kiongozi pia,zambi naye mwongo kwa nn hakutoa taarifa hawa wanasiasa ni waongo,wahuni,mafisadi na wazandiki sio ccm,chadema,cuf,nccr nk
 
Uwa nashangaa sana watu wanavyotoana macho, kwa ajili ya wanasiasa,hawa baba na Mama yao ni mmoja,Shtuka!
 
HIVI TUNAPOSEMA ARUDISHE PESA ZA WALIPA KODI; NI KWELI NI FEDHA ZA WALIPA KODI? AKIZIRUDISHA ZITATUFIKIA? Hii nchi ili urasimu uishe LAZIMA WATU WOTE WAONDOLEWE WAPANDWE WENGINE WAPYA! Anayebisha abishe nami nimpe mifano ya watu tuliowaita wazalendo kumbe ni sawa na kulala kwenye kitanda chenye kunguni mchana! Mkuu wa mkoa wa Kg aliwahi sema " SITAKI KUSIKIA HABARI ZA KILIMO CHA TUMBAKU KTK MKOA WANGU- ZAO HILI LINACHANGIA KIKUBWA KTK KUHARIBU MAZINGIRA", baada ya hapo; bodi ya Tumbaku taifa wakamchagua kuwa mw/kiti wa Bodi ya Tumbaku ATTT tanzania! Baada ya kuhudhuria kikao kimoja tu alikuja na kusema "WATU WOTE LIMENI TUMBAKU NI ZAO LINALO WEZA KUMWINUA MKULIMA KIUCHUMI". Nami nikakumbuka mikakati ya zamani kanisani kiuongozi " Mtu yeyote anayeikritisaizi dini mpeni cheo ktk dini hiyo" - utaona tu!
 
Ndugu zangu msisumbuke na Wabunge hii kitu iko idara zote za Serikali. Indeed ni kama kasheria kwamba ulamba mshiko whether unasafiri or not it is non of your boss business, au kufupisha safari etc... hii kitu ikifuatiliwa kwa undani itavua watu wengi nguo.

Sisi wadanganyika tukubali tu hakuna kitu kinaitwa mkombozi au sijui wawakilishi whatever...

Msidhani waBunge hawajui huu mchezo... uko sana... na hawakuwa wanasema ila ni kwa kuwa sasa wanaanza kujiandaa na uchaguzi.
Poleni wadanganyika wenzangu. Kwa hili hili hata Utouh hagusi...
 
Wakati anachukuwa alikuwa hajui kama anasafiri acheni utoto arudishe pesa za walipa kodi.

Siku hizi umekuwa Kubwa Jin g a Hapo pameandikwa kabisa ikatokea Dharula jimboni kwake kulikuwa na Harambee... au ndio Gongo za Dr. Slaa unazopinga zimekulevya... hujui hata unachoongea kwa Ulevi.... Noma Sana!
 
Suala dogo linasemwa sana!! Vipi hili la Alhaji Kapuya kubaka na kumwamukiza ukimwi mtoto wa miaka 14 mbona hakuna anayelitilia maanani?
 
Ndizo alizozitoa mchango kwenye harambee na kuwarudishia walipa kodi na si walipwa kodi.

Huo ushahidi atausemea mahakamani, na sheria ndio itasema kama ni haki fedha za serikali kubadilishwa matumizi kihuni hivyo.
 
Harambee za dharura ni nadra. Nyingi hupangwa na kuandaliwa kwa muda wa kutosha. Maelezo ya ziada kuhusu udharula huu yanahitajika.
 
Alitakiwa kurudisha pesa na kuandikiwa stakabadhi, siyo kutoa taarifa na kuomba muongozo.


Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums

Wanasiasa wanapenda sana kuingiza siasa kila mahali, hata pasipo na ulazima; au sijui wanatuona mamburula......sasa wewe umepewa pesa ya safari, safari hukwenda, si hata mtu mwenye utindio wa ubongo angejua kuwa kinachofuata (common sense) ni kurudisha pesa uliyochukua. Sasa muongozo wa hapa wa nini? hilo neno la kuomba muongozo limewakaa kichwani mpaka hata wanaanza kupoteza "common sense". Next time watatuambia nilishindwa kuleta maendeleo jimboni kwangu kwasababu nilikuwa nasubiri muongozo jinsi ya kusaidia wapiga kura wangu.

Hapo wote hao, Zambi na Nasari hakuna mwenye nafuu, issue ni kurudisha hiyo pesa na siyo kuomba miongozo.
 
Barua aliyoandika kwa katibu wa bunge ilishampa mwongozo, either kurudisha ama kuwasaidia wapiga kura wake. Wewe ni nyang'au ama? waambie wabunge wa ccm warudishe fedha au watolee taarifa walizifanyia nini

Huo mwongozo unaitwaje.. Btw Hakuna muongozo kama huo..

Sasa anasubiri nini kuzirudisha?

Jibu nadhani unalijua...

Hao ndo wabunge wa CHADEMA, CHAMA CHA UPINZANI.hAHAHAHA ,wanayoyafanya hakika ni ya kuzidi kumuumiza mTANZANIA.

.. Ni wana Siasa.
 
Harambee za dharura ni nadra. Nyingi hupangwa na kuandaliwa kwa muda wa kutosha. Maelezo ya ziada kuhusu udharula huu yanahitajika.

Kama haupo Tanzania hasa vijijini unaweza kusema hayo maneno, harambe inategemea ni harambe ya namna gani.
 
Leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wakiwemo na wa upinzani moyo uliumia sana. Nimefuatilia gazeti la Raia Mwema na ndo maana nikaamua kumpongeza huyo bwana mdogo Nassari kwa kweli ni mfano wa kuigwa

Amekiri kweli kuwa alichukua posho kwa ajili ya safari ya kwenda Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni vyema akajumuika na wananchi waliomchagua badala ya kusafiri.

Kizuri zaidi ni kwamba aliandika ujumbe kumtarifu katibu wa bunge juu ya dharula iliyokuwa imejitokeza na kuomba muongozo wake kuhusiana na fedha hiyo na nakala akapeleka kwa katibu mkuu CHADEMA.

Swali la kujiuliza hapo ni wabunge wangapi wa CCM wanaoweza kufanya hivyo ? nimesikiliza utetezi wa Godfrey Zambi mbunge wa Mbozi kwa kweli haukunishawishi. Yeye anasema alikuwa na ugeni wa Kinana mkoani kwake na baada ya hapo alifiwa na mdogo wake. Ni kweli kuwa asingeweza kuendelea na safari kwa sababu hizo lakini kwa kiongozi makini unapaswa kutoa taarifa kwa wakati juu ya yaliyokusibu kama alivyofanya Nassari na usisubiri mpaka uhojiwe na waandishi wa habari

Nawasilisha

ukipata dharula si unarudisha au inakuwaje?
 
Huu upuuzi haujadiliki wala huyo Nassari si mwaminifu alijua fika kuwa anatakiwa kwenda jimboni kwake kuonana na wanachi wa jimbo lake kwenye harambee maalumu iliyoandaliwa muda mrefu.Iweje akubali kuchukua posho ya kwenda nje ya nchi wakati anashughuli nyingine? Ni mwizi kama wengine hakutarajia kama hii siri ingevuja kurudisha hiyo fedha ni lazima na angekuwa si mwizi siku aliyowasilisha ujumbe wa kutokwenda safari angerudisha na hizo fedha.
Haya ndio mambo mheshimiwa Zitto anayotofautiana na wenzie wanamwita msaliti.
Nassari na wenzenu nyie ndio wasaliti kwa wananchi tuliowachagua mkatuwakilishe kumbe ndio kwanza mnaenda kutuza na kwa millioni nane za kwenda Malasia sheherekea Christmass vizuri ushatupiga bao.
 
Hospitalini hakuna madawa, Vijana wetu wa elimu ya juu wanakosa mikopo, walimu wanadai stahili zao, askari wetu wengi na hasa wa vyeo vya chini choka mbaya, akina mama wajawazito wanadaiwa mpaka mikasi na pamba wanapokwenda kujifungua, watoto wetu shule za msingi wengine hawajawahi kukalia dawati zaidi ya mawe na matofari. Inauma unapogundua kwamba kumbe wawakilishi wetu (wabunge) wanaolipwa zaidi ya 300,000/- kama posho kwa siku bado wakichukua posho za safari kwa mamilioni na kisha kuishia Chako ni Chako kuponda raha kwa fedha ya kodi zetu, wakiwa ukumbini wanajidai wanatupenda. AIBU YENU WAHESHIMIWA WABUNGE
 
Leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wakiwemo na wa upinzani moyo uliumia sana. Nimefuatilia gazeti la Raia Mwema na ndo maana nikaamua kumpongeza huyo bwana mdogo Nassari kwa kweli ni mfano wa kuigwa

Amekiri kweli kuwa alichukua posho kwa ajili ya safari ya kwenda Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni vyema akajumuika na wananchi waliomchagua badala ya kusafiri.

Kizuri zaidi ni kwamba aliandika ujumbe kumtarifu katibu wa bunge juu ya dharula iliyokuwa imejitokeza na kuomba muongozo wake kuhusiana na fedha hiyo na nakala akapeleka kwa katibu mkuu CHADEMA.

Swali la kujiuliza hapo ni wabunge wangapi wa CCM wanaoweza kufanya hivyo ? nimesikiliza utetezi wa Godfrey Zambi mbunge wa Mbozi kwa kweli haukunishawishi. Yeye anasema alikuwa na ugeni wa Kinana mkoani kwake na baada ya hapo alifiwa na mdogo wake. Ni kweli kuwa asingeweza kuendelea na safari kwa sababu hizo lakini kwa kiongozi makini unapaswa kutoa taarifa kwa wakati juu ya yaliyokusibu kama alivyofanya Nassari na usisubiri mpaka uhojiwe na waandishi wa habari

Nawasilisha

halafu Zitto akiwaambia watoe taarifa ya matumizi ya fedha wanazopewa anaitwa msaliti
 
Huyo bwana mdogo mshamba tu, km amepata dhara jimbon kwake c angerudisha hiyo pesa? Kulikuwa na ulazims gan wa kuitumia jimbon kwake! Km analipenda xn jimbo lake c atumie sehemu ua mshahara au posho yake km anavyofanya mnafki zitto? Acha kutetea mafisad hao dada angu
 
Back
Top Bottom