Leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wakiwemo na wa upinzani moyo uliumia sana. Nimefuatilia gazeti la Raia Mwema na ndo maana nikaamua kumpongeza huyo bwana mdogo Nassari kwa kweli ni mfano wa kuigwa
Amekiri kweli kuwa alichukua posho kwa ajili ya safari ya kwenda Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni vyema akajumuika na wananchi waliomchagua badala ya kusafiri.
Kizuri zaidi ni kwamba aliandika ujumbe kumtarifu katibu wa bunge juu ya dharula iliyokuwa imejitokeza na kuomba muongozo wake kuhusiana na fedha hiyo na nakala akapeleka kwa katibu mkuu CHADEMA.
Swali la kujiuliza hapo ni wabunge wangapi wa CCM wanaoweza kufanya hivyo ? nimesikiliza utetezi wa Godfrey Zambi mbunge wa Mbozi kwa kweli haukunishawishi. Yeye anasema alikuwa na ugeni wa Kinana mkoani kwake na baada ya hapo alifiwa na mdogo wake. Ni kweli kuwa asingeweza kuendelea na safari kwa sababu hizo lakini kwa kiongozi makini unapaswa kutoa taarifa kwa wakati juu ya yaliyokusibu kama alivyofanya Nassari na usisubiri mpaka uhojiwe na waandishi wa habari
Nawasilisha