Wabunge watafuna Posho hovyo! CCM, CHADEMA wote washiriki mchezo mchafu

jnuswe

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,270
549
Leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wakiwemo na wa upinzani moyo uliumia sana. Nimefuatilia gazeti la Raia Mwema na ndo maana nikaamua kumpongeza huyo bwana mdogo Nassari kwa kweli ni mfano wa kuigwa

Amekiri kweli kuwa alichukua posho kwa ajili ya safari ya kwenda Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni vyema akajumuika na wananchi waliomchagua badala ya kusafiri.

Kizuri zaidi ni kwamba aliandika ujumbe kumtarifu katibu wa bunge juu ya dharula iliyokuwa imejitokeza na kuomba muongozo wake kuhusiana na fedha hiyo na nakala akapeleka kwa katibu mkuu CHADEMA.

Swali la kujiuliza hapo ni wabunge wangapi wa CCM wanaoweza kufanya hivyo ? nimesikiliza utetezi wa Godfrey Zambi mbunge wa Mbozi kwa kweli haukunishawishi. Yeye anasema alikuwa na ugeni wa Kinana mkoani kwake na baada ya hapo alifiwa na mdogo wake. Ni kweli kuwa asingeweza kuendelea na safari kwa sababu hizo lakini kwa kiongozi makini unapaswa kutoa taarifa kwa wakati juu ya yaliyokusibu kama alivyofanya Nassari na usisubiri mpaka uhojiwe na waandishi wa habari

Nawasilisha
 
Cha muhimu arudishe fedha za walipa kodi hizi nyingine ni porojo tu.
 
Barua aliyoandika kwa katibu wa bunge ilishampa mwongozo, either kurudisha ama kuwasaidia wapiga kura wake. Wewe ni nyang'au ama? waambie wabunge wa ccm warudishe fedha au watolee taarifa walizifanyia nini
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mbunge wa arumeru mashariki,joshua nassari amekili kuchukua posho ya safari ya kwenda malaysia lakini hakwenda hiyo safari kwa kua alikua na harambee jimboni. Na amesema yupo tayari kurudisha hizo fedha. Source raia mwema la leo.
 
Hao ndo wabunge wa CHADEMA, CHAMA CHA UPINZANI.hAHAHAHA ,wanayoyafanya hakika ni ya kuzidi kumuumiza mTANZANIA.
 
Huo nao ni ufisadi kama ufisadi mwingine tu.

Angerudisha immediately baada ya kugundua kuwa hatakwenda kwenye hiyo safari sio mpaka ashtukiwe!
 
ignorantia juris non excusat(ignorance of law is no excuse)..
ukiwa mtumishi wa umma unatakiwa ujue kuwa hela unayobaki(au kutoitumia kabisa kama ilivyotarajiwa)ni lazima ikatiwe risiti(irudishwe) kama sheria ya fedha inavyotaka.Wabunge especially wa upinzani watakuwa wameni-disappoint sana kama wamechukua hela na hawakusafiri.
 
Leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wakiwemo na wa upinzani moyo uliumia sana. Nimefuatilia gazeti la Raia Mwema na ndo maana nikaamua kumpongeza huyo bwana mdogo Nassari kwa kweli ni mfano wa kuigwa

Amekiri kweli kuwa alichukua posho kwa ajili ya safari ya kwenda Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni vyema akajumuika na wananchi waliomchagua badala ya kusafiri.

Kizuri zaidi ni kwamba aliandika ujumbe kumtarifu katibu wa bunge juu ya dharula iliyokuwa imejitokeza na kuomba muongozo wake kuhusiana na fedha hiyo na nakala akapeleka kwa katibu mkuu CHADEMA.

Swali la kujiuliza hapo ni wabunge wangapi wa CCM wanaoweza kufanya hivyo ? nimesikiliza utetezi wa Godfrey Zambi mbunge wa Mbozi kwa kweli haukunishawishi. Yeye anasema alikuwa na ugeni wa Kinana mkoani kwake na baada ya hapo alifiwa na mdogo wake. Ni kweli kuwa asingeweza kuendelea na safari kwa sababu hizo lakini kwa kiongozi makini unapaswa kutoa taarifa kwa wakati juu ya yaliyokusibu kama alivyofanya Nassari na usisubiri mpaka uhojiwe na waandishi wa habari

Nawasilisha
Wakati anachukuwa alikuwa hajui kama anasafiri acheni utoto arudishe pesa za walipa kodi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom