Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 1,439
- 2,513
Umenena vyema Mkuu,Binafsi sikushangaa kabisa kumuona Jerry Silaa akiingia na lundo la vitabu na manual zinazoelezea sheria za kodi.
Kinachonishangaza ni baadhi ya wadau kumtaka Jerry Slaa kuiweka hadharani salary slip yake ili tuone namna asivyolipa kodi kana kwamba Jerry alisema wabunge hawakatwi PAYE.
Swali muhimu ni Je wabunge hawana misamaha ya kodi?
Magari wanayokopeshwa wanalipia kodi?
Hotel wanazojenga hamna namna wanapata unafuu kwenye manunuzi ya vifaa vya ujenzi?
Nk.....nk
Kodi ni suala mtambuka na upigaji uko kwenye " exemptions "
Jumaa kareem!
Kuna mmoja aliwahi niuzia kagari kake aisee ishu ili umana pale nataka nibadili umiliki. Ule mziki wa kodi ulikuwa si wa kitoto ikanibidi nami niiuze tu.
Hawa jamaa wanamteremko sana hawajui machungu tunayopitia sisi wengine.