Wabunge wana haki ya kudai nyongeza ya mshahara, hoja yao isikilizwe wasipuuzwe

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau,

Naona kuna vugu vugu sasa wabunge kutaka kuongezewa mshahara maana hauwatoshi, binafsi nadhani wana hoja ya msingi ni vyema wakasikilizwa.

Wengi tulikuwa tunajua wabunge wanalipwa pesa nyingi sana kutokana na kazi kubwa wanazozifanya lakini nilipofuatilia kiasi anacholipwa mbunge ni kiduchu sana almost 12M pm ni ndogo sana,na bado wakifika majimboni tunawapiga vizinga mpaka inaboa.

Kama wapo wanaosikilizwa kupanda madaraja basi na wabunge tunaomba pia wasikilizwe kama bajeti inaruhusu waongezewe mishahara kazi yao ya uwakilishi majimboni ni ngumu sana.
 
Aiseee, enzi za Mwendazake mbona hawakudai?

Yaani waongezwe mishahara kwakua Jimboni wanapigwa mizinga sana?

"Mimi naona Bora kujenga barabara kuliko kuongeza mishahara"- JPM akihotubia watumishi Mei mosi flani huko Nyanda za juu kusini.
 
Wabunge? Hufanya nini? Nakushauri uende hospitali ukapime akili yako. They contribute nothing, hoja ni kusifia mama na kushukuru Mungu jinsi wanavyotafuna nchi. Miezi 3 ya budget wameondoka na millioni 400+ tax free.

Wewe una jua kwa nini Bunge lilijengwa Dodoma, si karibu na Mirembe hospital. 99 % hawana akili.
 
Nakuheshimu lakini kwa hili inapidi uende muhimbili ama mirembe wakakupime kile simba sc walichompima JONAS MKUDE.

Au simu yako kashika mtoto, au we ni mnufaika wa moja kwa moja kwa hili (mbunge)

Ama wewe ni mnufaika kwa namna moja ama nyingine kwa hili(mtegemezi wa mbunge)?
 
Mkuu ww ni mbunge na nakufaham vizur ila sheria za mitandao haziniruhusu mimi kukutaja live kwenye public. Naona umekuja kutengeneza mazingira ya kuongezewa nyongeza ya mishahara huku ukijua fika kuwa 90% ya raia kwenye jimbo lako wanaishi katika umasikini wa kutupwa, na huna mbinu wala maarifa yoyote ya kuhakikisha kuwa raia hao wa kweny jimbo lako wanaishi maisha nafuu kama unavyoishi ww. Jimboni kwako hakuna maji, barabara wala hospital ya maana, badala ya kupigania vitu hivyo ww unapigania tumbo lako tu.
 
12m Vs 0.025m salalies, wa 12m anadai ajiongezee bungeni, mwalimu wa 0.025m tsh kwa mwezi hata pakusemea tu hana wala malupulupu hana.

kweli kuishi kwingi kuona mengi.
 
Sasa ukiwaongezea,vizinga ndio vitapungua au? Hilo sio suluhisho

Tatua tatizo kwanza, kwanini wananchi wanawapiga vizinga?

Mbunge kijana inabidi atumie kiinua mgongo chake kuanzisha hata mradi atoe ajira hata kwa vijana 20 tu, sasa Hawa wabunge wanavuta mkwanja mrefu, wanajenga majumba tu.
 
12m Vs 0.025m salalies, wa 12m anadai ajiongezee bungeni, mwalimu wa 0.025m tsh kwa mwezi hata pakusemea tu hana wala malupulupu hana.

kweli kuishi kwingi kuona
Mi naona wabunge wawe wanapokea mishahara sawa na waalimu! Na posho ya vikao wasipate maana ndiyo kazi waliyoajiriwa kuifanya! Bungeni ndiyo ofisini kwao! Si sawa mtu kulipwa posho kwa kukaa ofisini kwake na kufanya kazi!! Wakishindwa waache!
 
Kwa kweli 12M pm Ni kiduchu mno kwa mbunge, hasa majimno ya utopoloni huko wanakojua mbunge ni msamalia mwema, mbunge ni mfadhili, mbunge ni tajiri kuliko wote jimboni, mbunge ni kila kitu. 12M Ni kiduchu mno. Waongezewe walau iwe 40M pm.

BTW mshahara huu ni muda mrefu Sana. Tangu enzi za kina marehemu Sitta.
 
Habari wadau.

Naona kuna vugu vugu sasa wabunge kutaka kuongezewa mshahara maana hauwatoshi,binafsi nadhani wana hoja ya msingi ni vyema wakasikilizwa.

Wengi tulikuwa tunajua wabunge wanalipwa pesa nyingi sana kutokana na kazi kubwa wanazozifanya lakini nilipofuatilia kiasi anacholipwa mbunge ni kiduchu sana almost 12M pm ni ndogo sana,na bado wakifika majimboni tunawapiga vizinga mpaka inaboa.

Kama wapo wanaosikilizwa kupanda madaraja basi na wabunge tunaomba pia wasikilizwe kama bajeti inaruhusu waongezewe mishahara kazi yao ya uwakilishi majimboni ni ngumu sana.
Tuwe na busara.
Kwani mshahara hulipwa kulingana na vizinga au mizinga unayopigwa mtaani?

Kwa mshahara ule:
1: Hulipi kodi
2: Huna makato ya afya
3: Unalipwa allowance kwa kazi uliyoiomba tena mara 10 zaidi ya watendakazi wenzio.
4: Baada ya miaka 5 unachukua NSSF/PSSF usiyochangia

Wapeni wananchi mapumziko ya kuwalisha mkavimbewa.

Kila mmoja akianza kuangalia mwenzake/mwenye kazi sawa analipwaje huko nje mbona hapatakalika hapa, tutagawana mbao tu.
 
12m Vs 0.025m salalies, wa 12m anadai ajiongezee bungeni, mwalimu wa 0.025m tsh kwa mwezi hata pakusemea tu hana wala malupulupu hana.

kweli kuishi kwingi kuona mengi.
Ni mwalimu gani analipwa 25,000 ndugu? 🤔
 
Habari wadau,

Naona kuna vugu vugu sasa wabunge kutaka kuongezewa mshahara maana hauwatoshi, binafsi nadhani wana hoja ya msingi ni vyema wakasikilizwa.

Wengi tulikuwa tunajua wabunge wanalipwa pesa nyingi sana kutokana na kazi kubwa wanazozifanya lakini nilipofuatilia kiasi anacholipwa mbunge ni kiduchu sana almost 12M pm ni ndogo sana,na bado wakifika majimboni tunawapiga vizinga mpaka inaboa.

Kama wapo wanaosikilizwa kupanda madaraja basi na wabunge tunaomba pia wasikilizwe kama bajeti inaruhusu waongezewe mishahara kazi yao ya uwakilishi majimboni ni ngumu sana.
Mtoa mada nafikiri Ushaona kwamba watu wengi bado wanamentality ya unyonge "aliye namshahara mkubwa apunguziwe au hana haki ya kudai kuongezwa mshahara, ila walio chini Wana haki ya kudai"

Hii mentality tutaiondoa lini
 
Habari wadau,

Naona kuna vugu vugu sasa wabunge kutaka kuongezewa mshahara maana hauwatoshi, binafsi nadhani wana hoja ya msingi ni vyema wakasikilizwa.

Wengi tulikuwa tunajua wabunge wanalipwa pesa nyingi sana kutokana na kazi kubwa wanazozifanya lakini nilipofuatilia kiasi anacholipwa mbunge ni kiduchu sana almost 12M pm ni ndogo sana,na bado wakifika majimboni tunawapiga vizinga mpaka inaboa.

Kama wapo wanaosikilizwa kupanda madaraja basi na wabunge tunaomba pia wasikilizwe kama bajeti inaruhusu waongezewe mishahara kazi yao ya uwakilishi majimboni ni ngumu sana.
hoja nyingine za kipuuzi kama 12m hazitoshi jea Graduate anayelipwa 750,000.00 na yule wa kima cha chini 170,000.00 atasemaje? mbunge huyo huyo analipwa posho 300,000.00 kwa siku, analipwa mafuta ya gari na mshahara wa dereva. wewe utakua ni mbunge au mkeo mbunge sio bure
 
Habari wadau,

Naona kuna vugu vugu sasa wabunge kutaka kuongezewa mshahara maana hauwatoshi, binafsi nadhani wana hoja ya msingi ni vyema wakasikilizwa.

Wengi tulikuwa tunajua wabunge wanalipwa pesa nyingi sana kutokana na kazi kubwa wanazozifanya lakini nilipofuatilia kiasi anacholipwa mbunge ni kiduchu sana almost 12M pm ni ndogo sana,na bado wakifika majimboni tunawapiga vizinga mpaka inaboa.

Kama wapo wanaosikilizwa kupanda madaraja basi na wabunge tunaomba pia wasikilizwe kama bajeti inaruhusu waongezewe mishahara kazi yao ya uwakilishi majimboni ni ngumu sana.

Jiulize ni wafanya kazi wangapi serikalini na ofisi binafsi wanalipwa 12m? Je nini kazi na majukumu ya mbunge? Nakuhakikishia kulipa vizinga sio kati ya majukumu yake, je tumefikaje hapo?
 
Back
Top Bottom