BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,049
Waungwana, hawa wabunge wa CCM wanaonyesha upumbavu wao wa hali ya juu na kutaka kuwatumia lawama watendaji wa TANESCO ambao hawahusiki kabisa na matatizo ya shirika hilo.
Uendeshaji wa TANESCO ulikabidhiwa kwa makaburu wa net group ambao waliingizwa pale kwa mtutu wa bunduki za FFU enzi za fisadi Mkapa. Walilipwa mabilioni ya pesa pamoja na kuwa walikuwa hawajui chochote kuhusiana na uzalishaji na usambazaji wa umeme. Waliondooka makaburu wale waliiacha TANESCO katika hali mbaya kuliko walivyoikuta.
Mkataba wa IPTL ambao TANESCO inatakiwa kuwalipa hao jamaa bilioni nne kila mwezi hata kama hawazalishi umeme. Mkataba wa Richmond, TANESCO inawalipa hao mafisadi shilingi 152 millioni pamoja na kuwa hawazalishi chochote. Gesi toka Songo songo pamoja na kuwa ni ya kwetu lakini TANESCO wanailipia bei kubwa sana.
Yote haya hawa wabunge wanafiki hawayaoni, sasa wanawarushia watendaji wa TANESCO lawama kuhusiana na matatizo mbali mbali ndani ya shirika hilo!
Mimi nawaambia Wabunge hao wa CCM acheni unafiki na mawazo ya kifisadi! Watanzania tumechoshwa na usanii wenu!
Wabunge waigeuka Tanesco
na Salehe Mohamed, Dodoma
KATIKA hali isiyotarajiwa, baadhi ya wabunge wameligeuka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kudai kuwa matumizi mabovu ya fedha yanayofanywa na watendaji wake, ndiyo yaliyolifikisha shirika hilo hapo lilipo kiasi cha kushindwa kuzalisha umeme wa kutosha, hivyo kutegemea ruzuku ya serikali.
Aidha, wabunge hao walisema watendaji wa Tanesco walipopata nafasi za kuliendesha shirika hilo, walifikiria zaidi kuwapeleka watoto wao shule nje ya nchi na mambo mengine, badala ya kufikiria zaidi maendeleo ya shirika.
Wabunge hao walionyesha msimamo huo jana wakati wakichangia muswada wa umeme, uliowasilishwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Msimamo huo ni tofauti na ule waliouonyesha Februari mwaka huu, wakati walipoukataa muswada huo katika semina iliyoandaliwa na wizara kwa ajili ya kuwapatia ufafanuzi kuhusu miswada ya nishati.
Aidha, wabunge waliendelea na msimamo huo hata katika semina ya pili kuhusu miswada hiyo, iliyofanyika wiki chache zilizopita jijini Dar es Salaam.
Walikuwa wakiupinga muswada wa umeme kwa maelezo kuwa sheria hiyo itasababisha kifo kwa Tanesco, kwa kukaribisha wawekezaji binafsi wakati shirika hilo liko taabani kifedha.
Wabunge walibainisha kuwa, serikali inapaswa kwanza kuiwezesha Tanesco kuwa imara kifedha kwa sababu yenyewe (serikali) ndiyo imechangia shirika hilo kuporomoka.
Lakini kwa mshangao, tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma wakati wa semina kuhusu muswada huo ambapo wabunge wengi walitamka maneno makali kuupinga, na kuapa kutoupitisha kwa madai una lengo la kuiua Tanesco, jana wengi walionekana kuukubali na kuliponda Shirika la Tanesco.
Kabuzi Rwilomba (Busanda-CCM) ndiye aliyekuwa wa kwanza kuelekeza mashambulizi kwa Tanesco na kuusifia muswada huo, akisema kuwa awali aliupinga kwa sababu hakuuelewa vema.
Alisema kuwa muswada huo umekuja wakati muafaka na utasaidia kiasi kikubwa kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati ya umeme, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitawaliwa na Tanesco ambayo hivi sasa ipo taabani.
Rwilomba alisema kwa muda mrefu shirika hilo limekuwa likijiendesha kwa hasara pamoja na kushindwa kufikisha umeme maeneo ya vijijini, na watendaji wake wamekuwa na matumizi mabovu ya fedha zinazopatikan.
Alisema serikali imeamua kuisadia fedha Tanesco, ili iweze kujikwamua katika matatizo iliyonayo, lakini hazitakuwa na maana kama watendaji wake hawatazitumia katika maendeleo.
Rwilomba alisema historia ipo wazi kwa watendaji wa shirika hilo wanapopata fedha hufikiria zaidi kuwasomesha watoto wao nje ya nchi, badala ya kuangalia namna ya kuzalisha umeme pamoja na kuwapelekea watu wa vijijini ambao kwa muda mrefu wamekosa huduma hiyo.
"Tanesco ndugu zangu mnapobebwa na nyinyi mjibebe, fedha mtakazopewa na serikali mzitumie kuboresha shirika na wala si kwa ajili ya kujinufaisha, kwani mkifanya hivyo mtakwisha hasa baada ya kuja kwa kampuni binafsi za kuzalisha umeme," alisema Rwilomba.
Aidha, mbunge huyo aliwaonya watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), ambayo kwa mujibu wa muswada huo, ndio watakuwa na jukumu la kukubali wawekezaji katika sekta hiyo, kutoitumia fursa hiyo kujinufaisha kwa kupitisha watu wasio na uwezo kama ilivyotokea huko nyuma.
Alisema Tanzania ina historia nzuri na mifano ya wawekezaji wasio na uwezo wa kuwekeza katika sekta hiyo kiasi cha kulisababishia taifa hasara kubwa ambayo mpaka hivi sasa inaendelea kuibeba.
Mbunge mwingine aliyeishambulia Tanesco alikuwa ni Luhaga Mpina (Kisesa-CCM) aliyesema tatizo kubwa la Tanzania ni usimamizi mbovu wa sheria ambazo zinakuwa zimetungwa kwa malengo mazuri, ila utekelezaji wake ndio unaozua tafrani.
Alisema ni aibu kwa mashirika ya umma kushindwa kufanya kazi katika sekta husika ilhali mashirika ya watu binafsi yanafanya vizuri katika sekta hiyo hiyo.
Alisema kuwa ripoti ya ukaguzi wa hesabu iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha Tanesco imepata hasara ya sh bilioni 183 ambazo kama wangekuwa makini zingeweza kuwasaidia kuboresha shughuli zao.
"Hasara waliyopata hawa jamaa ni kubwa na kusingekuwapo na matatizo hayo, ingewasaidia katika shughuli zao za kila siku na kupunguza tatizo la kutegemea ruzuku," alisema Mpina.
Alisema kuna haja ya kuangalia sheria iliyoanzisha mashirika ya umma na kuifanyia marekebisho ili watendaji wake waweze kufanya kazi kulingana na sheria zitakazowekwa, kukomesha tabia ya kulegalega na kusababisha hasara ambazo zinaweza kuzuilika.
Mpina alisema mipango mingi ya mashirika hayo pamoja na ile ya serikali haitekelezwi hivyo kukwamisha shughuli za maendeleo ambazo zingekuwa na tija kwa taifa na wananchi wake katika harakati za kukuza uchumi na kuondokana na umasikini.
"Kutotekelezeka kwa mipango hii ni sawa na ufisadi kwa wananchi ambao wanahitaji huduma muhimu kama vile umeme, maji, barabara na mengineyo ili waweze kujikwamua kiuchumi," alisema Mpina.
Alisema haoni kama kweli serikali imedhamiria kuboresha huduma za umeme vijijini kwani mwaka 2007/08 zilihitajika sh trilioni 1.2, lakini zilizopitishwa ni sh bilioni 10 tu, jambo ambalo alisema ni mzaha kwa wananchi wenye kiu ya kupata umeme wa uhakika.
Naye Jeanista Mhagama, (Peramiho-CCM), alisema ni vema EWURA ikajiepusha kuwapatia leseni wawekezaji wanaotaka kuwekeza mjini pekee, kwani maeneo hayo tayari yana umeme wa uhakika.
Alishauri mamlaka hiyo iwabane wawekezaji wapya kuwekeza maeneo ya vijijini ambako kuna shida kubwa ya kutopatikana kwa umeme.
"Hapa ni lazima hawa ndugu zetu EWURA wawe macho katika leseni, hasa kwenye maeneo ya vijijini, lakini wasipofanya hivyo kuna hatari kila mwekezaji kukimbilia mjini na hivyo watu wa vijijini kuendelea na tatizo la kutokuwa na umeme wa kutosha," alisema Mhagama.
Aidha, alisema kama Tanesco watawezeshwa vizuri wanaweza kuwekeza vizuri maeneo ya mjini na karibu na wawekezaji wa sekta binafsi wapewe maeneo ya vijijini, hivyo kuwepo kwa mgawanyo wa umeme.
Awali, msemaji wa kambi ya upinzani, Mohamed Habib Mnyaa (Mkanyageni-CUF), alitoa angalizo kuhusu kifungu cha 11 cha muswada huo, ambacho kinahusu kuhamisha umiliki kwa mwekezaji.
Alisema Tanzania imepata fundisho kutoka kwa Richmond na Dowans, hivyo ni vema kifungu hicho kikawabana wawekezaji watakaoshindwa kuzalisha umeme mkataba wao uvunjwe na si kuhamisha umiliki.
"Kifungu hiki ni lazima kifanyiwe marekebisho, la sivyo tutawapa nafasi wawekezaji wasio makini kuja kuwekeza hapa nchini na kuwaacha wawekezaji makini kama ilivyofanyika kwa Dowans na Richmond," alisema Mnyaa.
Aidha, alisema pia ni vema muswada huo ukaangalia njia za kuwafanya wawekezaji wauze umeme wanaouzalisha hapahapa nchini na kutosheleza soko kabla ya kuuza nje.
Alisema hilo lisipofanyika, upo uwezekano wa kuwapata wawekezaji ambao watauza umeme wao wote nje ya nchi, hata kama kuna upungufu wa nishati hiyo nchini.
Muswada huo ulishindikana kuwasilishwa katika mkutano wa 10, baada ya wabunge kuupinga kwa nguvu zote, licha ya kufanyiwa semina elekezi.
Inaaminika kuwa imefanyika kazi kubwa ya kuwashawishi wabunge mmoja mmoja, hasa wale waliokuwa wameonyesha msimamo mkali, ili waukubali muswada huo ambao umeonekana kugusa hisia za wabunge wengi.
Wakati unaanza kujadiliwa jana, tayari wabunge 50 walikuwa wamejiandikisha kuomba kuchangia wakati miswada mingine iliyowasilishwa kwenye mkutano huu, ilikuwa ikichangiwa na wabunge chini ya saba.
[
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 3 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Wabunge kwa kawaida hawatuwakilishi wananchi tulio wachagua,wako bungeni kwaajili ya kuganga njaa zao.Hili litaendelea kuwa tatizo kubwa kwa Tanzania kama tusipowabadili na kuleta uwiano ulio sawa na wapinzani.Serekali mara nyingi inawaonga wabunge kwa kuleta semina kabla ya kupeleka miswada bungeni hivyo bunge linakuwa kama muhuri tu.
na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 19.04.08 @ 14:05 | #7410
Naungana na Kabonde kusema kwamba ni kweli wapo Wabunge wanaochangia hoja kwa ajili ya kuganga njaa na kujipendekeza. Ni hivi karibu gazeti moja lilitoa taarifa kwamba yasemekana baadhi ya Wabunge wa Viti Maalum walikuwa wamepewa mgao (hongo) na Rostam ili wampigie sana makofi atakapowasilisha hoja yake! Waswahili wanasema 'lisemwalo lipo na kama halipo laja'! Bunge letu hata lijikoshe vipi limeoza, maana wengi wa waliomo ndani ya Bunge hilo wameingia humo kwa kutumia pesa na si kwa utashi wa haki wa wananchi. Tunaomba Wabunge waweke maslahi ya nchi na ya wananchi mbele. Vinginevyo watapata laana na hukumu yao itakuwa hapa hapa duniani! Mwenyezi Mungu anayaona mateso ya wananchi kutokana na matendo ya Wabunge wa aina hiyo.
na Mswazi, dsm, - 19.04.08 @ 16:58 | #7445
KWA HIYO MJIULIZE KAMA MOTIVATION YA WABUNGE WETU NI 'INTELLECTUAL REASONING' AU 'EMOTIONAL EXPRESSIONISM'. KAMA NI 'INTELLECTUALISM', BASI HOJA HAIBADILIKI KAMA MUSWADA HAUJABADILIKA. KAMA NI 'EMOTIONALISM', SITASHANGAA WATU WAKIBADILKA BADILIKA. AFTER ALL, NI WACHACHE SANA WANAFANYA CRITICAL ANALYSIS YA KUTOSHA.