Jamani, hili jambo siyo la kufurahia kwa mtu yeyote yule mwenye hekima.
Sasa, leo humsalimii kwa mfano, Waziri wa Nishati na Madini, na inatokea kuwa jimboni kwako panahitaji umeme, Waziri anakuja pale jimboni kwako kuleta ufumbuzi JIULIZE HAYA MASWALI KISHA UTAONA KINACHOFANYIKA KUWA NI SIASA ZA WATU WA ELIMU YA CHEKECHEA.
je, utaziba mdomo?
Je hutamsalimu?
je hutamkaribisha wakati wa kuhutubia wananchi?
Je, utasema yeye ni chama tofauti na chama chako hivyo hupaswi kumsikiliza?
Je, utasema hutahudhuria kwa sababu ni chama tofauti na chako 'ukawa'
Mi naona vyama vyote vya siasa [tawala na upizani kwa ujumla wake] viache hayo maigizo ya wanafunzi wa chekechea.
Na pia, hapa tunajenga fukira finyu sana hata kwa wananchi kuelewa kuwa mtu akiwa chama tofauti na wewe huyu anakuwa ni adui.
Mi nilikuwa Tarime, miaka fulani hivi nikaona siasa kama hizo hadi katika ngazi ya familia, nilishangaa sana, nikasema kama ndiyo hivi tuendako pana giza sana mbele, ashukuliwe Mungu watu wakaona wanapotea ikabidi wabadilike kabisa.
Vyama vinapaswa viwe daraja tu ya kutuvusha kutoka mtu huyu kuwa kiongozi hadi kuleta mtu mwingine kuwa kiongozi na sio ugomvi kati ya hao viongozi wa vyama na ni jambo ambalo linaweza hamia kwa wananchi kama hatua za mapema hazitachukuliwa za kuwaelimisha hao wanaoijiita wawakilishi wa wananchi.
Kama ndiyo hivyo basi mimi naona, vyama vinakuwa vimepoteza maana na msingi wa kuwepo kwake katika jamii ya watu ya dunia ya sasa ya jamii iliyostaarabika kama hapa Tanzania.
Mfano, hadi mahusiano ya mke na mme kwa wabunge duuuh, sasa hii sio ndiyo kuleta watoto yatima katika taifa jamani?
Hebu fikili pale ambapo mbunge wa kike labda tayari kashika ujauzito si watasabisha mtoto awe yatima siku akizaliwa?
Pia, ukawa kuziba mdomo, kutoka bungeni hakuwasaidii wananchi hata tone bora wake waseme huko bugeni ili hata wakiwa na mkutano wanaweza kuwa na hoja ya msingi kuwa tulishauli wakataa, sasa leo wanaziba mdomo, wanatoka nje ya bunge hapo watasema waliwakilisha wananchi kweli?
Mambo mengine, siyo ya kuchekelea ama kukaa kimya ni ya kuwaonya watu walioshindwa kutambua wapelekapo taifa tena pasipo kuangalia wewe ni chama kipi au unatoka katika eneo gani.
Mfano, hii haimuathiri kabisaa aliyenacho ila asiyenacho ndiye ataumia kwa kauli kama hizi na vitendo hivi. Mimi nahisi tunahitaji vyama vya upinzani vipya kama mawazo na mwenendo wa vilivyopo ndiyo vinawaza hivi kama watoto wadogo.
Maana , hapa naona kama tamhthiliya fulani hivi inayoisha bila maudhui yoyote kwa mtizamaji/msomaji kuelewa chochote.
Asanteni.