Wabunge wagoma kusalimiana

Wabunge wagoma kusalimiana

Si unajua bajeti ilivyokuwa inawaumiza vichwa wabunge wa CCM kwa hiyo akawa anaomba kudesa fasta kabla hawajatoka nje. Kwa hiyo Kubenea akshtukia mchezo ikabidi amzibe mwenzake mdomo ajiekutoa majibu alafu yakionekana ya maana atajisifu baala ya kumsifu aliuempatia majibu.
kiukweli hawa wabunge wa chama hiki ni vilaza sana
 
Kitila Mkumbo amewashauri wanasiasa wa upinzani wabadilishe style ya upinzani kipindi hiki ch Magufuli.. Magufuli ni nyakati nyingine compare to JK
 
Mnafiki anapo kuja kukupa salamu za kinafiki unategemea jamaa yako alipo jirani afanye nini ndiyo kinachoonekana hapo
 
Muwatukane matusi ya nguoni ndani ya Bunge, kisha wakiwa nje mjibaraguze eti mnataka kuwasalimia!!! Ujinga wenu pelekeni mtaa wa lumumba.


Wednesday, June 22, 2016

Sakata la wabunge wa Ukawa kususa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson limefika pabaya baada ya baadhi ya wawakilishi hao kuanza kutowasalimia baadhi ya wabunge wa CCM.

Hatua hiyo ilikuwa dhahiri jana baada ya Ukawa kutangaza kuwa hawatashirikiana na wabunge wenzao wa chama tawala katika shughuli za kawaida za kijamii, kama vile michezo na kutumia kantini ya Bunge, wakisema wenzao wameanza kuwabagua.

Mbali na kitendo hicho, wabunge hao pia walitoka kimyakimya bungeni baada ya Dk Tulia kuingia, lakini safari hii hawakufanya mbwembwe za kujiziba midomo kama walivyofanya juzi.

Jana asubuhi, mbunge wa CCM Kangi Lugola alisema kuwa alisikitishwa baada ya kudai kuwa Mbunge wa Chadema (Viti Maalumu), Lucy Magereli hakumjibu salamu yake wakati akiingia bungeni licha ya kumsalimia mara tatu na kuwa katika umbali mfupi wa kusikika.

“Kusalimia ni jambo la utamaduni wetu. Nilikuwa namsalimia mbunge wa kike wa Ukawa, lakini hakujibu. Lakini, nikajua ni sababu ya wao kufunga mdomo na plasta, nikamtania au kwa sababu ya plasta hujibu ili isije kudondoka hakuitikia,” alisema Lugola.

Alisema ameshtushwa na hali ilipofikia na hajui sababu za msingi za wabunge wa Ukawa kufanya vitendo hivyo, kinyume na udugu na utamaduni wa Watanzania.

Mbunge huyo machachari, alisemaKubenea alimziba mdomo Msigwa kwa mkono ili asizungumze chochote.

Naye mbunge wa Sumve (CCM ) Richard Ndassa alisema jambo wanalolifanya wabunge wa Ukawa siyo jema na halina tija kufanywa na wawakilishi hao wa wananchi.

“Sisi ni wabunge, hivi inapofikia kususa kuongea na wabunge wenzako, hatima yake nini?” alisema.

“Mimi nilienda kuwasalimia kama kawaida ambavyo huwa tunafanya kwa wabunge awe CUF, CCM au Chadema, sasa unavyosusa una maanisha nini,”alilalamika Ndassa.

Alisema kitendo cha kutosalimia ni cha juu sana na kwamba iwapo Ukawa wanashauriwa na mtu basi inawapasa kuchuja mambo mengine, likiwamo hilo la kuwasusa wabunge wenzao.

Juzi Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia wakati anawaongoza wabunge wa Ukawa kutoka bungeni aliwatuhumu wabunge wenzao wa CCM kuwa wanawabagua

Naye Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea alisema; “Leo tumekubaliana hatutashiriki katika michezo na wabunge wa CCM, hilo tumeanza leo asubuhi kwenye mazoezi katika viwanja mbalimbali, hivi sasa tunatafakari hata kutafuta uwanja wetu.

“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,”

Kubenea alisema hata katika mechi zinazoandaliwa kwa ajili ya timu ya wabunge UKAWA hawatashiriki katika kipindi hiki cha wiki mbili zilizobakia za bajeti.

“Si katika michezo tu, hata katika mahusiano, tumekubaliana kama kuna wabunge wana mahusiano ya kimapenzi na wabunge wa CCM yasitishwe kwa muda wa wiki mbili mpaka tutakavyoamua vinginevyo,” alisema Kubenea.
 
Wao ukawa wakitaka wakomeshe zaidi watembee bila nguo hiyo itakuwa nzuri zaidi.
 
mwisho itafikia wataanza kuwekeana na sumu kwenye vyakula ,hili jambo sio dogo kihivyo
 
ata mimi ccm sishirikiani nao toka walipomuua Mawazo..ata akifa mtu wa ccm mtaa wa pili siendi..na mm nikivuta wasije
 
sentensi ya mwisho inasema "UKAWA MANA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA CCM". Jamani kumbe ndivyo mfanyavyo muwapo bungeni!, ndio maana wabunge wakiume wa CCM wanawasilimia sana wabunge wa kike wa UKAWA and viceversa imegundulika. Kama bunge lisemapo kuwa WANACHUO wanajiuza, makahaba etc sasa tutasema WABUNGE wanajiuza, makahaba etc ili iwe sawasawa, tofauti hapo naona ni HADHI YA UKAHABA, HADHI YA KUJIUZA
 
Acha wapitane kimya tu maana ni dhambi kusalimiana na msaliti wa wananchi kwa kupitisha vitu kutoka mhimili mwingine.
 
Kama mtu anakudharau una haja gani ya kujipendekeza kumsalimia?
Mwasisi wa kejeli na dharau ndio mwenye say na kila kitu.
Poa tu.Ila isifikie kwa wanachama kwanza.!!
Wanachama wataiga kutoka kwa kitendo wanachofanya viongozi wao,wao wapinzania wanadhani wanamkumoa madame spika kumbe wanajikomoa wenyewe na wao ndio wameanza kupandikiza mbegu za chuki na tabia mbaya ,sidhani mtu kama mimi ambaye ndie mpiga kura kususa kwao kunanisaidia kitu ,hapa wanaoumia sio CCM na serikali yake bali wapiga kura majimboni,na sasa ndio tunajua kwamba mpiga kura hana haki na mbunge wake bali viongozi wa vyama ndiowana haki na hao wabunge..
 
Si unajua bajeti ilivyokuwa inawaumiza vichwa wabunge wa CCM kwa hiyo akawa anaomba kudesa fasta kabla hawajatoka nje. Kwa hiyo Kubenea akshtukia mchezo ikabidi amzibe mwenzake mdomo ajiekutoa majibu alafu yakionekana ya maana atajisifu baala ya kumsifu aliuempatia majibu.

...kumbe alikuwa anamuomba Mh Msigwa amjazie majibu kwenye karatasi...hihihihihihihihi...
 
Back
Top Bottom