Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,716
- 46,432
Ukiwasikiliza wabunge asilimia 99 wakati wanachangia bajeti ya wizara ya elimu ni kama hawafahamu vizuri mzizi wa matatizo ya elimu nchi hii. Wengi wanazungumzia vitu vyepesi sana
Kuwasadia kwa uchache haya ni baadhi ya matatizo makubwa hasa katika shule na vyuo vya serikali;
1. Upungufu mkubwa wa walimu na wakufunzi unaosababisha ufundishaji duni.
2. Uhaba wa madarasa unaosababisha mrundikano wa wanafunzi darasani.
3. Kukosekana kwa chakula shuleni; watoto wanaosoma na njaa watatoka vilaza tu
4. Umbali mrefu kufika shule; Kuna wanafunzi wanavizia lifti kila siku kwenda shule!
5. Uhaba wa vitabu; kila mtoto anatakiwa awe na kitabu chake mwenyewe katika kila somo.
6. Maslahi duni kwa walimu, ili watu wafanye kazi yao vizuri wanahitaji motisha.
7. Vyuo vikuu kushuka ubora. Vimegeuka sehemu za kukariri na kupata vyeti tu badala ya sehemu za midahalo, "critical thinking" na kuzalisha mawazo mapya.
Jikiteni humu badala ya kulalamikia lugha, kutaka kusoma masters bila kufanya mtihani wa kidato cha nne, elimu ya ujasiriamali n.k