Wabunge waache kuendekeza vitendo vya uvunjaji wa sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge waache kuendekeza vitendo vya uvunjaji wa sheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pdidy, Jun 1, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,343
  Likes Received: 3,230
  Trophy Points: 280
  Wabunge waache kuendekeza vitendo vya uvunjaji wa sheria

  Na Mhariri
  29th May 2009


  Jana vyombo kadha vya habari, viliripoti habari zikiwanukuu baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Fedha na Uchumi wakieleza hofu yao kuhusiana na hatua ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuidhibiti Taasisi ya upatu ya Development Entrepreniurship Community Initiatives (Deci).

  Wabunge hao walisema kuwa uamuzi wa kuidhibiti taasisi hiyo, utawaweka wao (Wabunge) katika hali ngumu ya kisiasa katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka ujao.

  Walijenga hoja yao iliyoonekana ikilenga kuwashawishi maofisa waandamizi wa BoT juzi wakati walipokutana nao kupokea ripoti ya mwelekeo wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2009/2010, ili walegeze msimamo wao dhidi ya Deci.

  Kimsingi, wabunge hao wengi kutoka chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitoa hoja hiyo ili wao na chama chao waonekane kuwa wanawajali Watanzania.
  Kitendo hicho tunakichukulia kuwa baadhi ya Wabunge wanashindwa kutekeleza majukumu yao waliyopewa na Katiba ya nchi ya kushauri, kufuatilia na kukosoa utendaji mbovu wa serikali.

  Tunashindwa kuelewa inakuwaje Wabunge wakadiriki kuingilia kati kutetea watuhumiwa wa kuvunja sheria za nchi wasichukuliwe hatua na taasisi husika kwa kutumia kisingizio cha Uchaguzi Mkuu wa mwakani?

  Taarifa zilizoko ni kwamba Deci ilikuwa inaendesha shughuli zake kinyume cha sheria na shughuli hizo zikasimamishwa na serikali baada ya kubainika kuwa wananchi wengi wamepoteza fedha zao katika upatu.

  Tusingependa kunukuu maneno yaliyotolewa na baadhi ya Wabunge hao walioonyesha kukerwa na hatua ya BoT, lakini Wabunge, tena wale ambao ni wajumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi, badala ya kuibebesha lawama BoT kwa kushindwa kusimamisha shughuli za Deci mapema, nao walikuwa na jukumu la kuihoji serikali baada ya kuona shughuli za Deci zikiendelea.

  Kwa kuwa Wabunge wanaishi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, bila shaka waliwaona wananchi wao wakishiriki katika upatu huo lakini hawakuchukua hatua za kuwapa tahadhali. Kwa hiyo kama ni lawama za kutokuwajibika kwa kutotoa taarifa basi hawawezi kujivua lawama hizo.

  Kwa kuwa BoT imeingilia kati kwa ajili ya kuokoa fedha za wananchi hata kama imechelewa kuchukua hatua lakini ni jambo la busara kwa Wabunge kuliacha suala hilo kwa taasisi hiyo ambayo jukumu lake kubwa ni kusimamia mambo yote ya fedha nchini.

  Tunawashauri Wabunge kuacha kutetea shughuli za Deci kwa kuhofia kushindwa katika uchaguzi wa mwakani bali waliache suala hilo kwa BoT na vyombo vya sheria. Wanaopaswa kulihofia hilo ni wale waliohusika kwa njia moja ama nyingine kuwashawishi wapigakura wao kujiunga katika upatu huo.

  Kwa bahati mbaya imejengeka tabia mbaya kwa watu walioko katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini kuweka pembeni sheria badala yake kutetea vitendo vya uvunjaji wa sheria hasa unapofika wakati wa uchaguzi kwa lengo la kujifanya kuwa wanawajali wananchi.

  Kwa mfano, katika maeneo mengi ya mijiji, shughuli za biashara ambazo zinachafua mazingira zimerejea upya na ya viongozi wanasita kuchukua hatua wakidai wahusika waachwe kwa kuwa uchaguzi unakaribia.

  Tunawashauri viongozi katika ngazi zote, wakiwemo Wabunge wetu kutekeleza wajibu wao kwa dhati bila kuhofia kwamba uchaguzi mkuu unakaribia kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka wajibu na ni kinyume cha utawala wa sheria.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,351
  Likes Received: 1,026
  Trophy Points: 280
  Huenda baadhi yao walikuwa wamepanda huko DECI?
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ndio maana yake au? kwanini ute-te kitu ambacho unajua mwisho wake si mzuri. ndio uenda DECI inge last for long considering the number of its participants the whole thing depends on new members, through the reports it appears its was never shot of them. this meant those running the scheme were getting reach through the back of walalahoi tatizo hawa watu ni wagumu wa kuelewa kwamba itafika siku wengine wata kosa kwa sababu jamaa wana chukua faida na wanalipa kwa faida kwa maana amna hela inayo zalishwa nje member wanavyozidi muda wa malipo nao una zidi memba's wa kiisha wengi watalia ni bora tahadhari kabla ya hatari embu wajaribu kuwaambia DECI warudishe hela yao kama wote watapata kitu. alafu unakuta mtu anatetea kama ni mmbuge hapati kura kwa sababu anitakii mema.
   
 4. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,124
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hili ndilo tatizo la wanasiasa uchwara,wanajua fika kuwa DECI ilikuwa kinyume na sheria na ni UTAPERI,Kwa kuwa wengi wa waathirika wa DECI syndrome ni Masikini walioko kwenye majimbo yao na niwapiga kura anafumba macho dhidi ya yote ayajuayo kuwa ni mabaya na kuangalia namna ya kujipendekeza kwa wapiga kura,Hii ndiyo inayo fanya watu wahalarishe USHOGA,UTOAJI mimba nk.ili tu apate kura toka makundi husika,DECI iliingizwa kuziba pengo la kukosekana mipango mizuri ya kuwaelimisha wananchi (Wapiga kura) namna ya kuendesha maisha yao kwa shughuli halali,Jukumu la kuweka chachu kwa wananchi ili waendeshe maisha yao na kupigina na umasikini liko mikononi mwa Viongozi,Wabunge wakiwa ni sehemu ya hao vingozi,Baada ya kushindwa kwao kukawa na pengo ambalo wajanja waliliona na kuanzisha DECI kuliziba kwa muda kwa manufaa binafsi.Wabunge wanayo haki ya kuogopa kufutwa kwa DECI kwani hawana mbadala kwa wapiga kula wao
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,099
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hivi jamani hawa ni aina gani ya wawakilishi wa wananchi katika kusimamia serikali????

  jamani mara kwa mara nimekuwa nikishangazwa na uwezo mdogo wa wabunge katika kujenga hoja na kuishia kuwa watu wa kubabaisha na kudhalilisha nafasi zao..

  ama kwa hakika tuna safari ndefuu ya kuelekea kwenye maendeleo ya kweli kidemokrasiaa....cheap popularity....yale yale mpaka leo siwezi kuamini wabunge wa CCM wanaopiga kelele za ufisadi kwani ni WANAFIKI WAKUBWA...

  Imejengeka miongoni mwao wengi kuwa kushinda UBUNGE NI KUWA MGOMBEA NDANI YA CHAMA CHA MAFISADIIII...DR SLAA AMEONYESHA NJIA..

  Huwezi ukatenda tofauti na dhamira yako kwa muda urefuu bali utaishia kuwa mnafiki kwa masilahi ya kupita..

  siwashangai kuililia DECI...
   
Loading...