Wabunge wa UKAWA wafanya kikao kizito MIC Hotel

Kilityme

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
218
574
Salaam Wanabodi,
Kikao kizito cha wabunge wa Ukawa kinaendelea mpaka sasa eneo la ubungo ndani ya Mic hotel.

Ajenda nzito zinahusu hoja za kuibana Serikali kuhusu watuhumiwa wa Escrow waliorudishwa Serikalini na pia mustabali wa Zanzibar.

Kikao kinaongozwa na Edward Lowassa na mbowe.

Haya utamu wa bunge huo unakuja.
 
Last edited by a moderator:
Salaam Wanabodi,
Kikao kizito cha wabunge wa Ukawa kinaendelea mpaka sasa eneo la ubungo ndani ya Mic hotel.

Ajenda nzito zinahusu hoja za kuibana serikali kuhusu watuhumiwa wa escrow waliorudishwa serikalini na pia mustabali wa Zanzibar.

Kikao kinaongozwa na Edward Lowassa na mbowe.

Haya utamu wa bunge huo unakuja.
Suala la Escrow hilo wataadhirika sana wao labda waiombe Serikali kuhusu Zanzibar.
 
Last edited by a moderator:
Wamekosa cha kufanya kama ajenda zenyewe ndio hizo mimi nilifikiri wataongelea changamoto za utekelezaji wa mambo kama ya elimu bure kweli nimeamini ukawa ni wanaharakati sio wanasiasa.
 
Last edited by a moderator:
Ah nilifikiri bomoa bomoa kumbe escrow? Safari hii watatumia tochi kutafuta kasoro
Una akili wewe gharama ya maisha ipo juu mtaani huoni kama ni tatizo?

Mafuta soko la dunia yamedorora ila hapa kwetu gharama ziko juu

Shilingi imeshuka thamani siku hadi siku hiyo ni sawa.

Mahospitalini dawa bado tatizo hiyo ni kasoro.

Serikali hii haina nia muda mipango kwenye kilimo hilo ni kosa.

Mapato yanakusanywa pesa za miradi hazijafaka mpaka sasa hiyo ni kasoro.

Elimu bure labda kwenu huko mjini huku vijijini watu wanachangishwa mpaka mbuzi na ng'ombe HIYO BURE IKO WAPI kuongea ni kila mtu anaweza ila kutenda ni mtihani sana.

Mgogoro wa zanzibar
Bado Serikali yetu hainaonesha nia ya dhati kuutatua au kuumaliza amicably.

Serikali iliahidi kwa wafanyakazi kuwa itaondoa kodi pindi tu ikiingia madarakani lakin mpaka sasa ni bado na sidhan kama Serikali ina mpango huo.

Swala la umeme
Akiwa Arusha alisema nyie Tanesco nimewagundua mnafanya sabotage ili nishindwe nikose kura.

Sasa nawaambia nikishinda naanza na nyie ila yaliishia kama maneno.

Swala la mikopo

Akiwa Moshi alisema natambua Magufuli club mnavyonipigania na mimi sintowaacha pesa zenu na mikopo atakae zichelewesha ntampandilia hukohuko nikamkopoe ila sasa kwa taarifa hii ni wiki ya 10 pesa hazijaingia
 
Last edited by a moderator:
Magufuli hawezi kuua Upinzani kamwe. ameanza vibaya katika mengi. mfano kuteua wezi wa Escrow katika nyadhifa mbalimbali.
 
Last edited by a moderator:
Mpaka watapopeleka hoja ya kutaka majina ya waliochukua fedha za ESCROW kwa malumbesa yatajwe ndio nitawachukulia siriaz,zaidi ya hapo nitawaona kama wahuni tu.
Salaam Wanabodi,
Kikao kizito cha wabunge wa Ukawa kinaendelea mpaka sasa eneo la ubungo ndani ya Mic hotel.

Ajenda nzito zinahusu hoja za kuibana serikali kuhusu watuhumiwa wa escrow waliorudishwa serikalini na pia mustabali wa Zanzibar.

Kikao kinaongozwa na Edward Lowassa na mbowe.

Haya utamu wa bunge huo unakuja.
 
Salaam Wanabodi,
Kikao kizito cha wabunge wa Ukawa kinaendelea mpaka sasa eneo la ubungo ndani ya Mic hotel.

Ajenda nzito zinahusu hoja za kuibana serikali kuhusu watuhumiwa wa escrow waliorudishwa serikalini na pia mustabali wa Zanzibar.

Kikao kinaongozwa na Edward Lowassa na mbowe.

Haya utamu wa bunge huo unakuja.
Hamna picha ili tuone hicho kikao?
 
Kama kuna kipindi ambacho Tanzania inahitaji "upinzani imara" ni kipindi hiki cha 2015 - 2020.Hii ni kutokana na aina ya Utawala ambao JPM na Serikali wanautumia (MBC - Management By Crisis) ambao unaambatana na ziara za kustukiza sambamba na maigizo yenye maagizo mbele ya vyombo vya habari.
 
Hamna anayehangaika na ukawa, watu wako bize na jpm
 
maghufuli hawezi ua upinzani kamwe. ameanza vibaya katika mengi. mfano kuteua wezi wa escrow katika nyadhifa mbalimbali...
Kama tu Lowassa alivyo chaguliwa kuwania urais na CHADEMA.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom