Wabunge wa CCM waliopanga kumuona Lema gerezani waonywa, waitwa wasaliti

huyu raisi ni waajabu sana sasa kama wewe ni chadema na mkeo ni ccm unambagua haya mambo ni yale ya warundi na wanyarwanda

hopeless kabisa
Mkuu ni kweli lakini tumekuwa masikini wa akili hadi foreign mentality ya Hima imeshika madaraka.

R.I.P Mtikila
 
Rais John P Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliounda kamati kwenda gereza la Kisongo kumtembelea Lema.

Hii si sawa, badala ya rais kutuunganisha Watanzania anazidi kutugawa.

Kiongozi anayeongoza kwa visasi na chuki hatufai hata kama ni rais, ingawa hatuwezi kumfanya kitu lakini sisi ni watu wazima anapopotoka lazima tuseme.

Amewaonya pia wabunge wa CCM wanaogawa muda wao wa kuchangia kwa wapinzani, rais hujui kuwa nchi hii ni yetu sote na wote tuna jukumu la kuijenga, kama wabunge wanatoka sehemu mmoja na tatizo lao ni moja, maji, kuna ubaya gani kumwachia mbunge mwenzako kulizungumzia, huko unakotuelekeza siko Mh rais.

Watanzania ni wakarimu, wapole, tunasaidiana kwenye matatizo, ugonjwa, misiba, harusi na kadhalika, sasa wewe kama kiongozi wa familia unapozuia watoto wasifarijiane, wasitembeleane unafanya kosa, mwisho utazuia watu wasizikane kwa tofauti za itikadi zao.

Kwa hili la kuwazuia wabunge wa CCM wasimtembelee Lema rais umekosea, kumbuka jamii tunamoishi tumechanganyika familia moja inaweza kuwa na wanachama wa CCM, CUF, Chadema, NCCR, ACT Wazalendo nk.

Tukosoane kwa hoja tusitukanane.
 
Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni.

Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.

Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.

======================

Hii ni dalili ya Taifa linalojengwa katikati ya chuki ma uhasama.Taifa la visasi na kukomoana.Unaposikia Rais anawalaumu wabunge wa chama chake kumtembelea mbunge mwenzao wa chama kingine gerezani,unapata picha ya nini na nani anaweza kuwa nyuma ya mbunge husika kuwa gerezani.

Hii inakatisha tamaa,inaondoa moyo wa uaminifu hata kwa sie wachache ambao tulikuwa upande wa Rais ktk baadhi ya mambo anayoyasimamia.Kwa kauli hizi,Rais na mkuu wetu anatukatisha tamaa sana sana.

Unaposikia kauli za chuki kiasi hiki,unajiuliza pale mtu anapokuwa anataka aombewe,aombewe kwa minajili ya kuzidisha chuki na mtangamano au?

Rais mara nyingi husema yeye ni wa wote;maendeleo hayana chama,tudumishe amani na upendo maana Tanzania ni moja,lakini Tanzania itakuwa moja kwa mtindo huu wa kupandikiziana chuki na kutishana??

Tuzidi kuliombea Taifa.Na wengine tunazidi kukata tamaa.Mungu saidia.

CHANZO:
Gazeti la Mwananchi.
Mbunge wa viti maalum anayevujisha siri ni binti bulembo ndio maana baba yake kaambiwa amkanye mwanae.
 
Daaaahhh aisee hivi bunge si muhimili huru au ??sasa wabunge wanatawaliwa na wenyewe kila kitu kimekuwa uvundoo mtupu kwahyo ile juzi zile ngumi mtu kukatisha eneo la ccm mkulu ndio anapenda vile
 
Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni.

Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.

Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi.

======================

Hii ni dalili ya Taifa linalojengwa katikati ya chuki ma uhasama.Taifa la visasi na kukomoana.Unaposikia Rais anawalaumu wabunge wa chama chake kumtembelea mbunge mwenzao wa chama kingine gerezani,unapata picha ya nini na nani anaweza kuwa nyuma ya mbunge husika kuwa gerezani.

Hii inakatisha tamaa,inaondoa moyo wa uaminifu hata kwa sie wachache ambao tulikuwa upande wa Rais ktk baadhi ya mambo anayoyasimamia.Kwa kauli hizi,Rais na mkuu wetu anatukatisha tamaa sana sana.

Unaposikia kauli za chuki kiasi hiki,unajiuliza pale mtu anapokuwa anataka aombewe,aombewe kwa minajili ya kuzidisha chuki na mtangamano au?

Rais mara nyingi husema yeye ni wa wote;maendeleo hayana chama,tudumishe amani na upendo maana Tanzania ni moja,lakini Tanzania itakuwa moja kwa mtindo huu wa kupandikiziana chuki na kutishana??

Tuzidi kuliombea Taifa.Na wengine tunazidi kukata tamaa.Mungu saidia.
IMG-20170314-WA0010.jpg
Hii hapa
 
Cc,kwa wote mnao sema kua anayo nia nzuro ma taifa hili.hado hado hu lugendoo.

Baba wa taifa alishasema kwa katiba hii akipatikana asiye na busara......
 
Asubuhi wakati nawasha Tv nilikutana na hii habari kwenye kipindi cha magazeti kwamba Mh.Rais hakupendezwa namna Mbunge mmoja wa chama chake alivyompa mda wa maongezi mbunge wa upinzani bungeni, na eti kuna wabunge wa chama chake ambao walipanga kwenda kumtembelea Lema alipokuwa Gerezani eti nayo hakuipenda na ni usaliti...Nilijuliza Maswali mengi sana sijapata majibu..
1.Hivi Mh.Rais wabunge wa Ccm na Upinzani kutembeleana wakati wa matatatizo ni dhambi?
2. Hivi Leo Mfano Kuna Mbunge wa Chadema yupo gerezani akienda kutembelewa na mbunge wa ccm wewe inakupunguzia nini kwenye uongozi wako au inakuongezea nini?
3. Hivi Mh.Kikwete Licha ya kutukanwa kote kule lakini bado alidiriki kuwaita wapinzani ikulu na kunywa nao Juice kwa hiyo tuseme Kikwete alikuwa msaliti kwa chama chake? Kweli Mh. Rais tumefika hatua hii? Mh.Rais wakati unapokuwa kwenye maombi yako binafsi mda mwingine Muombe sana Mwenyezi Mungu akujalie Hekima za Mfalme Sulemain....na mda mwingine kabla hujaanza kuzungumza mahali popote muombe Mungu akupe kibali cha kuzungumza kwa uwezo wa roho mtakatifu .... leo nilivyosikia hii habari imenihuzunisha sana...Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom