barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni.
Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.
Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.
Rais amewaambia wabunge wa CCM kuwa yeye ndio aliyekataza bunge lisionakene "live" (mubashara)
[/COLOR][/SIZE][/FONT]
CHANZO: Gazeti la Mwananchi.
======================
Hii ni dalili ya Taifa linalojengwa katikati ya chuki ma uhasama.Taifa la visasi na kukomoana.Unaposikia Rais anawalaumu wabunge wa chama chake kumtembelea mbunge mwenzao wa chama kingine gerezani,unapata picha ya nini na nani anaweza kuwa nyuma ya mbunge husika kuwa gerezani.
Hii inakatisha tamaa,inaondoa moyo wa uaminifu hata kwa sie wachache ambao tulikuwa upande wa Rais ktk baadhi ya mambo anayoyasimamia.Kwa kauli hizi,Rais na mkuu wetu anatukatisha tamaa sana sana.
Unaposikia kauli za chuki kiasi hiki,unajiuliza pale mtu anapokuwa anataka aombewe,aombewe kwa minajili ya kuzidisha chuki na mtangamano au?
Rais mara nyingi husema yeye ni wa wote;maendeleo hayana chama,tudumishe amani na upendo maana Tanzania ni moja,lakini Tanzania itakuwa moja kwa mtindo huu wa kupandikiziana chuki na kutishana??
Tuzidi kuliombea Taifa.Na wengine tunazidi kukata tamaa.Mungu saidia.