Wabunge wa CCM waliopanga kumuona Lema gerezani waonywa, waitwa wasaliti

NI NGUMU KUAMINI. FIKRA YA KUWA KILA ALIYENAHATIA AU ANAYETUUMIWA NA UVUNJAJI WA SHERIA NI ADUI KAMA MUUAJI SI FIKRA NZURI.
TUPUNGUZE HIZI CHUKI ZITATUGHARIMU.
 
Rais Magufuli amewatisha wabunge CCM kwa kuwaonya vikali, amewashutumu wabunge hao kwa kutoa siri za CCM kwa upinzani na hata kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni.

Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM.

Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye,wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.

CHANZO: Gazeti la Mwananchi.

======================

Hii ni dalili ya Taifa linalojengwa katikati ya chuki ma uhasama.Taifa la visasi na kukomoana.Unaposikia Rais anawalaumu wabunge wa chama chake kumtembelea mbunge mwenzao wa chama kingine gerezani,unapata picha ya nini na nani anaweza kuwa nyuma ya mbunge husika kuwa gerezani.

Hii inakatisha tamaa,inaondoa moyo wa uaminifu hata kwa sie wachache ambao tulikuwa upande wa Rais ktk baadhi ya mambo anayoyasimamia.Kwa kauli hizi,Rais na mkuu wetu anatukatisha tamaa sana sana.

Unaposikia kauli za chuki kiasi hiki,unajiuliza pale mtu anapokuwa anataka aombewe,aombewe kwa minajili ya kuzidisha chuki na mtangamano au?

Rais mara nyingi husema yeye ni wa wote;maendeleo hayana chama,tudumishe amani na upendo maana Tanzania ni moja,lakini Tanzania itakuwa moja kwa mtindo huu wa kupandikiziana chuki na kutishana??

Tuzidi kuliombea Taifa.Na wengine tunazidi kukata tamaa.Mungu saidia.
Anawatrain wabunge wa CCM wajione there is nothing to loose. Ila Ukimlea mtoto vibaya,baada ya kukosa pa kuiba nje au huko nje wakianza choma moto tuu.Huyo mwizi hurudi nyumbani.
 
Wewe huwezi amini mh raisi akiwa kwenye hafla ya nmb aliwaasa wa tz wasiweke pesa benki nyingine zote ila nmb maana serikali ina hisa asilimia 31 so hela zoote tuweke nmb na benki nyingine tuweke 0.001% ya hela zetu ili hela zikienda nmb serikali itapata gawio la hisa na hisa zitasaidia wananchi. Je is that a presidential speech? Je anaona raha bank nyingine zikifa?, na je nn madhara kwa bank nyingine kufa , kwa taifa na kwa serikali? Je huyu ni raisi wa nmb tu? Bank nyongine wanajisikiaje wanaposikia mkuu wa nchi anelekeza taasisi zoooote za serikali zisiweke pesa au kufanya biashara na bank za biashara wanajisikiaje? ukizingatia mchango wao mkubwa sana wa kimaendeleo ktk uchumu wa nchi yetu? HUYO NDO RAISI. LIKE FATHER LIKE SON. Asanteni
 
Rais Magufuli amewaonya vikali wabunge wa CCM kwa kuwagawia wabunge wa upinzani muda wa maongezi bungeni. Pia Magufuli amewaonya wabunge wa CCM waliokuwa wamepanga kumtembelea mbunge mwenzao Godbless Lema gerezani na ameita kitendo hicho kama usaliti mkubwa kwa CCM. Na mwisho JPM amewapa somo, kwamba anajua kuna njama za kumwondoa Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwa kutokuwa na imani naye, NA KWAMBA wakishiriki kwenye mipango hiyo atalirejesha jina la Majaliwa kwa mara ya pili na bunge likilikataa atalivunja na nchi irudi kwenye uchaguzi wa nafasi zote.
CHANZO: Gazeti la Mwananchi.
[HASHTAG]#Your[/HASHTAG] take?
 
...wengine wanadhani suala ni kuisoma namba....hapana, ni zaidi ya kuisoma namba. My laugh comes last!
 
Mtu yeyote anayeficha asili yake na kujifichia kwenye kabila kubwa lazima ufahmu si wa kawaida.

Lawama zote zimuendee kikweti na familia yake kwa kuangamiza taifa ajili tu ya tamaa zao binafsi za uongozi hata kama hawana uwezo. Haya ndiyo matunda ya uongozi wake. Hovyo hovyo tu!
Kweli kabisa hapa namlaumu kikwete kwa kutuletea mtu wa hovyo kama huyu.
 
Mpaka muda wa maongezi anajua huwa wanapeana? Simu na mawasiliano ya wabunge yako salama kiasi gani? Yanaingiliwa?

Misibani je? Tusihudhurie?

Nimeona Facebook page ya upendo peneza akisema alikuwa msindikizaji kwenye harusi ya Lucy mayenga,mwana ccm,Lucy Mayenga naye msaliti?

Tuchukiane?

Now its your turn ccm members

hapana, anamaanisha kuna mbunge wa ccm alimpa mbunge wa upinzai dakika zake za kuongea bungeni basi ndiyo imemuuma sana mwenyekiti huyu wa CCM anayetangaza chuki dhidi ya wabunge wa upinzani.
 
Bunge lipo ktk kipindi kigumu ama likubali liwe rubber stamp ya serikali na kwa hivyo kupoteza heshima na umuhimu wake ama lisimame kama mhimili unaojitegemea hivyo kukutana na hasira za Rais, uamuzi ni wenu wabunge.
 
Everything kuhusu upinzani kwake nibatili. Labda nimkumbushe.. nchi zilizoendelea... upinzani hamaanishi kuwa ndio adui wa nchi...
Sasa yeye anachukulia upinzani ni adui wa nchi
Hapo ndipo huwa nashindwa kumuelewa muheshimiwa ........... kila siku anadai kuwa maendeleo hayana chama na yeye ni Rais wa wote bila kujali itikadi.

Kwa kweli maneno na vitendo ni tofauti kabisa!!! Tumeyaona haya kwenye ziara zake ............ Ziara za Serikali zimekaa kichama chama!!
 
Back
Top Bottom