Wabunge wa CCM wakutana saa saba, watambeba Ngeleja?

Jaxx

Senior Member
Mar 22, 2011
129
28
Tangazo la speaker wa Bunge limetia fola baada ya bunge kulindima kwa vicheko juu ya wabunge wote kuonana hali kukiwa na kila dalili kuwa budget ya Wizara ya Nishati na Madini haitapita. Hali hiyo inaashiria kuwa wabunge wanataka kuwekwa sawa (Kusetiwa) ili wakati wa kupitisha budget wawe ''RUBBER STAMP'' ya ''SIRIKALI''.

My intake; Wabunge wa CCM msikubali kubeba haibu hii!!
 
Every man/woman should fend for him/herself. CCM wapitishe hii Budget ya Ngeleja waone hasira ya Watanzania. Hawatarudi bungeni 2015.
 
Yaaani Nimekasirika sana nilivyosikia hilo Tangazo la Spika!!!
Hivi hii Nchi nani Katuroga??, Argggghhhhhhhhhh
 
Wabunge wa CHADEMA wajipange vizuri na kama ilivyokuwa kwa hoja ya posho hapa napo CHADEMA wanaweza kuunika 'unafiki' wa ccm. Miaka nenda rudi ccm wanaongea lakini hawatekelezi, na hata huu ukali wa baadhi ya wabunge wa ccm kuhusu umeme ni 'janja' yao ili waonekane wanasimamia maslahi ya Watanzania. Wanataka wafunike debate ili CHADEMA wasionekane kwenye umeme. Walikuwa wapi hawa ccm mpaka nchi ikaingia kwenye giza? CHADEMA waanikeni hawa!
 
Yaaani Nimekasirika sana nilivyosikia hilo Tangazo la Spika!!!
Hivi hii Nchi nani Katuroga??, Argggghhhhhhhhhh
Mpaka Mh Speaker kaona haibu ikabidi atumie mfano wa Wabunge wa CDM kukutana kuwa imekuwa ni utaratibu wa kawaida. Cha ajabu wabunge wote wamecheka maana wanajua nini kitaendelea huko kikaoni maana wanajua diyo wanaenda kuigawana ile 1,000,000,000(Bil 1) iliyotoka kwenye idara za Wizara ya Nishati na Madini
 
Na tusubiri hiyo jioni tuone MBIVU na MBICHI, lkn kwa CCM wataipitisha tu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Yaaani Nimekasirika sana nilivyosikia hilo Tangazo la Spika!!!
Hivi hii Nchi nani Katuroga??, Argggghhhhhhhhhh
Mkuu tulishindwa kuiondoa CCM madarakani mwaka jana, matokeo yake ndiyo haya leo hii rais aliyeko madarakani anakwambia tatizo la umeme ni "Mother Nature" what do you expect???
 
Nawashauri wabunge wa upinzani wa upinzani endapo CCM watataka kupitisha bajeti hii, mto nje wala utaratibu wa kura msiukubali
 
Na tusubiri hiyo jioni tuone MBIVU na MBICHI, lkn kwa CCM wataipitisha tu.

Tuone kama kweli CCM wana ujasiri kiasi gani jioni hii. Watayasimamia waliyosema au watakula matapishi?
 
hatuna umeme makwetu, mgao usio na ratiba unaendelea....ntasubiri taarifa kwenye magazeti.
 
Mpaka Mh Speaker kaona haibu ikabidi atumie mfano wa Wabunge wa CDM kukutana kuwa imekuwa ni utaratibu wa kawaida. Cha ajabu wabunge wote wamecheka maana wanajua nini kitaendelea huko kikaoni maana wanajua diyo wanaenda kuigawana ile 1,000,000,000(Bil 1) iliyotoka kwenye idara za Wizara ya Nishati na Madini
Ni kweli hapo umenena, ngoja tuone . Ila ushauri wangu wabunge wote wa CHADEMA ikiwezekana watoke nje ya Bunge ili kuweka msisitizo zaidi.
 
Wabunge wa CCM wanajipanga kama kamati kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati.

Umeme ni swala la kitaifa.Sio la CHADEMa wala CCM. Chonde wana CCM,ndayi ni watanzania.Kwanini mkubali ndugu zenu baba zenu,mama zenu,ndugu zenu na majrani zenu wakae gizani kwa nyinyi kupata umaarufu kwa Chama?? Cheo ni dhamana! Unaposimamia jambo la kitaifa kwa moyo Watanzania watakupatia 'CREDIT'

Please,Tuwe waungwana kwa swala la umeme!
 
Ndugu zangu nimefuatilia mjadala wa bajeti ya wizara na madini leo hii asubuhi wa nishati na madini, Japokuwa wachangiaji wengi walikuwa wa Chama tawala cha CCM wengi wamekataa katu kwamba hawaungi mkono bajeti hiyo kwa hiyo isipitishwe. Kinachonifurahisha hapa ni naman ambavyo wabunge wa CCM wameachikia mbali itikadi zao za chama chao na kuamua kulivalia njuga jambo hilo. Baada ya bunge kumalizika spika Anne Makinda ametangaza wabunge wote wa CCM wakutane ukumbi wa Msekwa kikao ambacho mpaka sasa kinaendelea, ninachowashauri wabunge wa CCM ni kwamba wasifanye uamuzi wowote wa kutaka kuipitisha bajeti hii kinyemela wajue watakuwa wamevunja imani yao kwa wananchi na kamwe hatutawaunga mkono kwa hili, tuko tayari kuingia mitaani. Itakuwa ni aibu kubwa sana kwa Wabunge wa CCM kuonesha ujasiri mkubwa wa kutetea masilahi ya taifa kikao cha asubuhi hlf jioni waje watugeuke. Hoja hii sio ya kisiasa wekeni masilahi ya Taifa mbele na hima mhimizeni waziri Ngereja ajiuzuru na apumzike kwa amani. ASANTENI SANA, MWACHENI NGEREJA APUMZIKE KWA AMANI

Wana JF mnalionaje hili?
 
Wabunge wa CCM wanajipanga kama kamati kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati.

Umeme ni swala la kitaifa.Sio la CHADEMa wala CCM. Chonde wana CCM,ndayi ni watanzania.Kwanini mkubali ndugu zenu baba zenu,mama zenu,ndugu zenu na majrani zenu wakae gizani kwa nyinyi kupata umaarufu kwa Chama?? Cheo ni dhamana! Unaposimamia jambo la kitaifa kwa moyo Watanzania watakupatia 'CREDIT'

Please,Tuwe waungwana kwa swala la umeme!

Tusiwabembeleze wacha ili 2015 ile kwao tena
 
Tangazo la speaker wa Bunge limetia fola baada ya bunge kulindima kwa vicheko juu ya wabunge wote kuonana hali kukiwa na kila dalili kuwa budget ya Wizara ya Nishati na Madini haitapita. Hali hiyo inaashiria kuwa wabunge wanataka kuwekwa swa( Kusetiwa) ili wakati wa kupitisha budget wawe ''RUBBER STAMP'' ya ''SIRIKALI''.
My intake; Wabunge wa CCM msikubalu kubeba haibu hii!!

kama hawa wabunge wa ccm wataenda kujipanga au kushurutishwa ili kuipitisha bajeti ya wizara ya nishati na madini ukizingatia hoja zao walizotoa kwa hisia kali na uchungu mpaka wengine tukastaajabu kama kweli hawa ni wabunge wa ccm tunayoijua au la!, hapo mjadala mzima wa wabunge wa ccm leo bungeni utakuwa ni mchezo wa kuigiza ulioandaliwa na kupikwa kwa umahiri mkubwa tena kwa mbwembwe za uhakika na baada ya hapo itakuwa ni more hate and shame on ccm and the government!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom