Wabunge wa CCM wakutana saa saba, watambeba Ngeleja?

Wabunge wa CCM kama walishapitisha bajeti kuu kwa mbwembwe watakataaje hii ya Wizara moja wakati ni sehemu ya bajeti kuu? Walishapotea njia kwa kupitisha bajeti ya Mkullo hivyo hawana cha kufanya wala hawawezi kurekebisha kitu chochote kwenye mafungu yaliyopangwa kwa kila wizara.
Hivi........... Ni kwa nini huwa inaanza bajeti kuu halafu hivi vibajeti mtoto vinafuata..??? Kwa upande wangu vingeanza hivi vibajeti vitoto halafuu iwe ya mwisho........ Mi ni Contradiction tu kukaa bajeti ndogo wakati ulishaikubali kuu
 
Iaelekea hujui maana ya "my take".Nenda ngumbaru.
Tangazo la speaker wa Bunge limetia fola baada ya bunge kulindima kwa vicheko juu ya wabunge wote kuonana hali kukiwa na kila dalili kuwa budget ya Wizara ya Nishati na Madini haitapita. Hali hiyo inaashiria kuwa wabunge wanataka kuwekwa sawa (Kusetiwa) ili wakati wa kupitisha budget wawe ''RUBBER STAMP'' ya ''SIRIKALI''.

My intake; Wabunge wa CCM msikubali kubeba haibu hii!!
 
Mi nasubiri maandamano tarehe 24 July, 2011. Nimechoka, nimeteseka sana, nimenyanyasika sana na sirudi nyuma hawa magamba wanavijereta makwao ndo maana hawaoni umuhimu wa nishati ya uhakika.
 
Yaaani Nimekasirika sana nilivyosikia hilo Tangazo la Spika!!!
Hivi hii Nchi nani Katuroga??, Argggghhhhhhhhhh
ina maana hujia aliyeturoga kweli??????!!!!!! ka hujui aliyeanza kutiroga ni yule mzee wa Butiama na kafimbo chake fu wakafata wachawi wengine watatu
 
Kwa mtazamo wangu kikao cha wabunge wa ccm mchana huu wanajipanga kupitisha bajeti na Ngeleja atapona kama kawaida yao ngoja tusubiri jion tuone itakuwaje, na sisi wananchi tusikubali mi nawaunga chadema mkono nipo tayari kuandamana usk na mchana ili tuondokane na tatizo la giza
 
Mi nasubiri maandamano tarehe 24 July, 2011. Nimechoka, nimeteseka sana, nimenyanyasika sana na sirudi nyuma hawa magamba wanavijereta makwao ndo maana hawaoni umuhimu wa nishati ya uhakika.

OLE WAO WAIPITISHE WATAJIPALIA MAKAA YA MAWE NA MOTO WAKE SI MDOGO KUUZIMA.WALIANZA VIZURI KAMA WAMEENDA KUPOZANA ILI WAIPITISHE WATAONA MOTO.


Ni vyema wakatoa mifano kwa Mawaziri wengine kuwa inakupasa kujituma kwa bidii kutatua matatizo ya wizara yako kama Mh Magufuri.
 
mimi ni kila imani kuwa hawa CCM wataipitisha tu hii budget ya Gelesha. kitu ninachoomba kwa wana Tz wenzangu sasa tumechoshwa na siasa za majukwaani tu bila vitendo. hao wa CCM wamefika mwisho na sasa tuelekee upande mwingine wa upinzani kunawe
 
Hapana....naamini MUNGU atakuwa upande wetu leo.............................na Goliath ataaanguka tu
 
Tuone kama kweli CCM wana ujasiri kiasi gani jioni hii. Watayasimamia waliyosema au watakula matapishi?

Kwa wabunge wa magamba usitarajie kwamba hiyo bajeti itakwama. Utashangaa na roho yako jioni watakuwa wamebadilika na shupaza sura zao. After all watakuwa wameshapata mgao wao.
 
Wabunge wa CCM wanajipanga kama kamati kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati.

Umeme ni swala la kitaifa.Sio la CHADEMa wala CCM. Chonde wana CCM,ndayi ni watanzania.Kwanini mkubali ndugu zenu baba zenu,mama zenu,ndugu zenu na majrani zenu wakae gizani kwa nyinyi kupata umaarufu kwa Chama?? Cheo ni dhamana! Unaposimamia jambo la kitaifa kwa moyo Watanzania watakupatia 'CREDIT'


Please,Tuwe waungwana kwa swala la umeme!
Sioni tatizo kubwa kukaa gizani tatizo linalonitisha ni watu kupunguzwa kazi kwasababu hakuna umeme kuna gazeti nilisoma wiki iliyo pita kuwa kuna wafanyakazi zadi ya 7000 wamesimamishwa hawa ni wale walio ajiriwa lakini kuna watanzania wengi sana walio jiajiri ambao kwasasa hawana uhakika na kazi zao kwasababu ya umeme sasa kama CCM inaona hili sawa...basi vyama vya upinzani viungane kwa hili kuishinikiza serikali
 
Kama bajeti haitapita nitambea bila nguo mtaani. sifuti kauli

Afadhali uanze kutembea tu kwa sababu kwa wabunge wa magamba usitegemee kitu. Tena kama uko dodoma nenda jioni hii ingia humo mjengoni bila nguo uwaachie na radhi.
 
Unapokuwa na akili kama za wabunge wa ccm kwa ujumla wao, ni ngumu kuikataa hii bajeti
 
Ndugu zangu nimefuatilia mjadala wa bajeti ya wizara na madini leo hii asubuhi wa nishati na madini, Japokuwa wachangiaji wengi walikuwa wa Chama tawala cha CCM wengi wamekataa katu kwamba hawaungi mkono bajeti hiyo kwa hiyo isipitishwe. Kinachonifurahisha hapa ni naman ambavyo wabunge wa CCM wameachikia mbali itikadi zao za chama chao na kuamua kulivalia njuga jambo hilo. Baada ya bunge kumalizika spika Anne Makinda ametangaza wabunge wote wa CCM wakutane ukumbi wa Msekwa kikao ambacho mpaka sasa kinaendelea, ninachowashauri wabunge wa CCM ni kwamba wasifanye uamuzi wowote wa kutaka kuipitisha bajeti hii kinyemela wajue watakuwa wamevunja imani yao kwa wananchi na kamwe hatutawaunga mkono kwa hili, tuko tayari kuingia mitaani. Itakuwa ni aibu kubwa sana kwa Wabunge wa CCM kuonesha ujasiri mkubwa wa kutetea masilahi ya taifa kikao cha asubuhi hlf jioni waje watugeuke. Hoja hii sio ya kisiasa wekeni masilahi ya Taifa mbele na hima mhimizeni waziri Ngereja ajiuzuru na apumzike kwa amani. ASANTENI SANA, MWACHENI NGEREJA APUMZIKE KWA AMANI

Wana JF mnalionaje hili?

Mara kwa mara wanaanza kwa makeke namna hii. Ngoja uone watakavyobadilika na kushupaza sura zao watakaporudi mjengoni jioni hii. Kama ulikuwa huwajui vizuri wabunge wa magamba leo ndiyo utawafahamu vizuri. Pumba pumba kabisa
 
Jna sikuwa na umeme nyumbani nikawa nawaza kama uchawi ungekuwa unafany akazi ningeloga umeme ukatike kwenye nyumbazao zote na hata wakitumia generators ugome. Wadau sijui hii inawezekana. maana nadhani wengi wa viongozi wetu hawajawahi kuona mgawo.
 
jamani what i dont understand ni hivi kweli ccm wote ni corrupt kiasi hicho yani inawezekana vipi the whole gvt hamna hata mmoja anaye feel sorry kuanzia vijana mpaka wazee..from what i know mtu ukishazeeka hata ambition zinapungua sasa ka ushachuma sana why dont u slow it down kidogo ukawatumikia wananchi kidogo...inauma sana kuona wakina sita,makinda na other ccm wakimsaidia ngeleja wao...bajeti itapita leo ila ntalia sana....
 
Back
Top Bottom