Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,084
Habari wanajf.
kwanini nina sema wabunge wa ccm wamedhihirisha ubovu wao.
Tumekuwa tunaona mijadala mbalimbali inayoendelea kwasasa ile ya kusema mawaziri mizigo, kwasasa tumeona magazeti mbalimbali yakisema wabunge wa ccm wameandikisha majina ya kukutana na uongozi wao kuwajadili mawaziri wao.
Kimsingi ni ukilaza wa hali ya juu sana kuona wabunge ambao muda mwingi wamekuwa wakitumia uwingi wao kukandamiza hoja za upinzani na kushindwa sasa kutumia uwingi wao kuwatoa mawaziri mizingo, hii inazihirisha ni jinsi gani wabunge hawa wasivyokuwa huru ama upeo wa kulitumia bunge vizuri na kuendelea kujidhalilisha.
Mawaziri wanao wapigia kelele kila siku wamekuwa wakisimama na kusema serikali sikivu pale wanapokuwa kwenye uchangiaji kwenye wizara husika na wamekuwa wakiwasifia mawaziri wao kama malaika vile, leo wanakuja eti wanasema mawziri wao ni mizigo ile hali walikuwa wakiwatusi wapinzani walivyokuwa wanasema mawaziri wa ccm ni janga la kitaifa. Kweli sikio la kufa halisikii dawa nenda kampumzike ccm maana umma umekuchoka na wabunge wako wanakudhalilisha sana.
M4C DAIMA....