Wabunge wa CCM wadhihirisha ubovu wao

Wabunge wengi wa ccm wameingia bungeni kwa kuhonga wananchi wa majimbo yao, wengi hawajui kwa nini wako bungeni, wengi wanachokijua ni matumbo yao na unafiki wa kuisifia serikali!
 
Habari wanajf.

kwanini nina sema wabunge wa ccm wamedhihirisha ubovu wao.
Tumekuwa tunaona mijadala mbalimbali inayoendelea kwasasa ile ya kusema mawaziri mizigo, kwasasa tumeona magazeti mbalimbali yakisema wabunge wa ccm wameandikisha majina ya kukutana na uongozi wao kuwajadili mawaziri wao.

Kimsingi ni ukilaza wa hali ya juu sana kuona wabunge ambao muda mwingi wamekuwa wakitumia uwingi wao kukandamiza hoja za upinzani na kushindwa sasa kutumia uwingi wao kuwatoa mawaziri mizingo, hii inazihirisha ni jinsi gani wabunge hawa wasivyokuwa huru ama upeo wa kulitumia bunge vizuri na kuendelea kujidhalilisha.

Mawaziri wanao wapigia kelele kila siku wamekuwa wakisimama na kusema serikali sikivu pale wanapokuwa kwenye uchangiaji kwenye wizara husika na wamekuwa wakiwasifia mawaziri wao kama malaika vile, leo wanakuja eti wanasema mawziri wao ni mizigo ile hali walikuwa wakiwatusi wapinzani walivyokuwa wanasema mawaziri wa ccm ni janga la kitaifa. Kweli sikio la kufa halisikii dawa nenda kampumzike ccm maana umma umekuchoka na wabunge wako wanakudhalilisha sana.

M4C DAIMA....

wanawasikiliza maboss wao kwanza, watu makini hujadili mambo yao ndani...
 
Hiyo mbona ndo walivyo kwani hukuwaona jinsi walivyokuwa eti wanalalamika kwa Kinana hela zimetengwa kwenye bajeti lkn hazifiki kwa wakati na ni watu hao hao wakiwa bungeni kila kitu naunga mkono hoja utafikiri malalamiko yanaenda kwa mtu mwenye mamlaka kuliko bunge. Shame on them

Kama hiyo ilikuwa kweli ndio kusadikika ya Shabani Robert. Kwa suala la pesa na bajeti, wabunge wanatakiwa wahoji na kuwajibisha serikali. Sasa kama watahoji chama (Kinana) sijui wanataka wamwajibishe Kinana/chama, au wanataka kumwambia Kinana awajibishe serikali? Kinana huyu huyu! Urai wake wa kuombe (Second class citizen) anatumwa na wabunge (1st class citizen) kuwajibisha serikali yetu. Pia uadilifu wa huyu TX wetu ni wamashaka. Hili la kuogopwa hata na tembo limekaa vipi? Kwani la CCM la kiongozi kutokuwa na hisa ktk kampuni Kinana halimhusu au lilishafutwa. Kama limefutwa ni kwa nini?
 
...

NIRAHA SANA KUMSIKILIZA MBUNGE WA CCM:


"Mheshimiwa Spika, naona upinzani wamefikia pabaya, wanaikashifu serikali sikivu ya CCM. Chama kimefanya mengi sana, maendeleo makubwa tumepata, shule za msingi, sekondari na vyuo viko vingi leo, barabara za lami, umeme nchi nzima mpaka vijijini, lakini CHADEMA wanakebehi. Naipongeza sana serikali ya chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, nikiendelea mbele naomba nielezee kwa kifupi matatizo ya jimbo langu. Kule hatuna shule ya sekondari katika kata sita, maji ni ndoto, tunategemea mvua. Shule zilizopo hazina ubora wala walimu wa kutosha. Rais alikuja sasa ni miaka sita akatuahidi umeme lakini mpaka leo hakuna lolote. Barabara ni mbovu hazipitiki. Nauliza ni lini serikali híi (ya CCM) ITATUSIKIA NA KUTULETEA MAENDELEO?"
(Makofi) kwa! Kwa! Kwa!

By yegella
Earthmover huyu aliunga mkono hoja au aliishia kuuliza maedeleo yatamfikia lini! Naomba unijuze ili nione kama alibadilika jumla au gamba lilimrudia mwishoni mwa mchango wake.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom