Wabunge na wataka Ubunge wakizuiwa kutoa misaada majimboni kwao... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na wataka Ubunge wakizuiwa kutoa misaada majimboni kwao...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 19, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Nimefikiria kuwa kama kuna jambo linaweza kulazimisha mabafiliko na uwajibikaji bungeni ni kuwazuia wabunge kutoa misaada ya aina yoyote majimboni kwao. Yaani wasitoe misaada ya ujenzi wa visima, madarasa, mabati, nk. Waliopita majimboni ndani ya mwaka miaka miwili wakitoa misaada nao wazuiwe. Nini kitatokea ama kwa wabunge au majimbo yao?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  misaada ni ipi?
  posho si kodi zetu???
  si wana mifuko ya majimbo?
  msaada hakuna hapa....warudishe kidogo wanachojitoea.....
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sijui kama nimeifahamu vizuri hoja yako, lakini kwa kutilia maanani kuwa lengo la kuwa na wabunge majimboni ni kupeleka na kutetea maendeleo ya majimbo yao, kuwazuwia wasifanye hivyo, kutakuwa na haja gani ya kuwa na wabunge? Kuwazuwia wabunge wasitoe misaada kunaweza kulazimisha mabadiliko kwa njia gani?

  Ni kweli kuwa wengine, na ni wengi, hufanya hivi zaidi kwa maslahi ya kisiasa kuliko nia ya kuleta maendeleo, lakini kwa wananchi ambao wana shida, misaada hii huwasaidia sana, hasa pale ambapo serikali kuu imeshindwa kufanya hivyo.

  Bahati nzuri kwa sasa wananchi wameamka kidogo, kwa hivyo ikiwa mbunge au mgombea ubunge anafanya hayo kama rushwa, ninawashauri wananchi wapokee "mlo" huo halafu siku ya uchaguzi ikifika wachague wale ambao wanahisi wana maslahi kwao na kuwatelekeza watoa rushwa.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Fikiria kidogo mtu kama Rostam Aziz aliingia Bungeni kufanya nini kama vitu vyote alivyotaka kufanya jimboni mwake aliweza kuvifanya kwa fedha yake?
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hiki ndicho kilio changu. Itungwe sheria inayokataza mbunge kutoa misaada jimboni kwake. Kinachoendelea sasa hivi is nothing more than 'institutional corruption'. Mbunge kazi yake ibakie kutunga sheria, kusikiliza kero/kuwakilisha kero za wananchi na kuisamamia serikali ili kuhahakisha kero hizo zinapatiwa ufumbuzi.

  Mbunge asiwe afisa miradi, mbunge asiwe mfadhili, na kubwa zaidi wabunge wasiwe ndio serikali. Hili limeachwa na sasa wananchi wanataka wabunge wajenge visima! Hela za kwenye majimbo zipo- tena nyingi sana kupitia halmashauri. Mbunge ahakikishe hela hizo zinatumika ipasavyo. Halmashauri ya Kishapu kwa mfano wamefuja zaidi ya Tshs 6 billion! Hizi ni hela nyingi sana kama uta-convert kwenye madarasa, madawati, dawa kwenye vituo vya afya, visima vya maji. Na Halmashauri zinafuja hela kwa sababu mwakilishi wa wananchi yuko busy anasaka pesa sijui wapi?

  Ukweli kama wabunge watakatazwa kutoa misaada tutaona cheche bungeni maana watakula sahani moja na serikali. Hela zipo, kinachokosekana na usimamizi. Na bunge ndio kazi yake.
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana kaka mm,mimi siku zote nakataa mbunge kutoa msaada jimboni,nilikuwa na rafiki yangu pale bungeni marehemu mbunge phares kabuye alikuwa anagombana sana na wabunge kutoka zanzibar yeye alikuwa anawaambia kule kwao kagera hadaiwi hela ila anadaiwa uwakilishi bungeni,
  na hapo ndipo tunapotakiwa kusimamia.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi wabunge wanaopenda kutoa misaada majimboni mwao wana sababu zao fulani fulani hivi... fikiria
   
 8. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mm hapa naona kama kuna watu unawasema sasa.
   
 9. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Maendeleo kwenye majimbo yanapaswa yaletwe na serikali na sio wabunge. Kazi ya wabunge ni kuhimiza serikali kuleta maendeleo. Kama wabunge wana pesa kiasi cha kuweza kuchangia miradi ya maendeleo, basi mishahara hiyo ipunguzwe ilingane sawa na ya watumishi wengine. Kuchangia katika miradi ni sawa na kutoa rushwa ili waweze kuchguliwa tena. Kwa namna hii inakuwa shida sana kwa mgombea ambaye mbunge kushinda. Ndio maana tunaona wabunge ambao wamekaa miaka mingi kwenye ubunge.

  Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
   
Loading...