Wabunge muondoeni spika

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,439
2,000
Huyu spika hafai na analiburuza bunge ili kuibeba serikali.

Ni kwanini ameahirisha bunge wakati muda bado upo mara baada ya Muhongo kuongea?

Huyu mama ana agenda ya siri.
 
luirhu

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
718
500
Kwani tatizo nini? Jioni si bunge litarejea?! Tuwe wavumilivu hatumwi mtoto Dukani hapa!
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,439
2,000
Kwani tatizo nini? Jioni si bunge litarejea?! Tuwe wavumilivu hatumwi mtoto Dukani hapa!
Anahujumu muda wa mjadala bila sababu za msingi.Kwanini ameahirisha bunge wakati kukikuwa na nusu saa nzima ya wabunge kujadili.
 
May 3, 2012
73
95
Kesho ndo siku ya mwisho ya kujadili hii inshu watu mnapigwa changa la macho kesho bunge linaisha hakuna kilichofanyika.Makinda amekua mbabe sana anaburuza wabunge anavotaka yeye
 
JohnShaaban

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
464
195
Wasipoteze muda, waanze mchakato wa kumtoa Makinda. Jioni akikaa kwenye kiti anampa nafasi Masele ambaye naye atamaliza muda, kisha anafunga mjadala.

Kamati ya PAC ikutane na kuandaa walau msemaji mmoja wa kujibu uongo wa Muhongo! Mfano, amesema uthibitisho wa Brela kuhusu PAP kumiliki hisa 7 za IPTL ulitolewa Dec. 2013, kipindi ambacho deal ilikuwa imeishafanywa!

Hawa jamaa wanachezea akili za Watanzania
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,135
2,000
Huyu spika hafai na analiburuza bunge ili kuibeba serikali.

Ni kwanini ameahirisha bunge wakati muda bado upo mara baada ya Muhongo kuongea?

Huyu mama ana agenda ya siri.
kitaeleweka tu, ngoja wakaangane wenyewe kwa wenyewe mpaka kieleweke.
 
KMANGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2014
673
500
Makinda ni pandikizi la MAFISADI hivyo kila afanyalo ndani ya bunge ni lazima apate ushauri na maelekezo kutoka kwa waliomuweka kwenye nafasi hiyo yaani MAFISADI wenyewe. Haitii shaka hata kidogo kuwa huyo Mama hana uwezo kabisa wa kuliongoza bunge zaidi ya kutumia ubabe na vitisho kwa wabunge wanaoonekana kukinzana na msimamo wake wa kidhalimu.
 
Opera Min

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
903
500
Huyu spika hafai na analiburuza bunge ili kuibeba serikali.

Ni kwanini ameahirisha bunge wakati muda bado upo mara baada ya Muhongo kuongea?

Huyu mama ana agenda ya siri.
wabunge wanapewa muda waka jiandae ukizingatia ripoti ya muhongo hawaja pewa sasa mtu aanze kuchangia tu bila kupitia hoja zote mbili?
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,647
2,000
Huyu spika hafai na analiburuza bunge ili kuibeba serikali.

Ni kwanini ameahirisha bunge wakati muda bado upo mara baada ya Muhongo kuongea?

Huyu mama ana agenda ya siri.

Mkuu, hilo sio jambo baya. Kwanza ilikuwa inakaribia saa saba mchana na ni kawaida muda huo Bunge huarishwa hadi mchana. Pili, inawapa nafasi wachangiaji kuanisha hoja za kamati ya Zitto/Filikunjombe na zile za "Profesa" ili wakati wa mjadala waangalie pande zote mbili kwa umakini.

Jambo la kushangaza ni kwa nini PM hakuzungumza kwa niaba ya serikali bali akamwachia Muhongo minus "h"
 
  • Thanks
Reactions: R.B

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Makinda ameshauriana na upande wa serikali kuwa waminye muda wa wabunge kuchangia, na mawaziri wapewe muda wa kutosha ili ikifika kesho bunge lìhairishwe mara moja, na mambo yaishie. Bunge hili halijitambui kamwe! Ndo maana walimpa likizo ndugai akale bata ufaransa!
 
traco

Member
Jan 14, 2014
41
0
Wakuu vumilieni nadhan amefanya hivyo kusudi ili wapitie rapurapu za muhongo ili walinganishe na ya PAC, hana pa kutokea amewasilisha majibu zaifu na mepesi dhidi ya hoja nzito za PAC. Walikosa mtu mahili na makini. Kama kawaida yake kazijibu kwa dharau, eti TRA wakadai PAP au IPTL hajui hata utaratibu wa kukokotoa kodi malipi yafanywapo.kweli ni mtu wa miamba na akaipasue vizur
 
wanatamani

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
416
250
Pesa za kijiko jamani sio za umaaa msimtie mawazo mzee wa tezi .kashajichokea sio kazi ndogo kupanga upya baraza la mawaziri. Kwa majibu ya uwongo hiyo imetoka pesa za kampeni jamani tisheti na mabango wataprintia majani jamani hizo zao vitendo kwenye sanduku la kura
 
nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Mkuu, hilo sio jambo baya. Kwanza ilikuwa inakaribia saa saba mchana na ni kawaida muda huo Bunge huarishwa hadi mchana. Pili, inawapa nafasi wachangiaji kuanisha hoja za kamati ya Zitto/Filikunjombe na zile za "Profesa" ili wakati wa mjadala waangalie pande zote mbili kwa umakini.

Jambo la kushangaza ni kwa nini PM hakuzungumza kwa niaba ya serikali bali akamwachia Muhongo minus "h"
jioni atapewa nafasi naibu waziri wa nishati wa madini kwa muda wa saa 1 na nusu, baada ya hapo bunge litaahirishwa mpaka kesho, na kesho mkutano wa bunge utahairishwa, makinda amedhamiria kuilinda serikali hii ya mafisadi!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom