Wabunge kama hawasikii kilio juu ya HESLB

Umesahau kuwa jiwe aliwapa mlungula wabunge wote wa lumumba wakati wa kupitisha hyo sheria?????Tatizo watanzania ni wepesi kusahau,mbowe alijitokeza kupinga hyo sheria akamtuhumu jiwe kuwahonga yy alijibu kirahisi eti ilikua ruzuku ya ccm
 
Unazungumzia wabunge gani labda??? Hawa wabunge la kijani sio?
 
Malengo ni kuanzisha vyanzo vipya vya mapato,wasikilize vilio vyakupunguza vyanzo vya mapato nani kasema.
 
TAKE NOTE: TANZANIA HATUNA WABUNGE... HAKUNA MBUNGE ALIYECHAGULIWA NA WANANCHI
 
Umesahau kuwa jiwe aliwapa mlungula wabunge wote wa lumumba wakati wa kupitisha hyo sheria?????Tatizo watanzania ni wepesi kusahau,mbowe alijitokeza kupinga hyo sheria akamtuhumu jiwe kuwahonga yy alijibu kirahisi eti ilikua ruzuku ya ccm
Wote waliopitisha nyingi ya sheria mbovu,wengi leo hii hawana nafasi hiyo tena na sheria hizo zina minya na wenyewe,ndio ile kusema malipo hapa hapa,maishani.
 
Hawa wabunge waliotokana na uchafuzi mkuu wa mwaka 2020, kwa sasa watakuwa wanajipanga kulilia pesa yao ya mkopo wa gari iliyopigwa panga, it is so unfortunate safari hii hatuna bunge bali lundo la waimbaji wa mapambio wa kupitisha hoja za malaika mkuu.
 
Hakina wabunge tena,
Waliyopo ni wajumbe wa kamati kuu ya CCM,
Hata wale Covid 19 Kama watakuwepo ,msitegemee watapaza sauti,ndiyo mashariti ya aliyewateua,


Muhimu ni kwamba kila timu ishinde mechi zake za nyumbani.
Kwahiyo mmeshindwa kuwafuta uwanachama hao covid 19?
 
Hawa wabunge wangu wa Tanzania nilikuwa nawasubiri kwa hamu kila kikao cha bunge angalau mmoja atapaza sauti juu ya hiki kilio cha watanzania juu ya asilimia 6 inayojulikana kama retention fee.

Ukweli ni kwamba hakuna wakuhoji Ile Sheria. Sheria Ile kama ingetokea kwamba ipigiwe Kura, nahisi ingekataliwa kwa asilimia miamoja.

Hata sijajua mantiki ya Ile Sheria. Sheria inamfanya mdaiwa wa deni kuwa na deni endelevu. Sheria Ile ni kandamizi kwa wanyonge.

Endapo ningepewa nafasi nitoe Maoni yangu juu ya Sheria Ile ningependekezwa ifutwe. Kama lengo la Sheria Ile ni kuongeza mapato serikali toka kwa wanufaika ningekuja na mapendekezo haya:

1: Deni lile liongezewe flat rate kwa wadaiwa wote kiasi cha 500,000/- hivi halafu deni lake likiisha basi.

2. Deni lizingatie vipato halisi vya watanzania

Kuna mkanganyiko Mkubwa pale unapoambiwa deni liloko kwenye salary slip halina Uhusiano na deni halisi liloko Bodi ya mkopo. Nachanganyikiwa na hiki kitu kinachoitwa DENI HALISI
Deni halisi?

Kuna watu walikuwa na deni Lao walilopewa na Bodi wakati wanahitimu vyuo mfano. 10mil. Walipo anza kulipa waliambiwa wamechelewesha waliongezewa mil. 4 juu kuwa mil 14. Hivyo deni hili ndiyo liliingizwa kwenye mshahara na kukatwa kila mwezi.

Mtu huyu siku deni hili liliisha kulingana na salary slip yake.

Alipowasiliana na Bodi aliambiwa hilo siyo deni Halisi, Deni halisi liko Bodi.

Maswali:
1: Hili ongezeko la juu la mil4 lilifidia vitu gani?

2: Hilo deni halisi liloko Bodi linahusu nini na Kwanini halikujumuishwa kwenye deni liloko kwenye salary slip?

Huenda Labda ni uwezo wangu wa kuangalia mambo ni mdogo,lakini kuna mahali Sheria ya mwaka 2016 ina mapungufu.

Pengine hiki ninachokilalamika hapa ni mawazo yangu binafsi tu, lakini huku mtaani ukioongea juu ya LoarnBoard watu huishiwa nguvu. Siyo hawataki kulipa hapana, wote wanafurahi na pia wanahamasa kulipa deni la serikali, lakini wanaichukia Sheria ya 2016 inavyotekelezwa inawaweka wanufaika kuwa na madeni yasiyo lipika.

Kama serikali inataka kupata uhalisia wa hili basi ifanye haya:
1: Kila wilaya wafungue dirisha la maoni na malalamiko juu ya LoarnBoard

2:bLoarn board wafungue tovuti ya maoni ya wadau juu ya LoarnBoard watapata maoni mengi

3:Ofisi za bunge kila jimbo, iruhusu kupokea maoni ya LoarnBoard

Asanteni, wabunge tusaidie
Wabunge wenyewe wale wa kigezo cha kujua kusoma na kuandika waliojazana mle au kuna bunge jingine!?
 
Back
Top Bottom