Wabunge kama hawasikii kilio juu ya HESLB

FATHER OF HISTORY

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
720
500
Hawa wabunge wangu wa Tanzania nilikuwa nawasubiri kwa hamu kila kikao cha bunge angalau mmoja atapaza sauti juu ya hiki kilio cha watanzania juu ya asilimia 6 inayojulikana kama retention fee.

Ukweli ni kwamba hakuna wakuhoji Ile Sheria. Sheria Ile kama ingetokea kwamba ipigiwe Kura, nahisi ingekataliwa kwa asilimia miamoja.

Hata sijajua mantiki ya Ile Sheria. Sheria inamfanya mdaiwa wa deni kuwa na deni endelevu. Sheria Ile ni kandamizi kwa wanyonge.

Endapo ningepewa nafasi nitoe Maoni yangu juu ya Sheria Ile ningependekezwa ifutwe. Kama lengo la Sheria Ile ni kuongeza mapato serikali toka kwa wanufaika ningekuja na mapendekezo haya:

1: Deni lile liongezewe flat rate kwa wadaiwa wote kiasi cha 500,000/- hivi halafu deni lake likiisha basi.

2. Deni lizingatie vipato halisi vya watanzania

Kuna mkanganyiko Mkubwa pale unapoambiwa deni liloko kwenye salary slip halina Uhusiano na deni halisi liloko Bodi ya mkopo. Nachanganyikiwa na hiki kitu kinachoitwa DENI HALISI
Deni halisi?

Kuna watu walikuwa na deni Lao walilopewa na Bodi wakati wanahitimu vyuo mfano. 10mil. Walipo anza kulipa waliambiwa wamechelewesha waliongezewa mil. 4 juu kuwa mil 14. Hivyo deni hili ndiyo liliingizwa kwenye mshahara na kukatwa kila mwezi.

Mtu huyu siku deni hili liliisha kulingana na salary slip yake.

Alipowasiliana na Bodi aliambiwa hilo siyo deni Halisi, Deni halisi liko Bodi.

Maswali:
1: Hili ongezeko la juu la mil4 lilifidia vitu gani?

2: Hilo deni halisi liloko Bodi linahusu nini na Kwanini halikujumuishwa kwenye deni liloko kwenye salary slip?

Huenda Labda ni uwezo wangu wa kuangalia mambo ni mdogo,lakini kuna mahali Sheria ya mwaka 2016 ina mapungufu.

Pengine hiki ninachokilalamika hapa ni mawazo yangu binafsi tu, lakini huku mtaani ukioongea juu ya LoarnBoard watu huishiwa nguvu. Siyo hawataki kulipa hapana, wote wanafurahi na pia wanahamasa kulipa deni la serikali, lakini wanaichukia Sheria ya 2016 inavyotekelezwa inawaweka wanufaika kuwa na madeni yasiyo lipika.

Kama serikali inataka kupata uhalisia wa hili basi ifanye haya:
1: Kila wilaya wafungue dirisha la maoni na malalamiko juu ya LoarnBoard

2:bLoarn board wafungue tovuti ya maoni ya wadau juu ya LoarnBoard watapata maoni mengi

3:Ofisi za bunge kila jimbo, iruhusu kupokea maoni ya LoarnBoard

Asanteni, wabunge tusaidie
 

East Wind

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
2,839
2,000
Inaonekana ule msemo wa alieshiba hamkumbuki mwenye njaaa.. huenda ukawa na ukweli fulani
 

gachacha

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
1,733
2,000
Wapige kelele vip wakat wao ndo walitunga hiyo sheria na kusainiwa na raisi hakuna sheria inatokea BUZA na kusainiwa lazima itokee bungeni , mitano tena mingine mbele
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,190
2,000
Acheni ujanja ujanja lipeni pesa .hao wabunge nao wanakatwa kama kawaida
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,948
2,000
Wapige kelele ili iweje wakati waliokua wanatutetea wametupwa nje na sisi tumeridhia..!

Kila mmoja atacheza ngoma kwa wakati wake

Mitano tena
Hakina wabunge tena,
Waliyopo ni wajumbe wa kamati kuu ya CCM,
Hata wale Covid 19 Kama watakuwepo ,msitegemee watapaza sauti,ndiyo mashariti ya aliyewateua,


Muhimu ni kwamba kila timu ishinde mechi zake za nyumbani.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
29,034
2,000
Ukweli mchungu ni kwamba wabunge waliopo bungeni hawajachaguliwa na wananchi.Watamtumikia aliewapeleka huko bungeni.Jiandae kuisoma namba!
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,083
2,000
Sina imani na wabunge kama wataweza kulisemea,
Mkuu wa nchi kwakuwa anayasoma huku,angechukia hatua za haraka kuwanusuru wanyonge.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,366
2,000
Wapige kelele ili iweje wakati waliokua wanatutetea wametupwa nje na sisi tumeridhia..!

Kila mmoja atacheza ngoma kwa wakati wake

Mitano tena
Akina Halima Mdee mbona wako bungeni na walisoma mkopo ya bodi ya mikopo?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom