Wabunge CHADEMA Kutoka Nje Ya Bunge: Tafsiri Yangu


Wewe Pumbavu kaa pembeni na akili yako kama sisimizi. Hayo uliyoyasema ni akili yako wewe na hakuna hata mtu mmoja anayeitakia mema nchi hii ambaye anaona chadema imekosea.

Kwanza wewe umeibukia wapi? Si ulikuwa unatumika na ccm kwenye kampeni, naona bado unajipendekeza. Njaa hii itawaua wewe na mwenzio michuzi.
Ninyi ndio watu wamewachoka kutokana na upuuzi wenu na tamaa yenu ya kukubali kumtumikia kafiri eti kwa sababu ya hela ya mpito.

Mwangalie mwenzio michuzi, watu wamempotezea na hakuna mtu anayesoma wala kupeleka habari kwenye blog yake tena zaidi ya yeye mwenyewe kupiga picha za udaku na kuzibandika hapo kwenye blog yake.

Na wewe naona unataka kutoka kwa kutumia mgongo wa chadema.
Kweli chadema tishio, kila mtu anataka umaarufu kupitia chadema. HAKUNA ATAKAYEWASIKILIZA NINYI WANAFIKI.
 
Majid

Nilidhani wewe una upeo zaidi ya hapo! Hawa Chadema, ni muhimu kuonyesha wanasimama wapi, wanatetea nini, na kama wako pamoja. Kilichojihirisha hapa, wana umoja mkubwa baina yao. Wanaamini kitu na wanakitekeleza kwa pamoja, wana utii kwa kiongozi wao. Hizi ndizo tunu ambazo kila mmoja wa vyama hivi anapaswa kuwa navyo.

CHADEMA hawakubaliani na hoja iliyokuwa mbele yao. Lakini hata kama wangebaki ndani wakapiga kura, bado kura yao ni kiduchu mno, hii ni hali halisi ya siasa zetu kwa sasa hivi. Ili tuweze kuwajua kwamba hawakushiriki katika kupiga kura zile wamefanya uwazi na utandawazi kama alivyosema Mkapa, wametoka nje, kwa hivyo hata baadae CCM inapokuwa imebanwa labda 2015 au 2020 ikitaka kanuni hizo zibadilishwe, au basi tuseme tafsiri mpya itolewe, CHADEMA watakuwa SAFI, HATUKUSHIRIKI KATIKA YALE MADUDU, nadhani hili ni vizuri rekodi ikawekwa! Ungepaswa uwapongeze hawa, sio kwa kuwa ni wazuri au la, bali kwa kuleta tamadani za kutusaidia huko mbele, WEWEW VIPI? Bureeeee!
 


PUNGWANI.........................................!!!! P*%#$@*&%$U!!! Muombe mama yako uzaliwe tena labda kautaahira katapungua!!!!
 
CDM weka superglue masikioni ili mivumo michafu kutoka kwa wanafiki iwavumie wenyewe waaibike kiukweli kadamnasi hao ni 5th colome mswamind.
Kutoka kwenu bungeni ni sahihi na hamkuvunja kanuni yeyote
Ninashukuru hamkuwa sehemu ya uovu ulioidhinishwa kwa manufaa ya wachache

Endeleeni hivyo nina hakika you have a plan
advance to contact CDM!
 
Kwa upuuzi kama huu hata nikila BAN sijali provided nimetoa hasira zangu kwa mara ya kwanza!!
 
Mimi sielewi kabisa mantiki ya watu kukimbilia kusema Chadema wanajimaliza Kisiasa kwa kutoka nje ya bunge..... kwa nini watanzania tunapenda conclusion (mahitimisho) rahisi na yasiyo na ukweli? Kwani hao CDM walipata wapi nguvu na wataipoteza vipi? Mbona pressure yao ya Katiba imeanza kuleta matunda?

Je mtu kama hukubaliani na kitu, unalazimika vipi kukipokea? kama wao waliamua kutoka kwa sababu hawakubaliani na marekebisho wamefanya kosa gani? Wangebaki na kupitisha, baadae wakalalamika ungeona watu humu wanasema kuwa Chadema walipitisha sasa wanalalama nini.... hii ni tabia ya watanzania wengi kupenda kulaumu tu bila hata kufikiria!

Je unafikiri wale akina Cheyo au Kafulila ndio watakuja kuwa na nguvu kuliko Chadema? Kumbuka CCM watawatumia only this time, ikija kwenye uchaguzi hawatakuwa na rafiki...ni unafiki tu, wao vyama vidogo wangekuwa na busara kama wangetambua nguvu ya Chadema na kuunga mkono kwa manufaa yao...leo wanashangilia, next time itakuwa zamu yao kulazimishwa kufanya kitu wasichokitaka ndio watajua!! Hivyo Bwana Majid na wengine, tusipende kuhukumu, tuache watu na vyama vyao wafanye maamuzi yao, ukitaka kuwashauri au kuwasaidia jiunge na hivyo Chama. Nadhani kama taasisi Chadema hakiendeshwi na wana mazingaombwe, kuna wasomi na watu wenye staha zao, na ndio mana wakapata zaidi ya 20% ya Kura za uraisi...hivyo heshimu pia hao watanzania waliowachagua, usijifanye wewe unajua kuchambua mambo ya kisiasa wakati hujawahi kuwa mwanasiasa au kupitia utaalamu huo! Tuwashukuru Chadema mana wamesaidia mageuzi mengi hapa nchini, ndio mana hata Sabondo aliwapa michango na kuwatambua kuwa ni taasisi muhimu sana kwa ustawi wa jamii yetu...tuwape moyo badala ya kukimbilia kuwakosoa ....
 
kutoka nje ya bunge ni utaratibu halali wa kuonyesha kutokubaliana na hoja hata kama wengi wataipitisha, niliamnini utakua na historia ya mabunge ya nchi mbalimbali,fuatilia bunge la kipindi cha Hitler pale ujerumani, India nk. Think criticaly.
 

Ndipo ufahamu wako ulipoishia mkuu?please!!
 
Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Duh...watoto wa darasa la pili nao wapo humu??
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!




22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 

Duh...na wana mipasho nao ndani?
 

Mkuu,

Ijapokuwa Chadema wanawatuhumu CUF kuwa CCM B it remains to be just a mere accusations je ni sahihi kwa wao kuwatenga? Chadema kimekuwa chama kinachobeza ubabe zaidi kulikoni kujenga hoja zenye mantiki. Sasa unapojiona wewe uko sahihi ukakataa kujadiliana na upande wa pili huoni kama wanaendeleza ubabe wa CCM. Binafsi nakuunga mkono maggid kwamba this is the beginning of the end of chadema na wanajenga maadui zaidi ya allies katika uwanja wa kisiasa.
 
Maggid
Tuna tatizo kubwa sana ambalo naona waandishi wote hamtaki kulizungumzia, nalo ni CUF kuwa serikalini at the same time wapinzani.
Mimi nafikiri hoja waliyonayo cdm ni ya msingi sana tena ya Kikatiba. Inabidi cuf kwa namna yoyote washirikishwe uundewaji wa serikali ya JMT na sio Upinzani.
Hili likifanyika then tutawahoji cdm kwa nn hawataki wapinzani wenzao.
Tusaidie majibu MAggid kuliko kuwashambulia cdm bila sababu; Hivi cuf ni nani hasa katika taifa letu??? Au ndoo Muungano tumevunja??? Mimi nina tatizo na hili zaidi ya vijembe vya wanaccm utafikiri waimba taarabu vile
 
Maggid!

CDM Walikuwa wanatafuta media attention period! kama ambavyo na wewe wamekupata na magazeti hiyo wameandika habari yao..lol.

Kuna siku watavua nguo wote ili muradi wapate media attention...

Ngoja tusubiri wataleta ngojera ipi tena, uzuri ni 2015 tutakvyo wapiga chini walie zaid...
 
Majid,

Hoja ya kafulila haina hoja kwa sababu kama chama kikipata 60% kitakuwa na sababu gani ya kuungana na vingine? Sababu kubwa ya vyama kuungana ni unyonge wao na vinaungana ili kuongeza nguvu zaidi. Hakuna chama duniani kilichoungana na chama kingine i hali kina nguvu kikiwa peke yake. Sikurajia mtu kama wewe ushabikie hii hoja ya Kafulila ambayo najua hata yeye mwenyewe aliitoa kwa lengo la kuchekesha Bunge tu.
 
..hata mimi naunga mkono CUF kushirikishwa ktk serikali ya muungano.

..pia CUF na CCM waunde kambi yao, hata kama siyo rasmi kisheria, ndani ya Bunge la Jamhuri.
 

wewe nawe njaa tu zinakusumbua, utaweza wapi kuwakosoa watu wanaokulipa kwa kazi za kijinga kabisa eti vigezo vya kitaalam, siku yenu inakuja wote ninyi mnaotafuna pesa ya nchi mtakiona..piiipoz pawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…