Wabunge CHADEMA Kutoka Nje Ya Bunge: Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CHADEMA Kutoka Nje Ya Bunge: Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 9, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  SASA ni dhahiri shahiri kuwa CHADEMA inapoteza mwelekeo. Hili si jambo jema kwa demokrasia yetu changa tunayotaka kuijenga.


  Nimesoma kwa makini magazetini habari kuhusu sakata la wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wa Bunge jana jioni. Hakika sikuona mantiki wa walichokifanya mbali ya CHADEMA kuanza kutengeneza ombwe la upinzani wenye maana uliotarajiwa na Watanzania wengi.


  Miezi mitano imepita tangu tumalize uchaguzi, CHADEMA bado hawaonekani kufunga ukurasa wa siasa za wakati wa kampeni za uchaguzi. CHADEMA wana lazima ya kuingia kwenye maisha magumu na ya kawaida ya kisiasa.


  Maisha ya kisiasa yenye changamoto zake. Migogoro ya ndani ya Chama ikiwamo kutofautiana kimawazo. Uimarishaji wa chama mikoani na wilayani, kwa nchi nzima na mengine mengi. Ni ukweli CHADEMA bado haijaimarika katika ngazi za chini.

  Na changamoto za kisiasa hazikimbiwi, hukabiliwa kwenye majukwaa ya kisiasa. Wabunge wa CHADEMA hawakuwa na sababu za msingi za kutoka nje ya bunge. Badala yake, wangepambana kwa hoja ndani ya Bunge. CHADEMA si wanajua, kuwa hatma ya jambo lile lilikuwa ni kupigiwa kura. Kwamba wangeshindwa. Ni sehemu ya mapambano ya kisiasa.

  Watanzania tuna matatizo haya mawili; Mosi, tu mahodari sana wa kuukana ukweli. Pili, tu mahodari sana wa kuupotosha ukweli. Ukichanganya na kukimbilia kushabikia mambo na kutofikiri kwa kina, basi, tunashindwa kabisa kuambizana ukweli hata kama tunauona. Kwa kitendo cha jana, Wabunge wa CHADEMA hawakuwa sahihi. Kuwaambia vinginevyo si kuwasaidia.


  Wakati mwingine kukimbilia kutoka nje ya Bunge hakupelekei kupata huruma ya kisiasa bali hasira za kisiasa kutoka kwa wapiga kura. Ndio, kuna gharama zake. Mtatoka nje bungeni mara ngapi? Na CHADEMA kutoka nje bungeni kulikuwa na hasara zaidi kuliko faida. Huku mitaani, kuna watu wanaoanza kuiangalia CHADEMA kwa miwani mingine. Kwa staili hii, itafika mahali Wabunge hao wakaja kuzomewa Kibaigwa, Msamvu na kwengineko.

  Na David yule wa Kafulila kausema ukweli wake; kuwa. "Tunashinda kwa asilimia 20 tunakataa mseto, tukipata asilimia 60 hali itakuwaje, ukipata kidogo uoneshe una busara ya kufanya kazi pamoja, kwa hali hiyo ukipewa kikubwa huwezi kuaminika." Anasema David Kafulila wa NCCR Mageuzi.


  Sikilizeni, enyi ndugu zangu wa CHADEMA, yale tuliokuwa tukiwashutumu CCM, CHADEMA sasa mnayafanya mara mbili yake! Tumeilaumu, na bado tunailaumu sana CCM kuwa chama kisichokubali mabadiliko. Chama ambacho hakitaki kujenga misingi ya kugawana madaraka na wengine.  <font color="black">Leo CHADEMA hamjaingia madarakani mnaanza mapema kuwachagua wa kukaa meza moja na nyinyi. Mnavikebei vyama vingine ikiwamo CUF. Tuchukue mfano
   
 2. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

  Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

  Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mnamvamia mjinga mtaonekana nanyi wajinga pia huyo jamaa alishanunuliwa hamna kitu! Halafu huyu si anablog yake anatafuta nini huku??
   
 5. n

  ngoko JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwa nini usiulize waliokabidhiwa nchi wametekeleza ahadi ngapi zaidi ya kufanya vikao vya kuonyesha uungwana wa kulipa dowans ?.
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people. By JK Nyerere
   
 7. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii nchi itawaliwe kijeshi tu,tumechoka na siasa.Maggid kaa utulie,mziki wa mwaka huu si wa kitoto,yatakuja kufika ya akina Ben Ali.
   
 8. c

  chumakipate Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  pole sana watanzania hao waliokwambia CDM imepoteza mwelekeo wamekudanganya.CDM walitoka nje na leo
  mchakato wa katiba mpya JK ameukubali la sivyo ingekua taabu CDM moto chiiiiini.
   
 9. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Muungano wa vyama pinzani ni mzuri sana na pia unakua na tija kwa wapiga kura lakini nilazima uangalie ninani unaungana nae na pia woote mnavisheni moja au kuna unafiki? Cuf tayari walishaungana na CCm huko zenj hivyo basi Chadema wangekubali kuungan ana wabunge wa vyama vingine na sio wa Cuf ila kitendo cha kukataa kuungana na vyama vingine pinzani huo sio uungana na kuna ubinafsi ambao madhara yake ni makubwa zaidi ya faida.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Haina shida kinyonga wetu nilijua utakuja na rangi nyingine tu!
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu sijui argument yako umeibase kwenye nini....
  Kwamba Chadema ili waonekane wapinzani lazima waungane na CUF...?

  According to Chadema CUF ni CCM B na sio wakuwaamini, Je ni kosa kufikilia hivyo.., Chadema wanatakiwa wafanye kazi kulingana na watu wanaowaona watawasaidia..., sasa wewe huko nje mshabiki ndio wa kuwachagulia watu wa kufanya nao kazi?

  Kutoka nje ya Bunge ni symbolic ya kuonyesha kutoridhika na CCM, that is normal.. na kama unajua CCM wanamajority bungeni hakuna kitu kitakachopita kwa kujadiliana Diplomatically.., kwahiyo Chadema cha kufanya ni kuwawekea break CCM, na kuhakikisha wanafunua madudu yao..., kazi kamili ipo mtaani Mjengoni its just a formality
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  kwa huku ni kwako wewe au? wekeni wazi muone kama kuna mtu atawafuata huku kwenu.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Wameshakurudisha kwenye payroll yao? kawajibu hivi, huku JF sio sehemu ya kuja kuleta propaganda na siasa za majitaka, kama wao ni mahodari wa kufafanuwa vifungu waendelee na kufafanua zaidi kwamba hakuna kambi ya upinzani kwani kambi zipo kwenye majeshi, na kawaeleze hii kwetu sio story, kwetu story tunataka kujuwa hatima ya KAGODA, DOWANS, DEEP GREEN FINANCE, MEREMETA N.K. Hatudanganyiki ng,ooooooooooooooooooooooooooooooooo. peleka pumba zako kwenye magazeti ya Habari leo, Rai na Uhuru na Mzalendo.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu ni Maggid wa Mjengwa! Sikumbuki mara ya mwisho ni lini aliandika substance .......tafadhali niko open minded kukumbushwa.
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Maggid.

  Niliyasikiliza maneno mazito na busara kutoka kwa Mheshimiwa kafulila sijui kama watalifanyia kazi au ndiyo mwendo mdundo.
   
 16. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hii ni Tafsiri ya Mtaani isiyo na mantiki ndani yake ila inaonyesha jambo moja tu. "IMEWATOUCH PABAYA

  "
   
 17. A

  Awo JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Kwa hiyo Maggid ni nini mantiki ya kurekebisha sheria ili kulazimisha muungano wa wapinzani? Ni wapi huko ambako watu wenye mitazamo tofauti walilazimishwa kuungana kwa mujibu wa sheria halafu mafanikio yakapatikana? Si kweli kwamba wanaotaka kuungana wakakubaliana juu ya misingi ya kuungana huko badala ya kuwalazimisha kwa kutumia dictatorship of the majority?

  Pili ni busara kweli watu wazima, wanajiita viongozi, wanafikia mahali wanaamua kubadili kanuni ili ku-suit their own situation? Umefikiria kuwa lililotoke jana ni precedent kwamba wakubwa hawa wataendele kubadili kanuni na sheria (imeshatokea kwenye suala simple majority) kwa manufaa yao binafsi?
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Mjengwa,

  ..nadhani wewe pia unapotosha.

  ..CDM hawakukimbia hoja ile bungeni. walichangia hoja nzima na walitoka nje wakati wa kuhitimisha hoja.

  ..kuhusu Kafulila kauli yake haina msingi. kama suala ni kufanya kazi pamoja kwanini hawadai wajumuishwe ktk madaraka na CCM.

  ..CDM wamefika hapo walipo kwa ridhaa ya wananchi. NCCR,CUF,UDP, wanapaswa kuheshimu nafasi ya CDM ambayo wameipata kwa kura za wananchi.

  ..sasa hivi vyama vilivyozembea wakati wa uchaguzi mpaka vikapata mbunge mmoja au wawili, vinapodai viwe na haki sawa na chama chenye 20% huoni kwamba huko ni kuleta vurugu na uchu wa madaraka tu?

  ..kuna chama kama UDP kina mbunge mmoja ambaye ni mwenyekiti John Cheyo. miaka yote hiki chama kimekuwepo wilayani Bariadi bila kufanya juhudi zozote zile kuyafikia maeneo mengine ya Tanzania. sasa kuna uhalali na mantiki gani kwa John Cheyo kujaribu kukikwamisha chama ambacho kimejielekeza ktk kuwakilisha wa-Tanzania wote?

  ..suala lingine la kuangalia ni mwenendo mzima wa hivi vyama vinavyoipinga CDM. kitendo chao cha kutumia wabunge wa CCM kuikandamiza CDM unakichukuliaje? kauli na matamko ya kashfa yaliyotolewa na CUF dhidi ya CDM and in particular Dr.Slaa unafikiri inajenga mazingira ya kufanya kazi pamoja?

  NB:

  ..Muungano wetu una matatizo. tatizo mojawapo ni hilo la udogo[numbers dont lie] wa Zanzibar kiasi kwamba inakuwa taabu kutenda haki ndani ya nchi hii.

  ..
   
 19. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ni maneno yapi hayo..., hivi wananchi waliichagua Chadema ili waende wakashirikiane na Chama ambacho from Chadema's point of view ni CCM - B, yaani waliipiga CCM chini ili Chadema ishirikiane na CCM ?, Hapa argument is CUF wapinzani wa kweli ?, according to Chadema sio, so who are you to tell them otherwise..? na Chadema wanaona wakiungana na hawa watu kazi zao za upinzani hazitafanikiwa, na wana kila haki ya kuchagua wa kunya nae kazi.
   
 20. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,987
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Hizo busara ambazo baadhi yetu tunawashauri Chadema wazifuate ndizo zilizotufikisha wa-TZ hapa tulipo leo.

  Tuache mazoea ya ngonjera za miaka nenda rudi zilizotufanya hata akina Dowans watunyee vichwani mwetu mchana kweupeee.

  Tufike mahali tukubali hali halisi kuwa changes kwenye nchi hii zinahitaji "hard ball stuff"...si nale nale zilezile za miaka yote kuanzia 1961!
  For once, Chadema wanatuonyesha kuwa "enough is enough"...hard ball is the only way out. And it indeed is!

  Maggid my friend...it's time to stop pretending and instead start thinking outside that dark box!!
   
Loading...