Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa mwandishi wa habari aliyeko Dodoma, anasema wabunge wa CCM hasa wale wanaojulikana kama wapambanaji wa ufisadi na wengine,wamekuwa na vikao juzi, jana na leo asubuhi wamekubaliana kuwa ni lazima aondoke kwenye unaibu spika kwa vile amekuwa akitumia jazba badala ya kuzingatia kanuni kwa vile hakuna kanuni inayomruhusu spika kumfungia vikao 5 papo kwa papo.
Pia wanadai amewaharibia mkakati wao ambao walikwisha upanga wa kumfungia Lema kufuatia tuhuma za kumsema Rais kuwa ni mdini, wanadai akifungiwa tena ataonekana anaonewa na hivyo kumpandisha juu kisiasa, kilichowaudhi ni pale walipomwita na hakwenda kuwasikiliza zaidi ya kuwaambia kuwa yupo bize na hakuna kanuni iliyovunjwa, pia akasikika akisema kuwa hizo ni fitna za Sitta kukosa uspika.
Leo wamekubaliana kupeleka azimio lao kwa Pinda na Jenister Mhagama kwa hoja kuwa Ndugai kwa kutumia jazba bila kufuata kanuni anasabisha chama kionekane dhaifu kuwa kinaogopa wapinzani hivyo kukifanya kidharauliwe na kuchukiwa na jamii.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa maazimio yamewekwa kwa maandishi na wamechaguliwa watu wawili kuyapeleka mbele.
Mchakato unaendelea tusubiri tuone.
Cha kwanza sioni ukweli katika habari hii,ndugai amewekwa hapo na ccm ili kulinda maslahi yao na actually alichokifanya ni part ya kulinda maslahi yenyewe,sasa alichokosea hapo ni kitu gani?pili swala la Lema na udini mbona liko wazi?njoo ukasali msikiti wa pangani hapa Arusha hayo mbona ni mambo ya kawaida?pili kwani Radio imani inachikisema au kutangaza mara zote kabla ya the soo called adhabu ya kufungiwa haukijui wewe?na mwenye uwezo wa kukikemea kama sio RAIS ni nani?tatu kampeni zimekuwa zikifanyika sana misikitini hasa za CCM na huo ni ukweli usiopingika,juzi tu nikusaidie KINANA baada ya kuwekwa kuwa katibu mkuu wa CCM aliswali na sisi hapa ARUSHA,na alianza mambo ya siasa kwa kukifagilia chama,jamani misikitini pamekuwa mahali pa kufanyia kampeni,najua wenzangu hawatapenda kwanini nimesema haya lakini ni lazima tuweke wazi kwani kesho na kesho kutwa CCM ilimsimamisha mkristu and is most likely je itakuwaje?kampeni zitaendelea misikitini au itakuwaje?

I see, kwa hiyo kesi ya nyani akahukumu ngedere? Huyuhuyu Pinda ambaye amekuwa akitetea watendaji wabovu serikalini wasijiuzulu ndiye anayepelekewa habari ya Ndugai kung'olewa halafu tutarajie kwamba atafanya lolote? Labda wangeitoa kama hoja bungeni ili wabunge wapige kura, ingeweza kuleta maana zaidi. Lakini kuipeleka kwa Pinda ni kupoteza muda tu. Pinda na Ndugai hawana hata tofauti.