Spika Tulia na Bunge lake wanatosha kwa Spika kutoliongoza Bunge kutengua kanuni muda wa Bunge uongezwe, na wabunge kutoomba muongozo wa Spika?

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,450
152,385
Katika mkutano wa Mbunge Mpina na mawakili wake, moja ya jambo lilionishangaza zaidi ni madai kuwa Spika hakuliongoza Bunge litengeu kanuni ili wapitishe azimio la kuongeza muda wa kikao cha Bunge kilichopaswa kuisha saa 1:45 usku kama kanuni/taratibu za vikao vya Bunge zinavyotaka.

Yaani kwa kawaida(na ambavyo hata mimi nakumbuka enzi zile za JK nilipokuwa nafuatilia sana Bunge), kikao kinachoanza jioni(saa 11 jioni kama sikosei), hutakiwa kufikia tamati saa 1:45 usiku, na kama watahitaji muda zaidi, basi utaratatibu ni kutengua kanuni ambapo Bunge hupitisha azimio la kuongeza muda kwa siku hiyo na Spika ndio huongoza hio shughuli kwa kuwahoiji wabunge kama wanaridhia muda uongezwe.

Sasa kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa mawakili, kumbe ile siku wanamjadili na kumchukulia hatua Mpina kwa kumfungia kutohudhuria vikao 15, hilo halikufanyika licha ya kikao cha Bunge kuendelea mpaka mida ya saa 3 usiku.

Binfsi najiuliza, Spika hakujua kuwa anatakiwa kutengua kanuni na kupata azimio la Bunge muda uongezwe?

Kama Spika alipitiwa, wabunge wote wale hakuna hata mmoja alieona hii kasoro na kuomba muongozo wa spika?

Kama kuna mbunge aliomba muongozo, mwenye kumbukumbu atutajie jina la huyo mbunge.

Mpaka hapa, je, Spika na Bunge lake wanatosha?

Wapinzani wangekuwepo Bungeni, haya yangetokea?
 
Ila huyu Mpina huyu... Ana back up moja la kjasusi.
Si kawaida. Hakuna mtu alithubutu hizi kelele wakati wa JIWE...
 
Back
Top Bottom