Wabunge CCM Wataka Ndugai ang'oke

Wabunge CCM Wataka Ndugai ang'oke

Mbona walikuwa wanashangilia wakati Ndugai anasema watolewe nje??? Unafki tu huo
 
Mhhh! Kazi kweli kweli maana taarifa kila kukicha
Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa mwandishi wa habari aliyeko Dodoma, anasema wabunge wa CCM hasa wale wanaojulikana kama wapambanaji wa ufisadi na wengine,wamekuwa na vikao juzi, jana na leo asubuhi wamekubaliana kuwa ni lazima aondoke kwenye unaibu spika kwa vile amekuwa akitumia jazba badala ya kuzingatia kanuni kwa vile hakuna kanuni inayomruhusu spika kumfungia vikao 5 papo kwa papo.

Pia wanadai amewaharibia mkakati wao ambao walikwisha upanga wa kumfungia Lema kufuatia tuhuma za kumsema Rais kuwa ni mdini, wanadai akifungiwa tena ataonekana anaonewa na hivyo kumpandisha juu kisiasa, kilichowaudhi ni pale walipomwita na hakwenda kuwasikiliza zaidi ya kuwaambia kuwa yupo bize na hakuna kanuni iliyovunjwa, pia akasikika akisema kuwa hizo ni fitna za Sitta kukosa uspika.

Leo wamekubaliana kupeleka azimio lao kwa Pinda na Jenister Mhagama kwa hoja kuwa Ndugai kwa kutumia jazba bila kufuata kanuni anasabisha chama kionekane dhaifu kuwa kinaogopa wapinzani hivyo kukifanya kidharauliwe na kuchukiwa na jamii.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa maazimio yamewekwa kwa maandishi na wamechaguliwa watu wawili kuyapeleka mbele.

Mchakato unaendelea tusubiri tuone.
 
nashauri hao jamaa wamuongeze na Makinda nae apigwe chiniiiiiiii

Mwenzenu nikilala naamshwa na zile kelele za """Polisi mtoeni nje Tindu Lissu!!!"""
Kwa wale waliorekodi ile clip ukienda sehemu halafu ukacheza ile clip na kuwauliza wanadhani ni wapi hizo kelele zilitokea watakwambia mengi sana.

Mfano:
Mwandishi: Ndugu wananchi hapa kuna sauti imerekodiwa nitaicheza halafu nikizima nitawaomba mnieleze ni wapi mnadhani kelele hizo zilikotokea. Kisha mwandishi anawasha ile clip
Clip Inasikika: Askari toa Tindu Lissu nje!!!! Toa nje, Tindu Lissu toka nje!!!
Mwandishi: Ndugu wananchi hapo mnadhani tukio hili liltokea katika mazingira yapi???

Wananchi:

Wa Kwanza- Ilitokea Bar walikuwa wamelewa Lissu akakataa kumnunulia Ndugai Bia. Ndipo Ndugai akaomba askari wa Bar wamtoe Tindu Lissu nje ya Bar!!!

Wa Pili- Hawa wawili inaelekea wanaugomvi wa siku nyingi ambao chanzo chake ni nje ya Bunge, sasa kwa visa tu Kiti kikakumbuka machungu kikachukulia hasira, maana kuomba miongozo si kuvunja kanuni za Bunge.
Wa Tatu- Job Ndugai na Makinda wanaegemea CCM kwani siku ambayo Makinda alitoa angalizo kwa wabunge kuwa atawatoa nje wakitoa matusi, siku ya pili Mh. Seukamba akatoa """Come on f.....k you""". Kama kuna usawa pale ilikuwa atolewe nje kwa tusi lile la nguoni. Mh. Mwigulu naye akatoa tusi la "Kishoga shoga" alipomwambia Mh. Mnyika "Wakubwa wanapoongea MTOTO WA KIUME" anatakiwa kukaa kimya.Kwa kweli tunakemea sana kauli hizi kutolewa na ORGAN YA SERIKALI tena Organ muhimu kiasi hiki.

Labda Waheshimiwa Wabunge tuwakumbushe kuwa mnakotoka huko majimboni mmeacha familia zenu yaani Mke/Mume na Watoto wenu. Unapomtukana Mbunge mwenzako kumwita ni "Mtoto wa Kiume" Unakuwa UMEMDHALILISHA SANA. Hamjawahi kuwa na kanuni za kukemea mambo haya kwasababu Maspika waliopita walikuwa MAKINI na hawakuruhusu MICHEZO HIYO. Mbunge kumbuka unapata mshahara ambao ni kodi yetu wananchi, kibaya zaidi mimi ninayekulipa nakatwa kodi wewe unayepokea hukatwi kodi. Ikiwa mngekuwa na uchungu huo wa kukatwa kodi hakika wala hamngekuwa na mambo hayo ya "Kishetani" Siwezi sema "Ya kitoto" Manaa watoto ni watakatifu sana na michezo yao ni mitakatifu sana. Watoto wetu wanashindwa kusoa vizuri nyie mnafunga safari kwenda Dodoma ambako wanakaa kuangalia Bunge wakitegemea kuna utetezi mtaufanya katika mchango yenu badala yake wanakuja kumsikia:-

Juma Nkamia: "Siongei na Mbwa, naongea na Mwenye Mbwa" Alipotakiwa kufuta kauli akakataa kwa kudai aliyeambiwa si mtu makini (Mbwa)
Mh. Serukamba: "Come on fu......k you" Hapo ilitokea bila woga hata pale baada ya Mh Makinda kuahidi kuwatoa wabunge wanaotoa matusi lakini huyu hakutolewa baadaye inasemekana aliomba radhi kwani alikuwa ameteleza.
Mh. Mwigulu Nchemba: "Wakubwa tunapoongea mtoto wa kiume unatakiwa ukae kimya. Hakutolewa na hakuomba radhi nadhani kwasbabu ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM.

Tahadhari sisi wananchi tuliowachagua tunadhani ni wakati sasa muonje machungu ya KODI Tutawataka Muanze kukatwa kodi kwenye mishahara tunayowalipa, kwani mnafanya upuuzi ndani ya BUNGE. Mmekuwa mkinajisi Utukufu wa Bunge kwa kauli zenu chafu.

jamani hii post imenilazimu kutafuta CV ya Ndugai job. ipo hivi

[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD]Open University of Tanzania[/TD]
[TD="align: center"]LLB[/TD]
[TD="align: center"]2000[/TD]
[TD="align: center"]Todate[/TD]
[TD="align: center"]NOT COMPLETED[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Norway[/TD]
[TD="align: center"]MSc. in Mgt. Natural Resources&Sustainable Agric.[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]1996[/TD]
[TD="align: center"]MASTERS DEGREE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Norway[/TD]
[TD="align: center"]PG Diploma in Mgt of Natural Resources[/TD]
[TD="align: center"]1994[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]POSTGRADUTE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]University of Dar es Salaam[/TD]
[TD="align: center"]BSc.(Zoology Wildlife Ecology)[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]
[TD="align: center"]1993[/TD]
[TD="align: center"]GRADUATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MWEKA Wildlife College[/TD]
[TD="align: center"]Diploma in Wildlife Management[/TD]
[TD="align: center"]1986[/TD]
[TD="align: center"]1988[/TD]
[TD="align: center"]DIPLOMA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Old Moshi High School[/TD]
[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1982[/TD]
[TD="align: center"]1984[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kibaha Secondary School[/TD]
[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1978[/TD]
[TD="align: center"]1981[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Matare Primary School[/TD]
[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1971[/TD]
[TD="align: center"]1977[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

kupitia link hii (Parliament of Tanzania) Nimegundua kumbe tunamwonea ndugai wa watu bure jamani, Huyu mheshimiwa sifa zake ni kwa wanyama zaidi, ana utaalamu wa kudeal na wanyama kuanzia diploma hadi masters, na sichelei kusema anapoongoza hapo anahisi anaongoza kundi la wanyama na wanatakiwa kwenda pale anapotaka, akasahau kuwa anaowaongoza ni binadamu tena wenye falsafa za ufahamu wa mwanadamu na sheria za maisha ya mwanadamu,
Kwa kifupi nafasi hii haimfai, na nashauri serikali yetu na wabunge waangalie CV, huyu jamaa alitakiwa awe Tarangire huko, au manyara, au Mikumi au Mkomazi ndo panamfaa, sio mahali hapo pa kufanya maamuzi yanayohusi raia.
 
Hata Nyerere (RIP) aliwahi kutabiri mpasuko ndani ya CCM hivyo siyo mageni
 
Hakuna kitu kama hicho wala hawajakaa kwani utakuwa ni ujinga umtoe Ndugai ili umuweke nani? Mwigulu?
Hayo ni mawazo ya wapinzani tena sio Wabunge wao ila ndoto za mashabiki
 
Ngoja tupime kwanza kama hii uzi ni genuine au ya kichina yaani Mchemba innovated mtego wa kutuingiza mkenge. Sitaongea kwa sasa ngoja nifanye assessment ya authenticity yake.
 
Labda kama wamezaliwa wengine, hili neno ccm ni kansa ya koo, wako ki maslahi zaidi, hawajui kilicho wapeleka mjengoni. Sitegemei kama wanaweza kuwa na ujasiri kiasi hicho, lets wait.
 
Je kama ngugai akitoka kweli kuna jema litakalo fanywa na serikali ya awamu ya nne?
 
Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa mwandishi wa habari aliyeko Dodoma, anasema wabunge wa CCM hasa wale wanaojulikana kama wapambanaji wa ufisadi na wengine,wamekuwa na vikao juzi, jana na leo asubuhi wamekubaliana kuwa ni lazima aondoke kwenye unaibu spika kwa vile amekuwa akitumia jazba badala ya kuzingatia kanuni kwa vile hakuna kanuni inayomruhusu spika kumfungia vikao 5 papo kwa papo.

Pia wanadai amewaharibia mkakati wao ambao walikwisha upanga wa kumfungia Lema kufuatia tuhuma za kumsema Rais kuwa ni mdini, wanadai akifungiwa tena ataonekana anaonewa na hivyo kumpandisha juu kisiasa, kilichowaudhi ni pale walipomwita na hakwenda kuwasikiliza zaidi ya kuwaambia kuwa yupo bize na hakuna kanuni iliyovunjwa, pia akasikika akisema kuwa hizo ni fitna za Sitta kukosa uspika.

Leo wamekubaliana kupeleka azimio lao kwa Pinda na Jenister Mhagama kwa hoja kuwa Ndugai kwa kutumia jazba bila kufuata kanuni anasabisha chama kionekane dhaifu kuwa kinaogopa wapinzani hivyo kukifanya kidharauliwe na kuchukiwa na jamii.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa maazimio yamewekwa kwa maandishi na wamechaguliwa watu wawili kuyapeleka mbele.

Mchakato unaendelea tusubiri tuone.

habari njema hizi!mjenga na mbomoa nchi ni mimi wewe na yule,hakika tukiamua tu tunaweza.
 
Pinda ataishia kusema:
... Nadhani
... Napata shida
... a a, basi tuliangalie hili
 
Back
Top Bottom