Wabunge CCM Wataka Ndugai ang'oke

Wabunge CCM Wataka Ndugai ang'oke

Nguvu ya Hoja

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
276
Reaction score
125
Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa mwandishi wa habari aliyeko Dodoma, anasema wabunge wa CCM hasa wale wanaojulikana kama wapambanaji wa ufisadi na wengine,wamekuwa na vikao juzi, jana na leo asubuhi wamekubaliana kuwa ni lazima aondoke kwenye unaibu spika kwa vile amekuwa akitumia jazba badala ya kuzingatia kanuni kwa vile hakuna kanuni inayomruhusu spika kumfungia vikao 5 papo kwa papo.

Pia wanadai amewaharibia mkakati wao ambao walikwisha upanga wa kumfungia Lema kufuatia tuhuma za kumsema Rais kuwa ni mdini, wanadai akifungiwa tena ataonekana anaonewa na hivyo kumpandisha juu kisiasa, kilichowaudhi ni pale walipomwita na hakwenda kuwasikiliza zaidi ya kuwaambia kuwa yupo bize na hakuna kanuni iliyovunjwa, pia akasikika akisema kuwa hizo ni fitna za Sitta kukosa uspika.

Leo wamekubaliana kupeleka azimio lao kwa Pinda na Jenister Mhagama kwa hoja kuwa Ndugai kwa kutumia jazba bila kufuata kanuni anasabisha chama kionekane dhaifu kuwa kinaogopa wapinzani hivyo kukifanya kidharauliwe na kuchukiwa na jamii.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa maazimio yamewekwa kwa maandishi na wamechaguliwa watu wawili kuyapeleka mbele.

Mchakato unaendelea tusubiri tuone.
 
Naunga mkono hoja
kwa taarifa za uhakika kutoka kwa mwandishi wa habari aliyeko dodoma,anasema wabunge wa ccm hasa wale wanaojulikana kama wapambanaji wa ufisadi na wengine,wamekuwa na vikao juzi,jana na leo asubuhi wamekubaliana kuwa ni lazima aondoke kwenye unaibu spika kwa vile amekuwa akitumia jazba badala ya kuzingatia kanuni kwa vile hakuna kanuni inayomruhusu spika kumfungia vikao 5 papo kwa papo. Pia wanadai amewaharibia mkakati wao ambao walikwisha upanga wa kumfungia lema kufuatia tuhuma za kumsema rais kuwa ni mdini,wanadai akifungiwa tena ataonekana anaonewa na hivyo kumpandisha juu kisiasa,kilichowaudhi ni pale walipomwita na hakwenda kuwasikiliza zaidi ya kuwaambia kuwa yupo bize na hakuna kanuni iliyovunjwa,pia akasikika akisema kuwa hizo ni fitna za sitta kukosa uspika. Leo wamekubaliana kupeleka azimio lao kwa pinda na jenister mhagama kwa hoja kuwa ndugai kwa kutumia jazba bila kufuata kanuni anasabisha chama kionekane dhaifu kuwa kinaogopa wapinzani hivyo kukifanya kidharauliwe na kuchukiwa na jamii. Kwa mujibu wa mtoa taarifa maazimio yamewekwa kwa maandishi na wamechaguliwa watu wawili kuyapeleka mbele. Mchakato unaendelea tusubiri tuone.
 
Kwa CCM sina hakika kama hili litatokea labda waungane na upinzani hapo issue yao itawezekana,ni ukweli usiopingika kuwa job anatumia hasira kuongoza bunge na pale anaposimama mtu wa CCM utamckia anasema mh A endelea na wewe B kaa chini{hata ile neno "mheshimiwa" kwa upinzani siku hiz haweki} naweza ona hapa kuna beef kati ya L na J
 
CCM in kitu basi? Yaani wanatukana matusi ya nguoni halafu wanawabambikizia wenzao kuwa wametukana na kuwafukuza bungeni. Kwa stahili hiyo wanawainua wapinzani juu bila hata kufikiri.
 
Kwa ccm sina hakika kama hili litatokea labda waungane na upinzani hapo issue yao itawezekana,ni ukweli usiopingika kuwa job anatumia hasira kuongoza bunge na pale anaposimama mtu wa ccm utamckia anasema mh A endelea na wewe B kaa chini{hata ile neno "mheshimiwa" kwa upinzani siku hiz haweki} naweza ona hapa kuna beef kati ya L na J
....Best hili linawezekana kabisa kwani hata humo ccm kwenyewe kuna baadhi ya wabunge wanaoamini kiukweli kabisa kuwa serikali yao kuna maeneo inachemka isipokuwa kwa kuwa Magambani inawanyima uwanja wa kuwachana wenzao!
 
Niko pembeni nangoja yatokee haya yaliyonenwa
 
kumbe ndani ya CCM bado kunawatu wanaakili;.
 
  • Thanks
Reactions: mij
Cha kwanza sioni ukweli katika habari hii,ndugai amewekwa hapo na ccm ili kulinda maslahi yao na actually alichokifanya ni part ya kulinda maslahi yenyewe,sasa alichokosea hapo ni kitu gani?pili swala la Lema na udini mbona liko wazi?njoo ukasali msikiti wa pangani hapa Arusha hayo mbona ni mambo ya kawaida?pili kwani Radio imani inachikisema au kutangaza mara zote kabla ya the soo called adhabu ya kufungiwa haukijui wewe?na mwenye uwezo wa kukikemea kama sio RAIS ni nani?tatu kampeni zimekuwa zikifanyika sana misikitini hasa za CCM na huo ni ukweli usiopingika,juzi tu nikusaidie KINANA baada ya kuwekwa kuwa katibu mkuu wa CCM aliswali na sisi hapa ARUSHA,na alianza mambo ya siasa kwa kukifagilia chama,jamani misikitini pamekuwa mahali pa kufanyia kampeni,najua wenzangu hawatapenda kwanini nimesema haya lakini ni lazima tuweke wazi kwani kesho na kesho kutwa CCM ilimsimamisha mkristu and is most likely je itakuwaje?kampeni zitaendelea misikitini au itakuwaje?
 
CCM kila siku wanasema tuache itikadi tunapojadli maswali ya kitaifa,kama jana uliangalia issue aliyokuwa analalamikia jj mnyika kuhusu Rais kuanzisha gv,unit ya kusimamia miradi ya kitaifa,John alijenga hoja mpk sisi huku mtaani tukamuelewa ila wana CCM kwa wingi wao wakakataa kata kata na kwa vijembe vya hapa na pale,nwys acha tuone kama CCM wanaweza mpiga chini Job
 
Kiti cha spika wa Bunge kimepwaya sana, na inanipa picha kwamba kuwa Spika wa Bunge kwa nchi yetu siyo ishu sana hata mimi MvaaTai naweza kukikalia tu nikawa nachemka lakini maisha yanaenda mbele
 
I see, kwa hiyo kesi ya nyani akahukumu ngedere? Huyuhuyu Pinda ambaye amekuwa akitetea watendaji wabovu serikalini wasijiuzulu ndiye anayepelekewa habari ya Ndugai kung'olewa halafu tutarajie kwamba atafanya lolote? Labda wangeitoa kama hoja bungeni ili wabunge wapige kura, ingeweza kuleta maana zaidi. Lakini kuipeleka kwa Pinda ni kupoteza muda tu. Pinda na Ndugai hawana hata tofauti.
 
Kwa vyovyote Lema amejiweka ktk nafasi nzuri ya kujijenga kisiasa..UAMUZI WOWOTE UTAMWEKA JUU ZAIDI.
 
CCM wamchague wenyewe halafu wamtoe wenyewe?
si ndio wataonekana dhaifu zaidi?
labda kama wamejiwa na roho wa haki na ukweli ndio wabadilike.
Ile haoja ya Lissu kumngoa spika Makinda imeishia wapi tena?
 
Wakimaliza wamngo'oe na yule mtetezi wa ikulu, sijui Bukuvi anaboa sana.
 
Ngoja Lukuvi awasikie watapigwa mkwara wa kufa wote watanywea.
Hilo suala la Lema ni mdini hapo sintawaelewa, aliyekuwa anatakiwa aongee kuhusu haya mambo ya kidini ni Rais na si Lema, sasa kama Rais na wasaidizi wake wako kimya ina maana wao (Rais & Co.) ndiyo wanahusika na wanaopandikiza huo udini
 
Back
Top Bottom