Wabunge CCM walalama mkutano wao na Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM walalama mkutano wao na Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 21, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,358
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Wabunge CCM walalama mkutano wao na Kikwete
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 20 November 2011 20:53
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Mwandishi Wetu, Dodoma
  BAADHI ya wabunge wa CCM wamelalamikia mkutano ulioitishwa baina yao na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kwamba haukuwa na tija tofauti na matarajio makubwa waliyokuwa nayo.

  Rais Kikwete, juzi usiku alikutana na wabunge wa chama chake katika Ukumbi wa St. Gasper nje kidogo ya Mji wa Dodoma lakini habari zilizopatikana jana zilisema mkutano huo uligeuka kuwa wa "chakula cha jioni."

  "Mkutano wenyewe haukuwa na tija, kwanza tulisubiri sana hadi watu wakaanza kukata tamaa, lakini hata Rais alipofika hakukuwa na mkutano kama tulivyoambiwa na badala yake tuliambiwa ni dinner tu (chakula cha usiku) halafu mazungumzo ni siku nyingine," alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria hafla hiyo.

  Mbunge mwingine alisema: "Wengine tulikuwa tumejipanga kumuomba Rais achukue hatua kuhusu mambo yanavyokwenda ndivyo sivyo, serikalini na kwenye chama, lakini ndiyo hivyo, haikuwezekana, maana tuliishia kula na baadaye kutawanyika."

  Usiku huo, Rais Kikwete alitoa hotuba fupi yenye sura ya salaam kwa wabunge hao huku akiwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya bungeni na kwa ujasiri wao wa kutokuwa wanyonge kwenye mijadala bungeni.

  Kikwete alinukuliwa na vyanzo vyetu akiwapongeza wabunge wa CCM kwa jinsi walivyoutetea Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 pamoja taarifa za Kamati mbili za Bunge zilizowasilishwa kuhusu sekta ya gesi na ile ya Kamati Teule.

  Mbunge mwingine aliyezungumza na gazeti hili alisema: "Sisi ndiyo tulimwomba Rais aje kuzungumza nasi, lakini hatujui ni nini kilichotokea, tumeahidiwa kwamba huenda akaja kusema na sisi tutakapokutana mwezi Februari mwakani."

  Kwa mujibu wa mbunge huyo, walikuwa wamejiandaa kuzungumzia matatizo ya nchi hasa kuyumba kwa uchumi, hali ngumu ya maisha na udhaifu katika utendaji wa Serikali ambao umekuwa ukiwaweka katika wakati mgumu kuwakabili wapinzani bungeni.

  "Mambo hayaendi kabisa, watendaji serikalini ni kama hawaoni, sasa tulidhani kwamba fursa hii ilikuwa ni ya kumshauri Rais aweze kuchukua hatua zaidi, vinginevyo tutakwama, hatuna matumaini kadri siku zinavyokwenda," alisema mbunge huyo.

  Jitihada za kumpata Mwenyekiti wa Kamati ya wabunge wa CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na katibu wa kamati hiyo, Jenister Mhagama (Mbunge wa Peramiho), kuzungumzia mkutano huo hazikufanikiwa.

  Taarifa rasmi kutoka Ikulu ilisema Rais alizungumza na wabunge wa CCM kisha kupata nao chakula cha usiku katika ukumbi wa St. Gasper.

  Taarifa hiyo ilisema Kikwete aliwapa changamoto wabunge hao kwenda kwa wapiga kura wao kuwaelimisha kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
  Taarifa hiyo imemnukuu Mwenyekiti huyo wa CCM akiwasisitizia wabunge hao umuhimu wa kutoa elimu kuhusu suala hilo, kutokana na kuwapo kwa upotoshaji unaofanywa kuhusu mchakato wa upatikanaji wa Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge.

  Mawazo ya wabunge

  Baadhi ya wabunge walisema kutoruhusiwa kwao juzi kuzungumza na Rais kunaweza kuwa kumechochewa na kikao cha wabunge wa CCM kilichokutana Alhamisi usiku, Novemba 17, mwaka huu chini ya Pinda.

  Katika kikao hicho, wabunge hao waliripotiwa kugeuka mbogo hasa baada ya kupewa taarifa kuhusu kile kilichokuwemo kwenye taarifa za kamati mbili za Bunge kwamba kulikuwa na madudu ambayo yanaichafua Serikali.

  Kutokana na hali hiyo, wabunge wanadaiwa kukataa kupokea maelezo ya kina kuhusu taarifa hizo na kumwambia Pinda kwamba taarifa hizo zisomwe kama zilivyo bungeni ili na wao wapate fursa ya kuchangia ndani ya ukumbi wa Bunge kama ilivyo kwa wapinzani.

  "Tulikataa maana tungekesha, halafu ni kama walitaka kutupunguza nguvu na sisi tukawa na msimamo kwa kutaka zisomwe kama zilivyo, tumechoka kubebana maana hawa wenzetu serikalini ni kama hawasikii, tunabebana mpaka lini!," alisema mbunge mwingine ambaye kama wenzake, hakutaka kutajwa gazetini.

  Katika siku za karibuni, wabunge wa CCM wameripotiwa kuwa wakali hasa wakieleza kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya mawaziri na watendaji wengine serikalini.

  Wakati wa Bunge la Bajeti, walikuwa ni wabunge wa CCM ambao walikuwa mwiba kwa mawaziri wengi kiasi cha kufikia hatua ya kukwamisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, hivyo Serikali kuamua kuiondoa kwenda kujipanga upya.

  Pia wabunge hao wakiwa kwenye kikao cha kamati ya chama, walikataa kusikiliza maelezo ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, wakisema lazima iwasilishwe bungeni ili wachangie kama wabunge wengine.

  Katika Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa Ijumaa iliyopita, wabunge hao wa CCM waliwasilisha majedwali ya marekebisho ya muswada huo kwa wingi kiasi cha kusababisha kuitishwa kwa kikao cha kamati yao kuwasihi kuondoa baadhi ya hoja zao.

  Imedaiwa kwamba hatua ya kupitiwa kwa majedwali hayo katika kikao hicho cha chama, ilitokana na wabunge hao wa CCM kuyawasilisha zaidi ya 40 huku mengine yakiwa na mapendekezo ya marekebisho ambayo yanadaiwa kuwa yalibeba ajenda zenye sura ya upinzani.

  Ni kutokana na hali hiyo, baadhi yao wanadhani kwamba huenda hilo likawa moja ya mambo yaliyowakwaza kuzungumza na Rais.

  Kuwasili kwa Rais
  Rais Kikwete aliwasili Dodoma juzi, jioni kwa lengo la kuongoza vikao vya CCM ambavyo ni Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho.

  Taarifa iliyotolewa jana mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye inaonyesha kuwa vikao hivyo vinaanza leo hado Novemba 27, mwaka huu.

  Nape katika taarifa hiyo alisema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itakutana leo na kesho na kufuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Novemba 23 na 24, wakati Novemba 25 hadi 27, kutakuwa na semina ya watendaji wa CCM ngazi ya taifa hadi wilaya.

  Washiriki wa semina hiyo watakuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, Sekretarieti za Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi ambazo ni UWT, UVCCM na WAZAZI, makatibu wa CCM wa mikoa na Wilaya zote nchini.

  SOURCE: Mwananchi  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kumbe mnajua kuwa huwa mnabebana! Na kwa nini mmbebe mtu anayefanya madudu na ufisadi? Ndio maana tumewachoka!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UKAIDI WA CHAMA CHA MAPINDUZI JUU YA 'MUSWADA WA MAKINDA' NA KUKUMBATIA MKONDO WA IKULU KUTEREMSHA KATIBA YA KISERIKALI BADALA YA KATIBA YA WANANCHI SASA KUWAGHARIMU VITI VYA UBUNGE TOKA 250 HADI 78 UCHAGUZI UJAO

  Si siri tena kwamba kwa jinsi Rais Kikwete na washauri wake wamekataa kusikiliza Wa-Tanzania kwa ujumla wetu na hata wajumbe chama chake mwenyewe hivyo kuanza kuwakimbia ovyo, NAPENDA NIELEZE HAPA LEO HII KWAMBA ENDAPO HAWATORUDI WALAU HATUA 10 NYUMA katika hili na kuweka wananchi mbele katika uundwaji wa SHERIA ITKAYOSIMAMIA UTUNGAJI WA KATIBA MPYA basi wategemee tu MDORORO KWA KILA KITU TANGU SASA HADI MWISHO WA YO NA TENA KWA AIBU KUBWA MBELE YA SAFARI.

  Ama kwa mkusudi au kwa kukusudia tu, Rais Kikwete ameifanya KAMBI YA UPINZANI NA ASASI ZA KIRAIA NCHINI KUIBUKA NA NGUVU KUBWA AJABU toka Dodoma tangu Sheria ya Ikulu ilipopitishwa bungeni. Kwa upande mwingine, CCM kinatoka Dodoma, baada ya hii SHERIA YA KUKWEPWA KAMA UKOMA NA WANANCHI WOTE NCHINI, kikiwa ni DHAIFU ZAIDI MACHONI MWAO WAPIGA KURA nchini kuliko hata ule udhaifu waliokwishajizolea tangu chama hicho kudaiwa kuiba kuraa zetu hapo mwaka 2010.

  Kwa mantiki hiyo hapo juu, kwa watu wenye kuona mbali sana, ni raisi sana leo KUTABIRI KWAMBA MUSWADA WA MAKINDA (Kama kashfa za EPA, Dowans na Richmond) hivi leo lishageuka mwiba kwa chama hiki na kwamba ndicho kitakachokua sababu kuu ya kuchangia KUPUNGUZA IDADI YA WABUNGE WAKE TOKA huko 250 hadi 78 ifikapo mwaka 2015.

  Hakika ni huruma, ni uchungu mkubwa lakini ndo kama hivyo HUKUMU UMESHATOKA KWA MAHAKAMA KUU YA UMMA hivyo mbunge mwingine yeyote awaye ama wa CCM au hata wa kambi ya upinzani atakayeonekana kulitetea kwa namna yoyote huu MUSWADA WA MAKINDA aka MKONDO WA KIKWETE KUELEKEA UPATIKANAJI WA KILE WANACHOKIITA 'KATIBA MPYA' lakini ya kiserikali, basi ni wazi mbunge huyo akafahamu kwamba KITI CHAKE CHA UBUNGE TAYARI KINAHESABIWA kubaki wazi kugombaniwa na wapinzani wake watakaoamua kusimama upande wa Umma wa Tanzania na wala si upande wa genge la wajanja wachache watafunao nchi bila huruma.

  Wenye masikio wasikie kwamba pindi tu Wapinzani watakapoanza kwenda kwa wananchi juu ya hili basi hadi hapo ndipo Jua la CCM na WAKAIDI WAKE wote litakapokua limeanza kuzama kiuhakika kweli kweli. Na hizo ndizo alama za nyakati hizi huku tukisema HAKUNA KULALA; Taifa ni kubwa zaidi kuliko Ana Makinda na zaidi hata ya bunge pia!!

  Utaifa mbeeeele kama tai mpaka tupate KATIBA MPYA YA WANANCHI hata kama itatuchukua miaka 100.
  Itakua ni shughuli nzito haijapatakuonekana kwa serikali ya Rais Kikwete kufanikiwa na jambo ambalo wananchi hatuliafiki wala kushirikiswa TANGU HATUA ZAKE ZOTE ZA AWALI!!!!


  Ila tu namuombea sana afya nje Rais Kikwete naye aje akaionje utamu wa HAKI NA UTU WA MTANZANIA pindi unpotetewa na KATIBA MPYA unaotungwa kwa UDEREVA wa wananchi wenyewe na wala si wa kuteremshwa na Serikali kama mane mane toka angani.

  Dalili zote za KURA ZA CHUKI ziko wazi tangu kwenye REFERENDUM kupitishwa rasimu hadi kwenye Uchaguzi Mkuu wenyewe mnamo 2015.

  Yeyote anayeinuia kugombe kiti chochote hata cha udiwani tu huko mbele ya safari; alama ndio hizo au tukuage pamoja na Rais Kikwete pindi anaporudi nyumbani baada ya kustaafu.
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wezi tuu ccm hakuna lolote!
   
 5. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo nashindwa kuwaelewa wabunge wa CCM,hawa wabunge wa CCM wanawakilisha wananchi na masilahi ya waliowachagua au wanawakilisha CCM katika bunge?Kwa sababu wanapokua bungeni hawatetei masilahi ya wananchi kwa makusudi au kwa shinikizo la chama chao hata kwa mambo ambayo ni wazi kwa masilahi ya wananchi.Uzoefu unaonyesha ya kwamba ya CCM kuanzia ngazi ya juu imejaa mafisadi,wala rushwa,wazembe n.k.Kitendo cha wabunge hao kutoa maamuzi yao kwa shikizo la chama chao HAWAWATENDEI HAKI WALIOWACHAGUA BALI WANALINDA MASILHI YA KUNDI DOGO LA WATU VIONGOZI WA CCM NA FAMILIA ZAO.Kitendo cha kutetea masilahi ya wananchi waliowachagua bungeni na baadae kulalamika nje ya bunge NI USALITI NA MATUSI KWA WANANCHI WANALIOWACHAGUA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  USHIRIKI WA WABUNGE WA CCM KUPITISHA HUU MUSWADA WA MAKINDA NI MITHILI YA AMRI YA KIJESHI KUTENDA KWANZA HAALAFU MASWALI BAADAYE JAPO SASA NI WAZI KWAMBA WENGI WAO NI MAJUTO TUPU MOYONI

  Ukisoma taarifa hiyo hapo juu magazetini ndipo mtu utakapogundua kwamba Upitishwaji wa HUU MUSWADA CHUKIZO kule Dodoma, kwao wao wabunge wa CCM, ilikua kama vile waliamrishwa kwamba KWANZA KAUPITISHE HUU MUSWADA HIVO HIVO hata kama hukubaliani nayo kisha kama kuna maswali zaidi basi uje ukatuulize baadaye.

  Lakini sasa wenzetu waheshimiwa hawa ukweli ulipowafikia kwamba walichokifanya bungeni Dodoma si tu kwamba ni utungaji wa sheria inayopingana na katiba ya sasa tunayokusudia kuweka kapuni bali ukweli ni kwamba mpaka hivi sasa wao na wananchi waheshimiwa wapiga kura ni kwamba kamwe hawatokaa waelewane tena lugha kwa usaliti wao wa kwenda Dodoma KUTETEA MASLAHI YA CHAMA CHAO ZAIDI na kuamua kutelekeza jukumu lao la kwanza walioiombea kazi KWENDA LEGICO KUTETEA MASLAHI YA UMMA NA MASLAHI YA UMMA tu kwa kipindi chote.

  Kwa kweli ilishangaza sana walipomuana hadi Mzee wa Kiraracha kaamua kujiondokea zake KWA SOLIDARITY na wabunge wa CHADEMA huku wao wakianza kubeza kitendo hicho cha ki-ujasiri na ki-uzalendo zaidi KUTETEA MASLAHI YA UMMA na kutoka nje hata kama idadi yenu ni ndogo kiasi cha kutoweza kubadilisha chochote.

  Hadi hapa kikubwa zaidi hapo ni ULE UJUMBE walioutuma wale wabunge waliojiamulia kutoka nje na NAMNA YA AJABU JINSI AMBVYO UJUMBE WAO HUO TAYARI umekwishapokelewa na wananchi wa rika na matabaka yote nchini hadi hivi sasa. Hakika ni jambo gumu sana kulishinda umma hta mtu ungelikua na majeshi zaidi ya Adolf Hitler wa miaka hiyo.

  Kwa mtaji wa mswada huu wa hivi majuzi, wanasiasa si kipindi kirefu sana kuanza kujipanga upya katika nyumb mbalimbli watakazoziona kuwa ni salama zaidi hata kabla ya kipindi cha uchaghuzi ujao kuwadia.
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anawapongeza vilaza wenzake kwa kutoa matusi mfululizo kwa siku tano bila kujibu hoja.Bure kabisa hawa magamba.
   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanajua sababu ya uzembe serikalini kwamba ni kubebana sasa kwann hawataki kutatua tatizo badala yake wanaangaika kutaka rais achukue hatua! zipi? Wakati nyinyi(wabunge) wenyewe mmekubaliana na hali iliyopo?
   
 9. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  CCM hii imefikia ukingoni kwani sioni namna nyingine ambayo ccm itarudia hali yake ya awali
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Chama chochote cha siasa na au kiongozi yeyote mwanasiasa akitamani kupata njia ya mkato zaidi kuanguka kwa kishindo kisiasa basi njia hiyo ni kule kwenda kinyume na umma; hadi hapo ni kwamba hata kama utaendelea kuonekan kwa BADO UMO UMO KWANZA kakini ukweli ni kwamba kufunikwa kwako na gamba gumu sana la historia ni swala la muda tu.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna wabunge wa CCM wanajua wanachokifanya. Sitta, Lowassa, January Makamba hawakuchangia kwenye huu muswada! Wether wanakubaliana na wenzao wa ccm au la hilo ni jengine lakini mbele ya wananchi hawajasema chochote. Watu kama wakina Anna Kilango na Lucinde na wana-CUF kama Hamad Rashid, Mnyaa watapata shida sana kurudi bungeni. Na ikitokea viti maalum vinafutwa bunge lijali litakuwa tofauti sana na sasa!
   
 12. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Wanafiki wakubwa hawa, wangemchana live kama kweli wanataka mabadiliko. Wakati wa uchangiaji walionyesha uwezo wa hali ya juu wa kujipendekeza na kujikomba kwa Dr Dr Dr Dr Dr JK, hasa wale waliokuwa wapambanaji wa ufisadi enzi za mzee Six, wakiongozwa na Sendeka na Kilango
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Deleted following post repetition
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  SAWA NA MIMEA VYAMA VYA SIASA NAVYO HUZALIWA, HUJITAMBALIA KWA SHIDA SANA, HUCHANUKA NA MWISHO WA SIKU VIKIKOSA DIRA, UBUNIFU NA KUUNGWA MKONO NA UMMA MWISHOWE HUFA NA KUZIKWA NA HISTORIA

  Mbaya zaidi ni kwamba wapo wabunge kibo ndani ya CCM ambao kama si kutumia kwao KIONAMBALI YAANI SAYANSI YA UCHAKACHUAJI WA UCHAGUZI majimboni mwao huko.

  Kwa kusema ukweli, yaani hata wao wenyewe tu wanafahamu kwamba wao hawauziki wala hawanunuliki kwa wapiga kura; ndio watu hao hao tuwatarajie kwenda kunadi muswada / sheria chukizo tangu mwanzo wa uundwaji wake hadi wananchi tukapate kuwaelewa somo na hatimaye kuwaunda mkono???

  Hebu hapa chini tukajitazamie vyama kongwe vilivyowaki kuwika sana katika historia ya ulimwengu lakini kwa makosa madogo madogo tu ya KUWACHUKULIA WANANCHI MAHAYAWANI mwisho vikakunjwa mtindo wa mkeka uliotapakaa choo cha binadamu na watu kuamua kuvitupilia mbali milele:  Once Mighty Party Falls, and Worries Grip Japan


  By MARTIN FACKLER

  Published: February 24, 2010

  TOKYO - What does a political party built on power and patronage, with few philosophical or ideological underpinnings, do when it is defeated and driven into the opposition? In the case of Japan's once formidable Liberal Democratic Party, it implodes like an old Las Vegas hotel being demolished.

  Enlarge This Image
  [​IMG]
  Junji Kurokawa/Associated Press

  Sadakazu Tanigaki, Liberal Democratic chief, right, and Prime Minister Yukio Hatoyama of the Democratic Party, seated left.

  This has led to hand-wringing in the Japanese press that the nation may be headed toward another period of de facto one-party government, only this time with the ascendant Democratic Party in charge.

  But optimists here say the Liberal Democrats' decline may be just the first step toward a much bigger political change: the destruction of the old structures of Japan's stunted democracy and the rise of new, more ideologically coherent parties in a livelier and more competitive political system.

  To see how far the Liberal Democrats have fallen, look no further than the party's cavernous headquarters in central Tokyo. The nine-story building, once the unchallenged seat of political power during much of the Liberal Democrats' half-century rule of Japan, has fallen eerily quiet and underused since the party's historic election defeat last summer.

  The party has become an empty shell of its former self. Thrust into the role of opposition party for the first time since its creation in 1955 (aside from a brief interlude in 1993), and with its number of lawmakers cut in half by last August's humiliating defeat, the party appears demoralized, devoid of fresh ideas and threatened by defections.

  Four lawmakers have indeed defected since the election, and speculation is rife that more will follow. The party's public approval ratings have never bounced back from the high teens, even as last summer's victor, the Democratic Party, has suffered a series of money scandals. Earlier this month, the party's own internal newspaper, the weekly Liberal Democrat, even warned that the party had virtually no hope of survival.

  "We haven't had experience as an opposition party," said Sadakazu Tanigaki, the Liberal Democratic Party chief and a former finance minister, who sat in a room filled with the unsmiling portraits of past party leaders. "People are running around wondering, ‘What do we do?' "
  For now, the contrast with the newly incumbent Democrats could not be starker.

  Despite fund-raising scandals, the Democrats still seem to brim with enthusiasm for their agenda of change, evident in their bustling, overcrowded offices just a block away, on a few floors of a building with a Pentax sign on top.

  With the Liberal Democrats in such obvious disarray, some now fear Japan faces the prospect of one-party rule by the Democrats. But many analysts and politicians say they do not expect the Democrats' hegemony to last long either, because they face many of the same weaknesses as the Liberal Democrats.

  "The Democratic Party has the same problem as the Liberal Democratic Party, in that both are broad tents filled with politicians of all ideological stripes," said Takeshi Sasaki, a professor of politics at Gakushuin University in Tokyo. "So long as Japan lacks modern political parties, it will lack true political competition."

  The Liberal Democrats, Mr. Sasaki and others say, ruled through much of the cold war with a hazily conservative platform built upon the bedrock of a close alliance with the United States, which also became a market for its exports. At the same time, it built up an imposing political machine that redistributed the fruits of Japan's postwar economic miracle to voters in less developed rural regions.

  Without that patronage machine, the party risks flying apart. In that, analysts say, it is more like the PRI in Mexico, which has yet to recover from its battering in 2000 after more than 70 uninterrupted years in power, than like political parties in the United States and Europe.

  "We never found a new direction after the fall of the Berlin Wall," said Mr. Tanigaki, the party chief, "and we are regretting that now." The party's shortcomings have become painfully apparent since its defeat, as it has failed to offer a clear-cut alternative to the Democrats' vaguely left-leaning plans to offer more aid to families and become more independent from Washington.

  Instead, the Liberal Democrats have adopted a short-term strategy of attacking the prime minister, Yukio Hatoyama, for the funding scandals involving him and the Democrats' power broker, Ichiro Ozawa. This has brought some support from voters, seen on Sunday when a Liberal Democratic candidate won an election for governor of Nagasaki prefecture. But political analysts and politicians say the approach could backfire if it appeared to lead Japan back into its former political paralysis.

  Indeed, there is growing frustration among conservatives at the party's inability to change. This became apparent last September when Mr. Tanigaki, 65, defeated a younger opponent, Taro Kono, 47, to lead the defeated party. Many younger lawmakers saw this as a move by the party's old guard to squelch Mr. Kono's promises to rejuvenate the party by such steps as abolishing its entrenched factions.

  Mr. Kono said the Liberal Democrats' only hope of victory was to reinvent themselves as a truly conservative party, with a clear agenda of small government and close ties with the United States. But he sounds a very pessimistic note about the party's future, so long as the old guard holds sway.

  He said the Liberal Democrats faced their next big test in parliamentary elections in July, when another defeat could prove a death blow.
  "People don't want the old Liberal Democratic Party," Mr. Kono said. "They want us to come back as a new, healthier party."

  But even if the Democrats win, they may soon face similar problems of internal divisions over policy, especially if they move beyond their current manifesto and into trickier issues like whether to raise taxes or cut social programs to rein in the budget deficits. When that happens, say analysts and politicians, the party could also break apart, paving the way for the radical reshuffling of parties along ideological lines that would complete the political revolution begun last summer.

  "After the breakup of the Liberal Democrats, it will be the Democrats' turn to fight internally and split," Kotaro Tamura, a Liberal Democratic lawmaker who left in December to join the incumbent Democrats. "That will be a big moment for Japanese democracy."

  A version of this article appeared in print on February 25, 2010, on page A10 of the National edition.

  SOURCE: Once Mighty Party Falls, and Worries Grip Japan - NYTimes.com
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Je, itakua vipi CCM ikija kuwa na sura zaidi ya hizi hapa chini hapo mbeleni kidogo?

  [SUP][/SUP] [​IMG] [​IMG]
  Puck cartoon by Frederick Burr Opper: "Lots of hunters after a very sick tiger" (1893)
   
 16. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hapa atawafanyeje.Katiba hacha waiunde wenyewe na NINAHAKIKA ITAWASURUBU WENYE
   
 17. N

  NIPENDEMIMI Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siamini
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wao walitegemea awaambie nini wakati aliyekuwa na ajenda ni yeye. Waache kulalama kwa kitu ambacho yeye hakuwaahidi!
   
 19. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mpaka kwenye hili unahitaji msaada wa kueleweshwa? Kweli wewe ni mwana CCM uliye na uelewa finyu!
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MUSWADA WA MAKINDA NI SAWA NA JUMBA LA DHAHABU ILIOJENGWA KATIKA MSINGI WA BISKUTI USWAHILINI

  Sheria ya Makinda iliopitishwa majuzi bungeni Dodoma ni sawa na jumba kuuuuubwa la kifahari liliojengwa kwa matofali ya dhahabu lakini chini yake likisimama juu ya MSINGI MARIDADI LAKINI ILIOJENGA KWA VIJIPANDE VYA BISKUTI.

  Kwa uelekeo huo, maana yake ni kwamba gharika la Umma wa Tanzania pindi tu utakapopiga basi tujue kwamba hakuna tena jumba hapo. Safari ndio hiyo inaendelea.

  Utaifa mbeeeeele kama tai, KATIBA MPYA kamwe hatutoiacha ianguke kama mane mane toka angani; KATIBA MPYA ni jukumu letu sisi wenyewe (unalienate right) kulitunga wenyewe TUKIWA TUMEUSHIKA USHUKANI SISI WENYEWE na wengine woote ikiwa ni pamoja na Rais, Ikulu, Bunge, Mwanasheria Mkuu na Serikali ya CCM kwa ujumla wake wakiwa ni sehemu ya ABIRIA WETU MUHIMU sana katika zoezi zima hili.
   
Loading...