Wabunge 50 Tanganyika 20 Zanzibar inakuwaje mgao huu??

Mbona mfano unao Tanzania? Hiyo tume ya Warioba si imeundwa kwa 50p ratio Zanzibar na bara? Au umeshasahau?

Mfano si Tanzania, huku kwetu tunachemsha,nataka mfano toka kwenye mataifa mengine yenye miungano,wapi umewahi kuona equal ratyio representation? Manaake usiwe mwepesi kukosoa wakati wewe ndio huelewi!

Kiufupi, hamna kitu kama hicho,population ndio inadetermine ratio ya uwakirishi, hata hivyo huku kwetu kmekuwa na upendeleo kwa Wazanzibar! Lakini wao hawalijui hilo! Nadhani na wewe ni mmojawao!

Ndio maana nimetoa mfano wa US,UK na kwingine kwingi,Wawakirishi huwa wanawakirisha watu,si Land!
 
Nimejaribu kupitia Rasimu nimeona hili la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano watakuwa 70, Tanganyika itatoa 50 na Zanzibar 20 ukiacha wale wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha watu wenye ulemavu na wengine mmoja mmoja kuwakilisha m'me na m'ke katika majimbo ya uchaguzi.,

Ivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2., inakuwaje nchi moja 50 nyengine 20??

Mbona hawa Tanganyika wanataka kuendelea kutuburuza tena kwene bunge? Ivi burundi nchi ndogo lakini inawakilisha wabunge sawa na nchi kubwa kwenye muungano wa afrika., inakuwaje Muungano huu wa Tanzania?

Nimeskia Kenya na Unganda wamevutiwa na Muungano huu uliotoka kwenye rasimu wa Tanzania wanataka kujiunga lakin sasa itakuwaje kwa mgao huu wa wabunge??

Duuu...hv jamani,viongozi wote hao 140 bado sijui wakuu wa mikoa,bado wabunge wa kuteuliwa,ma DC,viongozi wajuu kbs (Rais na Makamu wake) hivi watanzania tutaweza kuvumilia fedha zote za mishahara na marupu rupu watakayochukua hawa watu?

Wabunge 140 tu ni zaidi ya Tshs. 1,680,000,000/= kwa mwezi huoo...mmoja..!!Jamani,hii nchi kwa mtindo huu hatutafika..Mgawanyiko (GAPE) kati ya MATAJIRI na MASIKINI ndo utazidi kukuwa.

Yanini nchi masikini km hii kuwa na ruuundo la viongozi MZIGO? Naamini km walivyo MAWAZIRI MIZIGO hivi sasa,wapo pia WABUNGE MIZIGO...wao ni Bendera fuata upepo ilimradi mwisho wa mwezi ATM inasoma vyema.

Ni BORA km bado rasimu ina madudu km haya,tuanze upya ukusanyaji wa maoni..hii tuipige chini.

Mie binafsi hata suala la Serikali TATU bado siliafiki.Hivi,km nchi zimeungana,kuna haja gani ya kuwa na Serikali zaidi ya moja?

Marekani ni Muungano wa Nchi nyingi ndogo ndogo,mbona wao hawana Serikali zaidi ya moja? Mfumo wao wa Kiutawala wa "Gorvenors" ktk mikoa mbona uko poa tuu? Kwa nini ktk Muungano wetu huu tusiuige na kuufanyia kazi?! Sisi kazi yetu kuiga Upuuzi na Uchafu tu waufanyao watu wa Marekani na mataifa mengine ya Ulaya,lkn yaliyo mema,aaaa....

"SERIKALI TATU ITAVUNJA MUUNGANO.LAANA YA MWALIMU NYERERE INATUANDAMA TUSIPOKUWA MAKINI."

Alisema na Akisisitiza sana kuwa makini na Muungano,na kila mtu anakumbuka maneno ya mzee wetu yule...Jamani,tujihadhari,Unabii wa Mwl.Nyerere usije ukatimia kwa kukosa kwetu BUSARA na HEKIMA
 
Fumbua macho mkuu, hyo inawezekana vip? Tanganyika iwe sawa na zanzbr hata hvyo z azbr imepewa weng ukilingalisha na uwakilish wake ilitakiwa mpate wabunge 5! Tatizo lako unateswa na udini!

Hilo ndio tatizo lenu maana mtu akisema ukiweli atambiwa anasumbuliwa na udini. Acheni Tabia hii ya Umbumbumbu
 
sie muungano na hii mitwana tulilazimishwa na mpaka leo hatuutaki yote hii ni chuki yao dhidi ya uislam na wazanzibar km alivyosema pimbi wao nyerere

Kama wewe ni muislamu bila shaka unajua maiti hatukanwi.Kumwita Nyerere aliyekwisha kufa pimbi Mwenyezi Mungu akupe adhabu ile ikustahiliyo bado ungali hai.
 
Jiulize umoja wa mataifa kuna nchi chache tu zilizo na kura ya veto, kwa nini? Je ambazo hazina zinakosa sifa ya kuwa nchi/serikali. Huu unafiki wa kutokuukubali ukweli ndio unaenda kuua huu muungano.

Wewe hata maana ya veto huijui. Kaa kimya.
 
Wewe hata maana ya veto huijui. Kaa kimya.

Na hii ndio tofauti kubwa kati ya mtu anayechangia huku kashikiwa akili na anaye changia mawazo yake huru. Wewe aliyekushikia akili kasha kuelekeza serikali mbili basi. Unalazimika wala si hiari yako tena.
 
Ivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2., inakuwaje nchi moja 50 nyengine 20??

Mbona hawa Tanganyika wanataka kuendelea kutuburuza tena kwene bunge? Ivi burundi nchi ndogo lakini inawakilisha wabunge sawa na nchi kubwa kwenye muungano wa afrika., inakuwaje Muungano huu wa Tanzania?

Jaji Warioba HAIJAITENDEA HAKI Tanganyika,angetumia uwiano wa population Zanzibar ilistahili pungufu ya viti 10!

Ona Muungano wa USA uliofanyika kwa haki:California ina WABUNGE 55 KWA SABABU ni Jimbo kubwa zaidi na most populated na Wisconsin ina MBUNGE 1 KWA SABABU ni least populated!

Bunge la katiba lipunguze idadi hizi za wabunge wa ZNZ
 
Warioba kafanya sawa ila uwiano ungeendana na idadi ya watu wanaowakilishwa na wabunge! 60 : 10

Umekosea, Idadi ya tz inakaribia 50 mil. wakati Z'bar haijafikia 1 mil. Huoni uwakilishaji wa watu kwa haki unatakiwa kuwa na wabunge walau tuwapendelee wapate 50 : 5, badala ya 50 : 1. Idadi yao haijafika hata robo ya wakazi wa Dar!
 
Jaji Warioba HAIJAITENDEA HAKI Tanganyika,angetumia uwiano wa population Zanzibar ilistahili pungufu ya viti 10!

Ona Muungano wa USA uliofanyika kwa haki:California ina WABUNGE 55 KWA SABABU ni Jimbo kubwa zaidi na most populated na Wisconsin ina MBUNGE 1 KWA SABABU ni least populated!

Bunge la katiba lipunguze idadi hizi za wabunge wa ZNZ

hawaelewi hao, ni ubishi tuu,malafyale hawa wenyewe kilakitu wanaona wanaonewa.! ungekuwa ushauri wangu tngeuvunja kabisa na huo muungano, they are indeed trouble makers! tutakuja jutia baadaye
 
Iwapo nchi nyingine zitapenda kuingia kwenye huu muungano (federation) kitatumika kigezo hicho hicho cha uwakilishi wa wananchi kama zinavyotumia 'federations' nyingine mf. USA, UK, Switzerland, India, Urusi n.k. Muungano wa namna hii, hadi kufikia muungano wa Afrika nzima ndio iliyokuwa dhamira halisi ya waanzilishi wa huu muungano.
 
Mkuu acha kurukaruka. Tanganyika ina watu wengi zaidi wanaohitaji gharama kubwa zaidi kiulinzi kuliko Zanzibar. Hapa ndipo ile Option I uliyodai haina mashiko inavyoonesha jinsi ilivyo na mashiko.

mkuu umeniwahi, kwanini kwenye ulinzi atumie kanuni ambayo ataki itumike kwenye idadi ya wabunge?
 
lakini kama watakua taifa huru sidhani kama priority itakua ni kifaru cha vita,ukichukulia mahali ilipo,nchi itakayoishambulia zenj kwa vifaru inahitaji kwanza logistic ya ukweli,landingship na amphibious attack ship ili kupeleka zana na wanajeshi pwani ya zanzibar..zenj hakuna madini,nani aingie gharama yote and fop what?.

Ila ni sawa gharama zitakuwepo kwani watakua hawategemei tena chochote toka mainland.lakini kama watakua taifahuru lenye kiti UN na kuwa na balozi za nje watapata support.
Hatima ya muungano utavunjika tu,ni bora Tanganyika na zanzibar ziwe na mahusiano kama ya marekani na israel yaani special relationship.

Mkuu Si Tanganyika Wala Znz Itakuwa Na Kiti UN Bali Ni Jamuhuli Ya Muungano Wa Tz.
 
Hivi africa imeshaungana vile eh? nani vile rais wa afrika hivi sasa?wimbo wetu wa taifa huru la africa lyrics zake zipi vile? mhh bendera ya africa ina rangi ngapi vile? alaa na sasa tuna tumia sarafu ya africa kumbe? basi mie haya yoye siyajui kama afica imeshaungana ?nikumbusheni na mji mkuu wa africa jamani!

EAC acha uchovu.,
 
Hayo ni maoni ya watu na tume imeyaunganisha. Isije ikawa wewe ndiye uliyependekeza hivyo na huku kwenye mitandao unajifanya hili ni jambo jipya kwako. Tume haina makosa, imesema kilichosemwa na watu ikiwa ni pamoja na wewe wakati wa kutoa maoni.

ahaaa fine, sasa kama ni maoni na tume ilizingatia maoni basi kura za wazanzibari 66% ilitaka muungano wa mkataba, mbona tume haikuleta?? usibwabwaje usichokijuwa fuatilia mambo kwanza ndio uje hapa.,
 
Ndugu Rais Shein, jana ameuthibitishia Umma wa Watanzania kuwa pande zote mbili za muungano zimeshiriki vema katika mchakato wa rasimu ya kwanza na ya pili ya katiba mpya. kimsingi, tupo kwenye demokrasia ya uwakilishi, ikimaanisha watanzania ml. 45 hatuwezi kwenda kwenye bunge la katiba, kwa mujibu wa sensa ya 2012, Tanzania Bara ina makisio ya watu milioni 43,625,354 (japo wapo wengi ambao hawakuhesabiwa) na Tanzania Visiwani (Zanzibar) watu Milioni 1,303,569 (wapo pia ambao hawakuhesabiwa). sioni tatizo la uwiano hapo, kwanza hawaendi kushindana bali kujenga hoja! ebu tafuta uwiano kati ya wabunge 50 ya total population ya Watanzania bara ujue kila mbunge mmoja anawakilisha wananchi wangapi Vs uwiano wa wabunge 20 kwa total population ya Tanzania Visiwani (Zanzibar). utangundua kuwa hakuna uonevu wowote, kikubwa taasisi husika za uteuzi zituchagulie wabunge watenda kazi, wawajibikaji watakao litendea Taifa hili haki na vizazi vilivyopo na vijavyo.
 
Mfano si Tanzania, huku kwetu tunachemsha,nataka mfano toka kwenye mataifa mengine yenye miungano,wapi umewahi kuona equal ratyio representation? Manaake usiwe mwepesi kukosoa wakati wewe ndio huelewi!

Kiufupi, hamna kitu kama hicho,population ndio inadetermine ratio ya uwakirishi, hata hivyo huku kwetu kmekuwa na upendeleo kwa Wazanzibar! Lakini wao hawalijui hilo! Nadhani na wewe ni mmojawao!

Ndio maana nimetoa mfano wa US,UK na kwingine kwingi,Wawakirishi huwa wanawakirisha watu,si Land!

Kama issue ni gharama, tufanye 20:20 kwa gharama hiyo hiyo kwa upande wa Tanganyika na ZNZ!
 
ahaaa fine, sasa kama ni maoni na tume ilizingatia maoni basi kura za wazanzibari 66% ilitaka muungano wa mkataba, mbona tume haikuleta?? usibwabwaje usichokijuwa fuatilia mambo kwanza ndio uje hapa.,

Kubwabwaja ndio nini? Ulianza kujenga hoja vizuri kisha ukaingiza vitu vivyoeleweka! Inaelekea kulalamika na matusi ndivyo vinavyokuondolea stress! Endelea. Sina muda wa kubadilishana mawazo na mtu wa aina ya wewe.
 
Back
Top Bottom