Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Tulichofundishwa shuleni kuhusu Muungano, ni tofauti na ninayoyasikia Sasa!

Inasemekana, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haikuwa takwa la wananchi, bali la Karume na Nyerere, lakini zaidi, Nyerere.

Inasemekana, hata yale yanayoitwa Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar, yalikuwa ni mauaji katili, na yaliratibiwa na kusaidiwa, kwa sehemu kubwa, na Tanganyika. Hata silaha zilizotumika kwenye mapinduzi zilitoka Tanganyika.

Inasemekana, mapinduzi hayakulenga kumwondoa Mwarabu, bali Serikali halali kwa lengo la kukiweka madarakani Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na Tanganyika.

Inasemekana, tokea mfumo wa Vyama vingi uanze, chama kinachoungwa mkono na Tanganyika kimekuwa kikishinda uchaguzi bila ridhaa ya wapiga kura. Kwamba kishinde kisishinde, lazima kiingie madarakani, maadam tu kinaungwa mkono na Tanganyika.

Inasemekana, hata huu Muungano uliopo kwa sasa si Muungano bali ni Ukoloni. Kwamba Tanganyika inaitawala nchi nyingine kimabavu.

Inawezekana, kama Zanzibar ingekuwa na uwezo, ingeshajitoa kwenye Muungano. Kuenedelea kwake kuwepo kwenye Muungano ni kwa sababu tu inalazimishwa na Tanganyika.

Yameshasemwa mengi na kuandikwa mengi.

Uungwana ni vitendo. Ikiwa hayo yote yanayosemwa ni kweli, basi Zanzibar wana haki ya kuulakamikia Muungano.

Kama ni kweli, nini kifanyike?

Mosi, Tanganyika iiombe radhi Zanzibar kwa yote inayoamini imeitendea Zanzibar ndivyo isivyo, na kwa yale ambayo Zanzibar inailalamikia.

Pili, kura ya maoni iitishwe kwa wananchi wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar kuamua juu ya mustakabali wa Muungano.

Tatu, maamuzi ya wananchi yaheshimiwe.
 
Umwambie Samia na Mbarawa na mawaziri wa Zanzibar waliopo serikali ya muungano kwamba muungano uvunjwe sasa hawatakubali ila baada ya wao kustaafu tena shingo upande manake wana mali nyingi bara.
 
Tulichofundishwa shuleni kuhusu Muungano, ni tofauti na ninayoyasikia Sasa!

Inasemekana, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haikuwa takwa la wananchi, bali la Karume na Nyerere, lakini zaidi, Nyerere.
Sii kweli!, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Manowari za Uingereza zilitia nanga Mombasa tayari kuivamia Zanzibar, kuikomboa. Karume akaja kwa Nyerere kuomba ulinzi, ndipo, Nyerere akamshauri Karume tuungane kuwa nchi moja, Karume akajibu hata leo, wewe Rais mimi Makamo.
Inasemekana, hata yale yanayoitwa Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar, yalikuwa ni mauaji katili, na yaliratibiwa na kusaidiwa, kwa sehemu kubwa, na Tanganyika. Hata silaha zilizotumika kwenye mapinduzi zilitoka Tanganyika.
Sii kweli, huo ni uongo wa wapinga Mapinduzi Matukufu, ukweli ni huu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Inasemekana, mapinduzi hayakulenga kumwondoa Mwarabu, bali Serikali halali kwa lengo la kukiweka madarakani Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na Tanganyika.
Sii kweli
Inasemekana, tokea mfumo wa Vyama vingi uanze, chama kinachoungwa mkono na Tanganyika kimekuwa kikishinda uchaguzi bila ridhaa ya wapiga kura. Kwamba kishinde kisishinde, lazima kiingie madarakani, maadam tu kinaungwa mkono na Tanganyika.
Sii kweli
Inasemekana, hata huu Muungano uliopo kwa sasa si Muungano bali ni Ukoloni. Kwamba Tanganyika inaitawala nchi nyingine kimabavu.
Sii kweli, Zanzibar ilikuwa sehemu ya Tanganyika kabla haijamegeka!. Hivyo ni sehemu yetu kihalali kabisa!.
Inawezekana, kama Zanzibar ingekuwa na uwezo, ingeshajitoa kwenye Muungano. Kuenedelea kwake kuwepo kwenye Muungano ni kwa sababu tu inalazimishwa na Tanganyika.
Sii kweli
Yameshasemwa mengi na kuandikwa mengi.
ni kweli ila mengine ni ya kweli, mengine ni ya uongo!
Uungwana ni vitendo. Ikiwa hayo yote yanayosemwa ni kweli, basi Zanzibar wana haki ya kuulakamikia Muungano.
Si kweli
Kama ni kweli, nini kifanyike?
Na kama ni uongo?.
Mosi, Tanganyika iiombe radhi Zanzibar kwa yote inayoamini imeitendea Zanzibar ndivyo isivyo, na kwa yale ambayo Zanzibar inailalamikia.
Uungwana ni vitendo ni kweli kuna ndivyo sivyo
Pili, kura ya maoni iitishwe kwa wananchi wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar kuamua juu ya mustakabali wa Muungano.
Naunga mkono hoja na hata mimi hili nilishauri Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja
Tatu, maamuzi ya wananchi yaheshimiwe.
Hapa tuko pamoja.
P
 
Tatizo ni kwamba Zanzibar hawataki kujitegemea na wanapenda vya bure kutoka Tanganyika. Bajeti ya Zanzibar inatoka bara la sivyo Zanzibar wangekuwa wameshavunja muungano kitambo.
Mioyo ya Wazanzibar ilishaukataa Muungano siku nyingi. Tuko nao kimwili lakini si kifikra.

Ughaibuni huwa wanajitambulishaje? Mtanzania? Dhubutu!!!

Wanaojiita Watanzania ni Watanganyika. Mzanzibar akiwa ng'ambo hajiiti Mtanzania, bali Mzanzibar!!!
 
Mioyoni ya Wazanzibar ilishaukataa Muungano siku nyingi. Tuko nao kimwili lakini si kifikra.

Ughaibuni huwa wanajitambulishaje? Mtanzania? Dhubutu!!!

Wanaojiita Watanzania ni Watanganyika. Mzanzibar akiwa ng'ambo hajiiti Mtanzania, bali Mzanzibar!!!
Viongozi kutoka Zanzibar hata rais wa Zanzibar ndio wanaojua madhara ya kuvunja muungano, hao wengine wanajisemea tu. Zanzibar haijaweza bado kujitegemea kifedha siku wakiweza muungano utavunjika hapo hapo!
 
Back
Top Bottom