Wabunge 50 Tanganyika 20 Zanzibar inakuwaje mgao huu??

haiwezekani wazenj hawana uwezo huo,hii mambo ya serikali tatu yanakwenda kuua muungano sasa hivi.kumbe ndo maana kambarage alikua amegoma kabisa...ratio ya wabunge wa muungano pia ni issue kubwa.

Kati ya mambo ambayo naomba Mungu asaidie ni huu muungano kuvunjika!
Labda kama umuhimu wake umebaki siri ya viongozi.. Ila kwa mimi mvaa ndala mtaani bado sijaona!
Na kila mmoja arudi kwao.. Tunaung'ang'ania muungano wa nini?
 
Kama nitapiga kura ya hapana kwa rasimu hii basi ni kwa hicho kipengele.

Rasimu inapendekeza shirikisho la nchi mbili huru kwa hiyo ni lazima kuwe na uwiano katika mambo yahusuyo muungano.

Hiyo ratio ya 50:20 imetumia kanuni gani?

Option I: Kwa kuzingatia population ration ya nchi washirika. Kwa mujibu wa Sensa ya 2012 (ambayo pia wa-Tanganyika wengi hawakushiriki kwa sababu mbalimbali) inaonesha ratio ya Tanganyika:Zanzibar ni roughly 43:1 au 98%:2%. Kwa maana hiyo, idadi ya wabunge 70 maana yake, kwa kuzingatia ratio, Tanganyika ina-deserve 98% x 70 = 68.6 (69) na Zanzibar ina-deserve 1.

Option II: Mgao uwe sawa kwa sawa. Kwa maana hiyo kila nchi inatakiwa kuwa na wabunge 35. Sawa, ila kama ndivyo, na gharama za muungano tubebe sawa kwa sawa. Kwa mfano, bajeti ya Wizara ya Ulinzi kwa 2013/14 ni T.Shs. tr. 1.2/=. Kwa maana hiyo, Zanzibar inatakiwa kuchangia T.Shs. bn. 600/= kwa mpango huo wa sawa kwa sawa. Ila nasikia bajeti ya Zanzibar kwa kipindi hicho hicho ni T.Shs. bn. 600/=; sijui inakuwaje hapo! Vivyo hivyo kwenye ajira, kila penye ajira 100; 98 wa-Tanganyika wanobaki wa-Zanzibari.

Polepole kitaeleweka tu na kelele zenu za "tuacheni tupuwe". Kimsingi, Warioba kawapendelea sana ninyi!
 
Hapohapo kwenye ulinzi, rasilimali zinazotumika kuilinda Tanganyika za weza kuwa sawa na zinazo tumika Znz kwa kuangalia idadi ya watu na ukubwa wa eneo husika.

Ndio maana huu muungano hauta dumu kama hamna kura ya maoni na maridhiano. Vinginevyo labda udikteta utumike.
 
Aisee mrelbattawy umegundua eeh! Hata mimi nimeshangaa Zanzibar kupewa idadi kubwa hivyo ya wabunge. Kama haki ingetendeka, ilitakiwa kila mbunge 1 Zanzibar kuwe na wabunge 33 wa Tanganyika. Ikumbukwe kwamba ratio ya population ya Tanganyika to Zanzibar ni 43,625,354 : 1,303,569, kwa hiyo kwa wabunge 50 wa Tanganyika, sana sana wangetoka wabunge 2 wa Zanzibar

Tuliza akili yk sawa., umeambiwa ruwanda na burundi wametowa wawkilishi sawa kwenye muungano wa afrika wbunge 9 kila nchi, haikuangaliwa ukubwa na uwingi wa watu katika nchi husika.,

Nyinyi Tanganyika ndio maana hapo kabla mulikuwa munaona tabu kuitwa Tanganyika kwa kutokujuwa kwenu., sasa Jina la Tanganyika limewavaa badilisheni muite Tanga.,
 
Option I: Kwa kuzingatia population ration ya nchi washirika. Kwa mujibu wa Sensa ya 2012 (ambayo pia wa-Tanganyika wengi hawakushiriki kwa sababu mbalimbali) inaonesha ratio ya Tanganyika:Zanzibar ni roughly 43:1 au 98%:2%. Kwa maana hiyo, idadi ya wabunge 70 maana yake, kwa kuzingatia ratio, Tanganyika ina-deserve 98% x 70 = 68.6 (69) na Zanzibar ina-deserve 1.

Option II: Mgao uwe sawa kwa sawa. Kwa maana hiyo kila nchi inatakiwa kuwa na wabunge 35. Sawa, ila kama ndivyo, na gharama za muungano tubebe sawa kwa sawa. Kwa mfano, bajeti ya Wizara ya Ulinzi kwa 2013/14 ni T.Shs. tr. 1.2/=. Kwa maana hiyo, Zanzibar inatakiwa kuchangia T.Shs. bn. 600/= kwa mpango huo wa sawa kwa sawa. Ila nasikia bajeti ya Zanzibar kwa kipindi hicho hicho ni T.Shs. bn. 600/=; sijui inakuwaje hapo! Vivyo hivyo kwenye ajira, kila penye ajira 100; 98 wa-Tanganyika wanobaki wa-Zanzibari.

Polepole kitaeleweka tu na kelele zenu za "tuacheni tupuwe". Kimsingi, Warioba kawapendelea sana ninyi!

Naomba tuje kwenye option yako ya pili maana ya kwanza haina mashiko: Option ya kwanza ya kugawa wabunge wa muungano kwa kuangalia idadi ya watu haina mashiko kwa vile katika hilo bunge kitakochokuwa kinajadiliwa ndani yake ni maswala ya muungano ambayo yanahusu nchi mbili.

Option ya pili ya ku share cost za muungano sawa kwa sawa na yenyewe pia ina mapungufu. Unajua kwa nini?

Mambo mengi yaliyo kwenye idara za muungano ni quantity based!

mfano; issue za ulinzi, Tanganyika ina eneo kubwa linalohitaji askari wengi na vifaa vingi vya kuilinda ukilinganisha na ZNZ.

Kwa mantiki hiyo, ukisema budget ya ulinzi igaiwe sawa kwa sawa, hapo utakuwa unainyonya ZNZ.

Decision making ni qualitative na sio quantitative based.

kwa hiyo chombo cha kutoa maamuzi kiwe na uwakilishi unaofanana ili maamuzi yasiwe ya upande mmoja.

Natoa hoja.
 
Kama nitapiga kura ya hapana kwa rasimu hii basi ni kwa hicho kipengele.

Rasimu inapendekeza shirikisho la nchi mbili huru kwa hiyo ni lazima kuwe na uwiano katika mambo yahusuyo muungano.

Hiyo ratio ya 50:20 imetumia kanuni gani?

Nilikuwepo mjadala mmoja mkali kuhusu mjadala wa bajeti za kuendesha shughuli za muungano. moja likawa kama wajumbe ni nusu kwa nusu kila upande ugharimie bajeti yao ikaonekana kwa Zanzibar itakuwa ni mauaji kwenye bajeti yao wazanzibari wakagoma.Na bara wakasema na sisi hatutakubali kubeba zigo.Ndipo wazanzibari wakapendekeza itumike idadi ya watu mbunge anawakilisha na kila upande uchangie ratio ya hao wabunge watakaoingia kufuatana na idadi (population) anaowakilisha.Ndio nadhani ikapatikana hiyo Ratio na wazanzibari wakakubali na bara wakakubali.
 
Naomba tuje kwenye option yako ya pili maana ya kwanza haina mashiko: Option ya kwanza ya kugawa wabunge wa muungano kwa kuangalia idadi ya watu haina mashiko kwa vile katika hilo bunge kitakochokuwa kinajadiliwa ndani yake ni maswala ya muungano ambayo yanahusu nchi mbili.

Option ya pili ya ku share cost za muungano sawa kwa sawa na yenyewe pia ina mapungufu. Unajua kwa nini?

Mambo mengi yaliyo kwenye idara za muungano ni quantity based!

mfano; issue za ulinzi, Tanganyika ina eneo kubwa linalohitaji askari wengi na vifaa vingi vya kuilinda ukilinganisha na ZNZ.

Kwa mantiki hiyo, ukisema budget ya ulinzi igaiwe sawa kwa sawa, hapo utakuwa unainyonya ZNZ.

Decision making ni qualitative na sio quantitative based.

kwa hiyo chombo cha kutoa maamuzi kiwe na uwakilishi unaofanana ili maamuzi yasiwe ya upande mmoja.

Natoa hoja.

Mkuu acha kurukaruka. Tanganyika ina watu wengi zaidi wanaohitaji gharama kubwa zaidi kiulinzi kuliko Zanzibar. Hapa ndipo ile Option I uliyodai haina mashiko inavyoonesha jinsi ilivyo na mashiko.
 
Hakuna usawa katika hili, kwa sababu kwenye mambo ya muungano hayohayo kuna ambayo yata kuwa yaki wa favour zaidi ama watanganyika, ama waznz. Sasa kura ni 50-50, ili jambo lipite linahita tuseme 66%. Huoni tayari kutakuwa na mkanganyiko kila mmoja atakapo amua kuwa na msimamo wa kutokubali kumezwa.

Wengi wetu hapa tuna jifanya kutojua kuwa misimamo ya Znz ya kutokumwezwa ndio imewaamsha watanganyika wengi waliokuwa wamelala, na sasa imezaa haya yote tuyaonayo.
 
Tuliza akili yk sawa., umeambiwa ruwanda na burundi wametowa wawkilishi sawa kwenye muungano wa afrika wbunge 9 kila nchi, haikuangaliwa ukubwa na uwingi wa watu katika nchi husika.,

Nyinyi Tanganyika ndio maana hapo kabla mulikuwa munaona tabu kuitwa Tanganyika kwa kutokujuwa kwenu., sasa Jina la Tanganyika limewavaa badilisheni muite Tanga.,
Kwenye muungano wa afrika kuna uwakilishi wa makundi kuna nchi zina uwakilishi mkubwa na michango yao ni mikubwa nchi hizo ni south africa, algeria, misri, libya, nchi nyingine ziko katika kundi la mchango mdogo na uwakilishi mdogo
 
Mkuu acha kurukaruka. Tanganyika ina watu wengi zaidi wanaohitaji gharama kubwa zaidi kiulinzi kuliko Zanzibar. Hapa ndipo ile Option I uliyodai haina mashiko inavyoonesha jinsi ilivyo na mashiko.

Umeshaniona naruka ruka tena! Read between the lines.

Hiyo ratio haikubaliki. Bunge ni chombo chenye maamuzi. Ratio hiyo inaipa uwezo wa Tanganyika kuweza kupitisha sheria yoyote inayohusu muungano bila Zanzibar kuwa na sauti ya kupinga. 50:20 ni sawa na 71p kwa 29p.

Ni ujuha kukubali uwiano wa namna hiyo.
Uamuzi wowote ambao Tanganyika watataka kuupitisha, utapita hata kama hao wawakilishi wote wa ZNZ wakiukataa hata kama utatumia kigezo cha simple majority.
 
Kwa sababu tu za kutaka madaraka, Zanziba hawatakubali hata huo upendeleo wa Warioba. Mh. Warioba aliufurahia upole wa Watanganyika. Tumezoea Hewala Bwana mkubwa. Hii ndiyo imepelekea Warioba kuja na formula yake ya ratio hii ya 50:20. Mna wabembeleza nini hawa watu?
Hata mngewaambia iwe 20 Tanganyika na 50 Zenj bado wangesema mnawaonea. Nasema hakuna muungano bila kuwauliza wananchi kama wanauhitaji huo muungano. Anzia Zanzibar mje bara.
 
Umeshaniona naruka ruka tena! Read between the lines.

Hiyo ratio haikubaliki. Bunge ni chombo chenye maamuzi. Ratio hiyo inaipa uwezo wa Tanganyika kuweza kupitisha sheria yoyote inayohusu muungano bila Zanzibar kuwa na sauti ya kupinga. 50:20 ni sawa na 71p kwa 29p.

Ni ujuha kukubali uwiano wa namna hiyo.
Uamuzi wowote ambao Tanganyika watataka kuupitisha, utapita hata kama hao wawakilishi wote wa ZNZ wakiukataa hata kama utatumia kigezo cha simple majority.

Mbunge hawakilishi ramani anawakilisha watu.Ni watu wanaoungana siyo ramani.Hivyo ukiwa na watu laki moja NCHI NZIMA zanzibar wakawa na watu elfu ishirini,Kama kila mbunge anawakilisha watu elfu ishirini ina maana Zanzibar watakuwa na mbunge mmoja bara wabunge wanne.Usawa katika muungano ni usawa wa uwakilishi wa watu si uwakilishi wa ramani au kipande cha ardhi kuwa we unatoka Zanzibar yule anatoka bara.Muungano ni wa watu sio ramani.Suala la kuwa wabunge wengi wakipitisha inakuweje ni kuwa ktk muungano umimi unakufa sheria ya wengi wape ndio inafanya kazi na ndio demokrasia.Kelele za mimi mzanzibar au mbara zinabaki kule kwenye nchi zenu maana katika serikali kuna serikali tatu ile ya muungano ukiingia u-nchi wako unaacha getini kule ni mambo ya muungano kwenda mbele.
 
Fumbua macho mkuu, hyo inawezekana vip? Tanganyika iwe sawa na zanzbr hata hvyo z azbr imepewa weng ukilingalisha na uwakilish wake ilitakiwa mpate wabunge 5! Tatizo lako unateswa na udini!

Udini ukujaje hapa! Hatujaona kiashiria cha udini ktk bandiko lake, wewe ndio umeanza kuibadili hii mada. Usitupeleke huko.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Unataka wawe Sawa na udogo wa nchi kule wengine wawe wabunge wa mtaa au...
 
Nimejaribu kupitia Rasimu nimeona hili la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano watakuwa 70, Tanganyika itatoa 50 na Zanzibar 20 ukiacha wale wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha watu wenye ulemavu na wengine mmoja mmoja kuwakilisha m'me na m'ke katika majimbo ya uchaguzi.,

Ivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2., inakuwaje nchi moja 50 nyengine 20??

Mbona hawa Tanganyika wanataka kuendelea kutuburuza tena kwene bunge? Ivi burundi nchi ndogo lakini inawakilisha wabunge sawa na nchi kubwa kwenye muungano wa afrika., inakuwaje Muungano huu wa Tanzania?

Nimeskia Kenya na Unganda wamevutiwa na Muungano huu uliotoka kwenye rasimu wa Tanzania wanataka kujiunga lakin sasa itakuwaje kwa mgao huu wa wabunge??

Hayo ni maoni ya watu na tume imeyaunganisha. Isije ikawa wewe ndiye uliyependekeza hivyo na huku kwenye mitandao unajifanya hili ni jambo jipya kwako. Tume haina makosa, imesema kilichosemwa na watu ikiwa ni pamoja na wewe wakati wa kutoa maoni.
 
Yani kama ni uwiano wa uwakilishi ilibidi Bunge la Muungano liwe na uwiano wa 68:2. Kwa sababu....Watanganyika ni 44M na Wazanzibari ni 1.3M ambao mathematically...ni ratio ya 68:2. Hiyo 50:20 wamependelewa saaaaaaaaana, washukuru.
 
Hapohapo kwenye ulinzi, rasilimali zinazotumika kuilinda Tanganyika za weza kuwa sawa na zinazo tumika Znz kwa kuangalia idadi ya watu na ukubwa wa eneo husika.

Ndio maana huu muungano hauta dumu kama hamna kura ya maoni na maridhiano. Vinginevyo labda udikteta utumike.
mfano katika hiyo bajeti ya ulinzi wachange sawa bilion 600 kila upande,halafu kwa Tanganyika zitumike bilioni 900 na kisha zenj bilion 300.sidhani kuwa itakua sawa na hiyo ni wizara moja tu kati ya 7 zinapendekezwa kuwa za muungano.gharama inakuwa juu,ukichukulia bajeti ya zanzibar ilivo ndogo,watadai kujitoa.sasa sijui unawalazimisha vipi kuchangia kwanza hawana,pili hawataki.
 
Yani kama ni uwiano wa uwakilishi ilibidi Bunge la Muungano liwe na uwiano wa 68:2. Kwa sababu....Watanganyika ni 44M na Wazanzibari ni 1.3M ambao mathematically...ni ratio ya 68:2. Hiyo 50:20 wamependelewa saaaaaaaaana, washukuru.
hiyo ratio ya 20:50 iko fair lakini Tanganyika wanaweza kuona inawalalia kwa kigezo cha wingi na ukubwa wa eneo.
 
mfano katika hiyo bajeti ya ulinzi wachange sawa bilion 600 kila upande,halafu kwa Tanganyika zitumike bilioni 900 na kisha zenj bilion 300.sidhani kuwa itakua sawa na hiyo ni wizara moja tu kati ya 7 zinapendekezwa kuwa za muungano.gharama inakuwa juu,ukichukulia bajeti ya zanzibar ilivo ndogo,watadai kujitoa.sasa sijui unawalazimisha vipi kuchangia kwanza hawana,pili hawataki.

Na hapo ndipo ilipo "siri" kwamba japo wengi wametaka Serikali 3, lakini hazitadumu; tena CCM wanajenga sana hoja kwenye hili. Tatizo ninaloliona hapa, ilitakiwa wananchi waulizwe kwanza kama wanautaka au hawautaki Muungano tena waulizwe kwanza wazanzibari. Baada ya hapo mengine yangefuata.
 
Back
Top Bottom