Wabunge 50 Tanganyika 20 Zanzibar inakuwaje mgao huu??

Kubwabwaja ndio nini? Ulianza kujenga hoja vizuri kisha ukaingiza vitu vivyoeleweka! Inaelekea kulalamika na matusi ndivyo vinavyokuondolea stress! Endelea. Sina muda wa kubadilishana mawazo na mtu wa aina ya wewe.

ukikosa hoja unakaa kimya kama ulivyoamua., kubwabwaja ni kuongea porojo projo mambo uisiyoyajuwa.,
 
Nimejaribu kupitia Rasimu nimeona hili la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano watakuwa 70, Tanganyika itatoa 50 na Zanzibar 20 ukiacha wale wa kuteuliwa na Rais kuwakilisha watu wenye ulemavu na wengine mmoja mmoja kuwakilisha m'me na m'ke katika majimbo ya uchaguzi.,

Ivi warioba na tume yake hapa kweli walitenda haki? mana ukiisoma Rasimu inazungumza wazi wazi ni shirikisho la nchi 2., inakuwaje nchi moja 50 nyengine 20??

Mbona hawa Tanganyika wanataka kuendelea kutuburuza tena kwene bunge? Ivi burundi nchi ndogo lakini inawakilisha wabunge sawa na nchi kubwa kwenye muungano wa afrika., inakuwaje Muungano huu wa Tanzania?

Nimeskia Kenya na Unganda wamevutiwa na Muungano huu uliotoka kwenye rasimu wa Tanzania wanataka kujiunga lakin sasa itakuwaje kwa mgao huu wa wabunge??
Jibu ni rahisi ulinzi na usalama ikiwemo Polisi znz haina uwezo wa kuchangia kabisa achili hiyo unyosema 50/20, unaelewa hapo. Kasema Vuai kasema mwenyekiti wa kamati ya blw

Acheni utamaduni wa kugawana vyeo,kumbatieni utamaduni wa kuwajibika. Unataka wabunge huwezi kuwalipia. Ala!
Wale wanaokuja Dodoma SMZ haiwezi kuwalipa unataka miaka mingine ya mteremko, no way!

Wznz acheni kufikiria vyeo tu, lazima mfikirie na gharama zinazotokana na hivyo vyeo.
Hao unaosema 20 SMZ haitawalipa kama ilivyogoma umeme bado unataka usawa.

Tanganyika imerudi, shangilieni sana wznz.
 
Tumechoka na nyie kwanza kazi kutafuta vyeo kwenye muungano. Mkitaka bakini na nchi yenu muweke watu wote wabunge. Wabunge 20 kwa watu milioni moja na wabunge 50 kwa watu milioni 45 huna akili ya kuona kama wazanzibari ni wengi sana? Kila siku kulinganisha EAC na tanzania, kwani EAC ni jamhuri au nchi moja. Kazi kuzungusha maneno.
 
Miye hapana yangu itapatikana kwa kutokuwekwa mahakama ya Qadhi kwenye katiba.

Nani anataka mahakama za kukata watu vichwa na kupiga mawe wanawake hadi kufa kwa hukumu za unyanyasaji wa kijinsia usio kifani. Hatutaki hata kusikia
 
Tumechoka na nyie kwanza kazi kutafuta vyeo kwenye muungano. Mkitaka bakini na nchi yenu muweke watu wote wabunge. Wabunge 20 kwa watu milioni moja na wabunge 50 kwa watu milioni 45 huna akili ya kuona kama wazanzibari ni wengi sana? Kila siku kulinganisha EAC na tanzania, kwani EAC ni jamhuri au nchi moja. Kazi kuzungusha maneno.

EAC ni shirikisho la nchi tofauti kuna tofauti gani na shirikisho hili Tanganyk na Zanzbr ambalo pia ni nchi 2 tofauti., lakin kwann tanganyika mnapenda kuipangia Zanzibar? huwo mda umekwisha muungano huu ndo tunauvunja tena
 
Jibu ni rahisi ulinzi na usalama ikiwemo Polisi znz haina uwezo wa kuchangia kabisa achili hiyo unyosema 50/20, unaelewa hapo. Kasema Vuai kasema mwenyekiti wa kamati ya blw

Acheni utamaduni wa kugawana vyeo,kumbatieni utamaduni wa kuwajibika. Unataka wabunge huwezi kuwalipia. Ala!
Wale wanaokuja Dodoma SMZ haiwezi kuwalipa unataka miaka mingine ya mteremko, no way!

Wznz acheni kufikiria vyeo tu, lazima mfikirie na gharama zinazotokana na hivyo vyeo.
Hao unaosema 20 SMZ haitawalipa kama ilivyogoma umeme bado unataka usawa.

Tanganyika imerudi, shangilieni sana wznz.

Kwanini wewe ni mtanganyika?
 
Nani anataka mahakama za kukata watu vichwa na kupiga mawe wanawake hadi kufa kwa hukumu za unyanyasaji wa kijinsia usio kifani. Hatutaki hata kusikia

Lakini mafisadi kututia ufukara kwako poa.
 
EAC ni shirikisho la nchi tofauti kuna tofauti gani na shirikisho hili Tanganyk na Zanzbr ambalo pia ni nchi 2 tofauti., lakin kwann tanganyika mnapenda kuipangia Zanzibar? huwo mda umekwisha muungano huu ndo tunauvunja tena

Ttzo watanganyika wengi wana mawazo ya kikoloni.
 
mi nafikiri kila kitu kiwe sawa kama wabunge wawe 50 ratio na uchangiaji pia uwe hivyo hivyo haya mambo ndio tulionya toka mwanzo hatuwezi kuwa na muungano wa nchi tatu ni bora tuwe na nchi moja au tuvunje muungano tatizo warioba na tume yake walijiona ni mawazo yao ni bora zaidi
 
Wabunge ni nusu kwa nusu ,sasa mkiwa wakubwa kama tembo na wengine kuwa wadogo kaka susumizhi ,tunaungana kama nchi mbili ,mnataka Muungano ndio hivyo hamuutaki tokomeeni mbele , nyie subilini zije hizo tatu ,haitavuka miaka wala muda kila mmoja kivyake hakuna mbili wala tatu. Tunawavuta tu ,tumewageuza njiwa mgeni!!
 
ukikosa hoja unakaa kimya kama ulivyoamua., kubwabwaja ni kuongea porojo projo mambo uisiyoyajuwa.,

Kujua kusikokusaidia si sawa tu na kutokujua? Utajitofautishaje na anayebwabwaja? JF itafungwa maana tuko wengi.
 
Ni kweli kabisa kaka ila hili la Mali za tanu na ccm ya chini ya miaka ya 1993 zirudishwe kwa watanzania kisha tuanze upyaaaa
 
Back
Top Bottom