Wabongo na ushamba wa kushangaa wazungu

mwanahabari93

JF-Expert Member
May 20, 2015
263
169
Watanzania tuna matatizo gan nilikuwa najua ushamba umeshatuisha tangu kipindi icho huwezi amini hadi leo wabongo tena vijana na watuwazima bado wanaendelea kushangaa wazungu.........Tatizo ni nini....au kipi tunachokishangaa......kwa wale wazungu.....Watanzania tuwe washamba na tushangae vitu vinavyofaa kushangaa.....Kushangaa wazungu ni kitu kinachonikera na kuniumiza moyo na kunipa mawazo..........wewe unasemaje mwana jamii forums
 
Mpaka zama hizi kwelii? Arusha nilikuta wazungu hadi waliopangisha single room uswahilini na wanashinda kwenye vijiwe vya shoe shine...
 
Mkuu wewe umeona kushangaa. Hata mimi nakubaliana na wewe lakini nikuambie kuna kubwa zaidi: Kuabudu na kutukuza wazungu. Wabongo wanatukuza wazungu kiasi kwamba mtu yuko tayari kumgharamia mzungu wa fedha ili aonekane yuko nae kama rafiki. Kuna kipindi nilikuwa Temeke akaja mzungu mmoja mwanaume akawa anajichanganya kwenye vijiwe na kulala guest house za uswahilini ili ajifunze kiswahili kwa urahisi. Nakuambia watu walikuwa wanamgombea kama mpira wa kona ili tu awe karibu nao. Mfano mwingine. Niliwahi kuishi Ulaya kwa muda mrefu kabla sijaoa. Niliporudi Bongo nikaoa mdada mtanzania. Unajua watu walikuwa wanasemaje? Huyu mjinga kweli. Na kukaa Ulaya kote hakuoa mzungu halafu anarudi kuoa mweusi?
 
Na dada zetu wanAwashobokea wakijua wazungu mambo safi kumbe wengine ni homeless wkt huku tz hamna homeless km huko amerika ulaya
 
Na kwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele ndo hata majina yetu ya asili yanavyozidi kupotea!

Unakutana na mdada anaitwa Paige Michael au Brooke William!

Kama hujaonana naye unaweza kudhani labda huyo mtu si Mtanzania.

Unaweza kudhani ni mgeni labda.

Kumbe wapi. Ni Mtanzania.
 
Inategemea huyo mzungu kafanya nini ,watu wanakulana mate kwenye Bus ,upo na maza na mshua utaacha kushangaa ??
 
Babu yangu aliwahi kuniambia enzi zao walikimbilia gari ya mzungu mbeleni mzungu akakatisha kichakani kushusha vitu alivotoka wakazunguka upande wa pili wakaenda kushangaa vitu vya mzungu
 
huwezi amini arusha hi tabia hamna kabisa.kila mzawa wa arusha ni mjanja.

huwezi mfananisha chali wa chuga na sharobaro wa dar au mfuga ng'ombe wa mwanza kwani lazima watamshangaa mzungu tu.washamba bobezi
 
kweli Arusha hii tabia sijaiona nimeishi pale kwa mda kidogo ila sijaona mambo kama hayo
 
kweli
Mpaka zama hizi kwelii? Arusha nilikuta wazungu hadi waliopangisha single room uswahilini na wanashinda kwenye vijiwe vya shoe shine...
kweli Arusha tabia hizi hakuna pale tofauti na mikoa mingine
 
huwezi amini arusha hi tabia hamna kabisa.kila mzawa wa arusha ni mjanja.

huwezi mfananisha chali wa chuga na sharobaro wa dar au mfuga ng'ombe wa mwanza kwani lazima watamshangaa mzungu tu.washamba bobezi
Duh vijana wa Arusha mnafurahisha sana.
 
Na dada zetu wanAwashobokea wakijua wazungu mambo safi kumbe wengine ni homeless wkt huku tz hamna homeless km huko amerika ulaya
Kwel wadada wakitanzania wengi ni washamba nakumbuka nilikuwa nasoma chuo flan hapa Tz nilikuwa nikishuhuda wadada walivyo washamba kwa wageni...ambao sio wa tz
 
Na dada zetu wanAwashobokea wakijua wazungu mambo safi kumbe wengine ni homeless wkt huku tz hamna homeless km huko amerika ulaya
Wewe unaishi tanzania ipi? Watu kibao wanalala nje na kushindia mlo mmoja kama sio njaa kabisa nchi hii.
 
Bora sisi tunavyowashangaa kuliko wao wanavyotushangaa tukiwa nchini kwao.

Wanatushangaa mpaka wanaturushia ndizi barabarani.
 
Na dada zetu wanAwashobokea wakijua wazungu mambo safi kumbe wengine ni homeless wkt huku tz hamna homeless km huko amerika ulaya
Mbona hapa kwetu homeless Ni wengi sana, watu tunaishi kwenye chumba kimoja Na kila kitu hapo hapo Kama tuko STORE! Kuna tofauti gani na hao homeless wa ulaya?
 
Back
Top Bottom