Wabongo dili hilooo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabongo dili hilooo...

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by malisak, Jul 27, 2010.

 1. malisak

  malisak JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 16, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Wananchi wa maeneo mbalimbali ya jiji wameonekana kufurahia ujio wa kiwanda cha Wachina kilichoamua kununua soli za viatu ambavyo vimetumika.

  Shuhuda wetu alishuhudia idadi kubwa ya vijana na wazee wakiwa wamejitokeza kwa wingi kiwandani hapo Keko Mwanga tayari kwa ajili ya kupima na kuuza soli za viatu ambazo zimechakaa katika kiwanda hicho.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana hao walisema kuwa, wanauza kilogramu moja ya soli hizo za viatu kwa sh. 400 hivyo wanaona ni bei nzuri na wamekuwa wakijipatia fedha nyingi kuliko hata vibarua wa viwandani.

  Walisema kuwa kwa siku mtu anaweza kupata sh. 30,000 huku wachapakazi wakijinyakulia sh.50,000 hali ambayo inaonyesha kuboresha maisha ya watu wengi.

  Baadhi ya wananchi wamesema huenda soli hizo wanunuzi wake hutumia kutengenezea viatu aina ya Yeboyebo wanavyovizalisha.

  Biashara ya ununuzi wa soli hizo umezaa matunda kwa kuondokana na kero ya utupaji uchafu uliokithiri ndani ya solo la Mchikichini ambapo hiivi sasa huwezi ukakuta kiatu kichakavu au soli vikiwa vimezagaa.

  Baadhi ya vijana walisema kuwa awali wao walikuwa na vibarua katika viwanda vya jirani na hapo lakini walipo ona kuwa dili hilo linalipa ikawalazimu kusimama kazi katika viwanda hivyo kwa ajili ya kujiongezea kipato mpaka hapo watakapo sitisha zoezi hilo hapo baadae.



  KWA HISANI YA DARHOTWIRE.COM
   
 2. R

  Renegade JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,761
  Likes Received: 1,062
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa vizuri , angalau inapunguza utupaji taka ovyo, Good news.
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndo mwanzo wa kuibiwa viatu ile desturi yetu watanzania ya kuvua viatu kuviacha mlangoni unapoingia ndani kwako au kwa rafiki yako itabidi isitishwe maana viabaka hawatachelewa kuvipitia.............:smile-big:
   
 4. K

  Kinte Member

  #4
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  ..itachekesha ikiwa watachukua kiatu chako kwa ajili ya soli, kwa kuwa watahitaji viatu kadhaa kabla hawajapata 1kg na kujipatia shilingi 400 :smile:
   
 5. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #5
  Jul 27, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mbavu zangu.

  mi nafikiri kiatu ni ghali kuliko soli.

  Hata kama kimechakaa akikiosha akapita nacho tandale akatangaza dau la 500, anauza fasta...
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Watanzania bado tuna kazi ndefu!
  Mtu anabandika Tangazo kwenye business forum kuhusu biashara ya sole chakavu kwa wachina!! Kuna biashara nyingi za uzalishaji zinalipa sana tu, vijana acheni uzembe wa mjini, njooni shambani jamani tulime na kufuga, pesa zipo shamba jamani, kuajiriwa ni kumzalishia mtu!
   
 7. M

  Malila JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Akarudi baba mmoja,toka safari ya mbali,
  Kavimba yote mapaja,na kutetemeka mwili,
  Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
  Wakataka na kauli,iwafae maishani.

  Mgonjwa aliwaambia kama mnataka mali mtayapata shambani. Hao madogo wakishamaliza kuokota soli za viatu zote nini kitafuata. Kwa sababu soli hazitupwi kila siku jamani.
   
 8. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  Kaka hujui kuwa sisi wabongo ni mabingwa wa kupenda "shortcuts"? kilimo matunda yake mpaka msimu upite au ng'ombe mpaka akue ndio unaanza kumkamua maziwa wakati soli ya kiatu unaokota na kuuza chapu kwa haraka, hivyo ndivyo tunavyopenda wabongo. Hata hivyo ndugu yangu naunga mkono hoja yako kwa 100%, mimi zamani nilikuwa nafikiri wazungu wametushinda maendeleo kwa bahati tu lakini tangu nije hapa nimegundua wenzetu kumbe wako "serious" sana na kufanya kazi, hata hicho kilimo tunachokikwepa wenzetu wanakithamini vilevile. Sehemu ya umaskini wetu inatokana na UVIVU KATIKA KAZI NARUDIA TENA, UVIVU. Pia tunaendelea tu kuwaangalia wageni wanakuja na kuchukua fursa zetu halafu sisi tunabaki watu wa kuzunguka na kuokota soli chakavu ili tukawauzie hao wageni kwa ajili ya shughuli za kiwanda chao......hii kali mgeni anakua bosi mwenyeji unageuka kibarua....mmmh! na wachina sasa mpaka wataanza kugombea nafasi za uongozi manake wamejaa kila kona!
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Biashara gani nyingi zinazolipa unazome tupe mfano. zinahitaji min capital ya shilingi ngapi? We jiulize wabunge wangapi wana mashamba japo ya mifano majimboni kwao. Sioni kama hii issue ni ya kuzalilisha. Tuache siasa.

  Kuna biashara nyingi zinalipa lakini hii ni ya soli chakavu. hii ni sawa sawa biashara ya vitu vya plastic.
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280

  Wacha uongo sio desturi ya Watanzania wote kuvua viatu na kuviacha mlangoni. Labda useme waislam wanapokwenda kusali ijumaa kwenye misikiti.
   
 11. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sio waislam wanapokwenda kuswali tu, watu wengi wanavua viatu hata kwenye milango ya nyumba zao. Si vyema na kukurupuka na neno WACHA UONGO.
   
 12. a

  afande samwel Senior Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 13, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kasheshe
   
 13. malisak

  malisak JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Mar 16, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  JS watu wanaiba katika nyumba za ibada mpaka ndala papa na nguru husgangai?, na hata vile viatu vilivyooza na kunadiwa mpaka 500 mchikichini vitapanda bei
   
 14. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2010
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukitaka raha ya Jf anzisha mjadala mtamu kama huu
  Mimi mbavu sina
   
 15. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Yap mijadala yenye kulenga manufaa ilikuwa inachangiwa kwa kusitasita lakini sio huu:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
   
 16. W

  Wifra Member

  #16
  Jul 28, 2010
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunaokaa uswhilini, milango inatazama barabaran kazi tunayo!!
   
Loading...