Machafu ya kiwanda cha Mkulazi Holding Campany Limited

Rocky City

JF-Expert Member
Nov 22, 2017
874
662
Hiki ni kiwanda cha sukari cha Mkulazi kilichopo Dakawa ni kiwanda tunacho ambiwa kikubwa Afrika Mashariki na kati. kwa kuzalisha sukari.

Mzee Magufuli alipambania Tanzania ya viwanda na huenda hicho ni moja ya jitiada zake, RIP, lakini kiwanda hiki serikali ya sasa kwa mambo yanavyo kwenda sioni uhai wake kwa mambo yafuatayo.

1. Managements mbovu sana

2. Nimefika pale vibarua wanafanya kazi over dose kibarua akienda pale kesho hawa wa mashambani wanapigwa mzigo mzito sana, hapa sio shida punda afike mzigo ufike.

3. Hili ndio lilolo nishangaza sana, malipo ya vibarua yanalipwa mikononi yani wanapanga foleni ndani ya kiwanda humo wanalipwa sh 6500 asubuhi hadi jioni saa kumi, hakuna chakula wala nini, huu ni unyanyasaji wa hali ya juu sana.

4. Kwanini malipo haya yalipwe mkononi hapa ndio mwanya wa rushwa ulipo, tena kuna wengine walilamika pale kuwa kuna wakati wanalipwa sh 6000 mia tano zao wanaambiwa chenji inasumbua.

, huu ni ukandamizaji mkubwa kwa Watanzania hawa, serikali ifatilie hili jambo.

4. Ofisini watu wanapiga story tu na vicheko muda wote miguu juu huku, ofisi zingine wazi tangu sa 3 hadi sa 6 mtu alikwenda kunywa chai kiwanda hiki pesa ya serikali imepotea tu.
 
Hiyo ni mishahara ya kawaida kabisa kwa wafanyakazi wa viwandani kama vibarua. Kila tukisema mnaonaga kama tunadanganya kwa sabab mnapewa perdiem na Taasisi zenu 170k au 250k kwas siku huko vikaoni

Mm nimewahi kulipa buku 4 kiwandani na nilishinda na njaa. Inapigwa kazi mkuu mpaka unahisi haja ndogo inakuporonyoka. Wakuu wenye uwezo wa kuwasiadia vijana humu wasaidieni. Na hiyo ndo mishahara yenyew ili faida ipatikane hapo kiwandan
 
Hawakuwa na business strategy, ni Bora wakaingia ubia WA 51% by 49%
Management mbov makampuni makubwa karibu yote yako hivyo. Hasa yanatomiliki viwanda, mfumo huru huu. Unapewa ovaroli la mwaka Jana linanuka jasho. Utakataa vipi?

Hapo kuwepo na standard tu, mana hawa vibarua hata vyama vya kutetea haki za wafanyakazi haviwatambui.
 
Means wafanyakazi hawa kwa uwingi wao hawana uwezo wa ku push back pamoja na kuona haki zao zinakandamizwa, uoga na uzuzu wao wanakubali kuwa kwenye mazingira hayo, mchina anayewekeza pale morogoro Tanzania keshajua hawa ni waoga,mchina anayewekeza pale Thembisa anaelewa kuwa one mistake kiwanda kitawaka moto, matokeo yake ana respect na kuwatendea haki wafanyakazi, tuendelee kulalama humu
 
Hiyo ni mishahara ya kawaida kabisa kwa wafanyakazi wa viwandani kama vibarua. Kila tukisema mnaonaga kama tunadanganya kwa sabab mnapewa perdiem na Taasisi zenu 170k au 250k kwas siku huko vikaoni

Mm nimewahi kulipa buku 4 kiwandani na nilishinda na njaa. Inapigwa kazi mkuu mpaka unahisi haja ndogo inakuporonyoka. Wakuu wenye uwezo wa kuwasiadia vijana humu wasaidieni. Na hiyo ndo mishahara yenyew ili faida ipatikane hapo kiwandan
Mkuu kwa bakhressa iyo sio?
 
Dah! Inasikitisha sana.

Vibarua inabidi waandamane kupinga suala hilo, wasipoandamana basi hali hiyo haitoisha.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hiyo ni mishahara ya kawaida kabisa kwa wafanyakazi wa viwandani kama vibarua. Kila tukisema mnaonaga kama tunadanganya kwa sabab mnapewa perdiem na Taasisi zenu 170k au 250k kwas siku huko vikaoni

Mm nimewahi kulipa buku 4 kiwandani na nilishinda na njaa. Inapigwa kazi mkuu mpaka unahisi haja ndogo inakuporonyoka. Wakuu wenye uwezo wa kuwasiadia vijana humu wasaidieni. Na hiyo ndo mishahara yenyew ili faida ipatikane hapo kiwandan
Kwamba wakipewa 12 kiwanda kitafilisika ?
Nimewah kuona kiwanda flan pale buguruni mangiri wanalipwa 3500 mzigo wa massa 10 halafu wados wanakula million nyingi plus kila weekend 250k
 
Back
Top Bottom