engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,441
acha unazi,tumeona ufunguzi asilimia kubwa ya washiriki wamekwenda na suti zao,ama hujaona tukuletee picha?
ingia hapa THE SPORAH SHOW.
Naona vitambi tu hapo sijui hawa ndo wale wanaokwenda na vimada wao au wake za watu badala ya kuwapeleka wananmichezo
Yaani Timu ya Tanzania inavalishwa suti za Mariedo!!!??? Kwa nini wasivalishwe angalau vazi la Kimasai ambalo huwa liko la kike na la kiume wauenzi utamaduni wetu??? Wangevaa kimasai wakaweka na sime na rungu kwa kwenda mbele, mbona timu ya Burundi waliaandamana wameshika fimbo. Wizara ya michezo hakuna ubunifu kabisa. Ebu cheki hapa chini timu ya Fiji kiongozi kavaa sketi ya makuti kuuenzi utamaduni wao, na timu ya Mexico mshiriki kavaa kavaa kofia la galoni tatu somberero kuuenzi utamaduni wao!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!
View attachment 60145
View attachment 60146
Niliitazama parade yao jana usiku na huyo aliyeshika bendera anitwa Zakia Mrisho, mwanariadha. Lakini tazama hapa chini naona wengine wanabandika picha tofauti sijui walipita tena au ni uwanja mwingine.
![]()
Unaweza kukuta ktk hiyo timu viongozi ni wengi kuliko hata wanamichezo!
Mkuu nashukuru kwa kunifahamisha kwamba watalii wetu walifika salama salimini. Kikubwa tusubiri zawadi ya visingizio.
Usikubali kuingizwa mjini kirahisi. Hii ni picha ya olympic ya mwaka 2004 huko Korea kusini au 2008 huko Beijing, angalia vizuri utaona washereshaji ni wasichana wa kichina au wakorea. Hatudanganyiki, wao wa mwaka huu wamevttishwa suti za mariedo kama walivyowasilishwa na mwana JF Mbuzi Mzee.
Wanamichezo wako 6 (wanariadha 4, muogeleaji 1, na ngumi 1), wakati viongozi wako 12; yaani kila mwanamichezo ana viongozi wawili. Majirani zetu Kenya wamepeleka timu ya watu 40 wakiwemo wanariadha 16 na viongozi 10, yaani kila wanamichezo wanne wana kiongozi mmoja. Wanaokwenda wamejituma wameaanza kuvuna medali tangu jana, China ikiongoza na medali 6 zikiwemo za dhahabu 4 na bronze 2. Kama ilivyokuwa kule Korea 2004 na Beijing 2008, watalii wetu wako London wakiuza sura, na nina hakika hawatarudi na medali yoyote ila watakuwa na lundo la mizigo na wakiwa na visingizio kibao, mara hali ya hewa, mara ukungu, chakula, lugha, technohama, michakato, vipaumbele blaah blaah.
i