Wabeba box wengi wamerudi na ndoto...

Wabeba box wengi wamerudi na ndoto...

Hizi mada za wabeba mabox na wala vumbi zishapitwa na wakati.. Ndo maana watu wamechuna, maisha ni popote tu ukitusua bongo pouwa tu na usipotusua ulaya pouwa tu ila tofauti ni kua mmoja anaishi third world na mwingine first world hio ndio tafauti...
Third world na first world??? Hujajua wanavyoishi huko wengi wao ndo maana wasema hivi. In fact, huku ndo first world na kule third world kwao, sio wote ila wengi.
 
Naona huu uzi umewagusa wengi....kumbe wengi wabeba box huku
 
Hivi "Kubeba Box" ndo kufanyaje...? Huu msamiati umenipit kidoogo......!
Ni kitendo cha kuinama unaacha makalio wazi huku nyuma mzungu anakufanya kitu mbaya! Si unajua unapotaka kubeba mzigo mzito lazima uiname? Mwulize Mzee Mwanakijiji, Nyani Ngabu, King'asti (huyu yeye huwa anashuhudia kaka zake wanavyosota), Le Mutuz yeye yalimchosha akaachia kamba!
 
Hivi "Kubeba Box" ndo kufanyaje...? Huu msamiati umenipit kidoogo......!
Vijana wengi wa kiafrika waliokwenda ulaya au marekani kazi rahisi kuzipata ni za kwenye maduka na supermarkets. kazi zenyewe zinakuwa hasahasa ni kubeba maboxi ya bidhaa mbalimbali na kuyapanga au kupanga bidhaa vizuri ndani ya duka. inaweza kuwa kubeba box toka store hadi dukani au kutoka sehem moja hadi nyingine ndani ya supermakert. ndio maana hawa wanaitwa wabeba box.
 
mnawasaidiaje waliopo hapa kutwa kunywa virobs tuanze kuwasema waliopo nje hapa hakuna kazi za ovyo watanzania wenzetu wanasafisha majiji wao katika hali mbaya ya uchafu tuwaseme walio nje au chuki tuu wakuu..
 
Uzi una ukweli mtupu huu.
Wapo wengi sana, wengine visa zilishaisha sasa ni illegal migrants huko huko, wakiwaona polisi wanakimbia na kurudi hawawezi kwa kosa la ku-over stay visa zao. Wapo kwenye limbo state, full stress na maisha ni ghali sana huko.
Kwa kweli wengi wana hali mbaya sana huko, wangejilipua tu warudi au waende ktk balozi huko kwa msaada zaidi.
Sio kweli. Uki over stay ni kosa lakini ukiamua kurudi kwenu unarudi tu bila shida. Kitakachokufanya usirudi kwenu labda ni kukosa nauli ila sio kwa kuogopa kosa la kuishi kinyume na sheria, hata ukiondoka watakachofanya ni kukupiga ban tu muda kadhaa
 
Sio kweli. Uki over stay ni kosa lakini ukiamua kurudi kwenu unarudi tu bila shida. Kitakachokufanya usirudi kwenu labda ni kukosa nauli ila sio kwa kuogopa kosa la kuishi kinyume na sheria, hata ukiondoka watakachofanya ni kukupiga ban tu muda kadhaa

Nilikuomba uniletee simu kwa siri umekuja kunianika sasa
 
Back
Top Bottom