Wabaya wa CHADEMA wavurugana!

Wabaya wa CHADEMA wavurugana!

Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Kama lilivyo Uhuru, Mzalendo na habari leo. Lakini mbona hamlifungii kama ni la udaku. Lilifikia hadi kushawishi polisi wasikubali kutumiwa, na bado hamjalifungia. Ukiona hivi, ujue habari zake zinatoka kwenye reliable source.
 
ilianza chadema au nchi acha kutumia masaburi kufikir
Mnashindwa mtihani siyo kwakuwa hamna akili bali kwasababu hamuelewi maswali, mnajibu maswali ambayo hamjaulizwa. Umepewa swali lakini unatunga la kwako kwenye chumba cha mtihani na kulijibu, ukitoka unashangilia kuwa "nimefaulu mtihani". Ngoja nkusaide bwamdogo, umechangia mada ambayo ilipaswa kusema "bila CDM hakuna nchi hii". Hii ni mada ambayo umeianzishwa mwenyewe na kuijibu, wanasema "bene curere sed extra viam" manake "you are running very well but OUTSIDE the point or the track". Nilichokisema ni kuwa: nchi hii bila CDM hakuna habari manake ni kuwa, habari nyingi zinazotolewa katika vyombo vingi vya habari vinaihusu CDM na si vinginevyo. Sasa, ninafikiri kwa kutumia masaburi au we ndo unajibu kwa kutumia masaburi? Click your head mkuu and shun your damn emotions!!!!!

Genekai!
 
kuwa wapuuzi ambao bado wanasoma tanzania daima gazeti la mbowe lilijaa wachaga wa hai

UDINI na UKABILA ndivyo vilivyokufanya uwapotoshe wafuasi wako na hata leo huna pa kwenda!!... CHAMA CHA WATU wa KIGOMA unachouza kadi zake TABATA na KIBAHA unashindwa kukiendesha?!!! Zungumzia CHAUMA ili tujue sera zako!!!
 
Tuelewe kwamba vyombo vingi vya habari yakiwemo magazeti na waandishi wamenyamazishwa, gazeti namba moja ambalo bado lina ubavu wa kuandika mambo haya kwa uwazi ni Tanzania Daima.

Kuna wengi kutoka vyombo vingine vya habari ambao kwa namna moja au nyingine vyombo vya habari wanavyofanyia kazi vimewekewa uzio wa kutoa habari kama hizi, wameamua kupitishia habari hizo muhimu kwa umma kwa gazeti ambalo liko wazi kuzianika hadharani.

Kwamba mmoja anayehisiwa kutoa habari huenda siye maana kati ya hao waliowanunua kutoka chadema wamo wengine wenye msimamo wa akina
Saanane.

Ndani ya CCM huko kunako mtaa wa makao madogo wamejaa akina Saanane, hao TISS wamegawanyika, ni viongozi wa juu tu ndio wamebaki wameshikamana na magamba, dogodogo washajua wanachosukumiziwa kukifanya ni kulinda masilahi ya vigogo wao badala ya wao wenyewe.
 
wengi watasema habari hii ni ya kidaku lakini inadhihirisha kuwa ujenzi wa 'babel' umefikia pazuri zaidi ya wakati wowote na ni jukumu la cdm kusoma mwendelezo wa haya.
Pesa na nguvu za kidunia hazijawahi kushindana na nguvu ya umma ikilindwa na Mungu
 
Watatajana hadi mshangae na mkuu wa kaya anavyoelekeza.Kwa uhakika nilio nao,hakuna sehemu ya ajira hapa nchini ambako CHADEMA haina mtu!Huko wanakopitisha ma M-PESA,AIRTEL M,TIGO,Walimu,Jeshi,Polisi,Usalama wa CCM wamejaa tele...Hebu jaribu kufanya urafiki na wajeshi wachache halafu uwadodose uone kwamba km si waakati tu umebakia magamba yasepe!KILA MAHALI na wako tayari kuacha kazi..Chezea CDM wewe!
Ni kweli mkuu tupo wengi tu....!!!
 
kuwa wapuuzi ambao bado wanasoma tanzania daima gazeti la mbowe lilijaa wachaga wa hai

Punguza jazba mkuu. Kwani Tanzania Daima au Mbowe ndiyo waliokukosesha ubunge 2010? Si nasikia uliuuza mwenyewe? Na wachaga wa Hai, kama wana sifa, hawafai kufanya kazi Tanzania Daima? Ona hapa chini orodha ya Wachaga walioko TANZANIA DAIMA;

1. Dkt. Lilian Mbowe - Mkurugenzi Mtendaji
2. Ansbert Ngurumo - Mhariri Mtendaji
3. Martin Malera - Mhariri
4. Tullo Chambo - Mhariri wa Michezo
5. Joseph Senga - Mpiga Picha Mkuu
6. Marcus Mtinga - Meneja Usambazaji
7. Saum Abdulkheri - Msanifu Kurasa Mkuu
8. Twalib Mungulu - Meneja Matangazo
 
Chadema ni mpango wa mungu hakuna wakushindana na chadema.hahahaha yaani mwenyezi atuletee njia ya kupitia ili kuiona neema alotujalia wanakuja wavimba macho wanajaribu kushindana ila wataumbuka saa yoyote na muda wowote. hua naiombea chadema timly
 
SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu kufichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare, baadhi ya wahusika wameanza kuvurugana.

Kwa mujibu wa Lissu, njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA.

Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.

Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.

Jana gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.

Vile vile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana kuhusu kuvuja kwa siri zao.

Saumu akiwa katika grosari maarufu kwa jina la Kwa Kimaro jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.

“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.

Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”

Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.

“Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.

Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana.

Katika madai yake, Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.

“Awali walipewa 400,000, wakapewa tena 300,000, pia wakapewa 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu.

Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kama anahusika nazo kwa namna yoyote.

CHANZO:TANZANIA DAIMA

MY TAKE:
HUU NI MWANZO TU WA KUUMBUKA!

Nashangaa sana kuona Mtaka Leo mwigu.. Anaendelea kutamba na kutanua Wakati Kila kona amatajatwa hivi hapa tutaiaminije serikali Yetu?
 
Yaani mtu ananunuliwa kwa sh 400000 tu! Hv kwanini hawa mgamba wanatumia pesa za wananchi kukidhoofisha chadema? Ila wangoje 2015 watakiona cha mtemakuni.
 
Kama mmeweza kuwagundua hao vijana kwa nini inakuwa ngumu kugundua kuwa Lwakatare ni mmoja wao?
Je, mbafikiri CHADEMA kumtosa Lwakatare itakuwa njema kwa CCM na Mwigulu? Hasha haiwezi kuwapendeza ila kukumbatia Nyigu ibawapa faraja sana. Mwenye masikio na asikie habari hii.
 
Kazi ya ccm itakuwa kukanusha lkn haita saidia bora watubu kwa kuwafukarisha wa tz kwa miaka 50 na kuwaomba msamaha na kukabidhi nchi
 
duh,kweli CHADEMA noma,wanapiga kazi TISS ya siku hz cha mdoli tu inasubiria,good beginning to the victory of lwakatare proceedings against the liars,story teller's CCM
 
Back
Top Bottom