Wabaya wa CHADEMA wavurugana!

Wabaya wa CHADEMA wavurugana!

Vijana wa lumumba wanapiga kazi kweli kweli,asiyefanya kazi na asile! Komaeni vijna.Hakuna ajira na serikali haina mpango na nyie,tumikeni kama kinga lakn kaeni mkijua inatumika mara mmoja.
 
Mwigulu Nchemba aka Osama bin Laden wa TZ ataumbuka sana na ufadhili wake wa Ugaidi. Halafu kuonyesha alivyo ziro kichwani anatoa ufadhili wa fedha kwa kutumia Mpesa ambayo inaweza kuwa traced na mtu yeyote.
Huyu sio kiongozi wa kutegemewa tena kama anaweza kuandaa mipango michafu hivyo dhidi ya raia mwenzie wa nchi hii hata kama wanatofautiana itikadi.
 
Mwigulu Nchemba aka Osama bin Laden wa TZ ataumbuka sana na ufadhili wake wa Ugaidi. Halafu kuonyesha alivyo ziro kichwani anatoa ufadhili wa fedha kwa kutumia Mpesa ambayo inaweza kuwa traced na mtu yeyote.
Huyu sio kiongozi wa kutegemewa tena kama anaweza kuandaa mipango michafu hivyo dhidi ya raia mwenzie wa nchi hii hata kama wanatofautiana itikadi.
 
Hapa ndipo ninapowapendea wana - CHADEMA wa JF! Anaanza mmoja anakuja kudondosha bonge la porojo jukwaani! Kisha,wanatokea wengine kiasi cha kumi hivi au hata kumi na tano kisha wanashikana mikono na kuizunguka porojo husika na kuanza kuimbishana "Ukuti! Ukuti! Wa Nazi, wa nazi! Ukuti, ukuti; wa nazi, wa nazi; Ukija upepo; wapepea ! ukija upepo, wapepea!!" Mwenye wowowo anazungusha wowowo, mwenye kitambi anazungusha kitambi;akina sie tunaishia kutikisa machogo tu;kutahamaki, kumbe kuepepea kwa ukuti si kudondoka kwa mnazi!!
 
Mi nilishasema siku nyingi, huu utitiri wa vijana wanaojifanya wanauchungu na hii nchi ni janga la kitaifa....Wengi wapo kwenye siasa kwa maslai binafsi hivyo wanatumika ovyo katika mambo ya kijinga kabisa! What is TZS 400,000/=.....nA HAWA HAPO CDM WAMEJAA TELE NJAA TUUU INAWAWEKA KUWA KARIBU NA CHAMA. NAOMBA SASA HIVI VIJANA WOTE WALIOPO HAPO MAKAO MAKUU LAZIMA IJULIKANE WANAFANYA KAZI GANI ZA KUAJIRIWA NA SIO KUSHINDA HAPO
Mi nashauri CDM wawaweze kujiajiri ili wajipatie ridhiki halali, hata bodaboda wawape wapige kazi.
 
Hizi HABARI siku hizi wala sio habari....
 
SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu kufichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare, baadhi ya wahusika wameanza kuvurugana.

Kwa mujibu wa Lissu, njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA.

Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.

Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.

Jana gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.

Vile vile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana kuhusu kuvuja kwa siri zao.

Saumu akiwa katika grosari maarufu kwa jina la Kwa Kimaro jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.

“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.

Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”

Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.

“Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.

Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana.

Katika madai yake, Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.

“Awali walipewa 400,000, wakapewa tena 300,000, pia wakapewa 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu.

Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kama anahusika nazo kwa namna yoyote.

CHANZO:TANZANIA DAIMA

MY TAKE:
HUU NI MWANZO TU WA KUUMBUKA!

Jamani Chadema mbona mnatuangusha sisi wapenda mabadiliko, kila siku tunasikia kuna watu wanahongwa ili wakisaliti chama, kitu kinachosikitisha ni kiwango cha hongo yaani watu wanahongwa elfu hamsini hadi laki tatu, hizi fedha si wani pm tu ni watumie, inasikitisha kwa kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kuwa wapuuzi ambao bado wanasoma tanzania daima gazeti la mbowe lilijaa wachaga wa hai

Baada ya kutimuliwa Chadema ndiyo unayajua hayo? Kweli njaa mabaya haya kachukue posho
 
Jamani Chadema mbona mnatuangusha sisi wapenda mabadiliko, kila siku tunasikia kuna watu wanahongwa ili wakisaliti chama, kitu kinachosikitisha ni kiwango cha hongo yaani watu wanahongwa elfu hamsini hadi laki tatu, hizi fedha si wani pm tu ni watumie, inasikitisha kwa kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mbona hizi pesa zinatoka hapo ulipo na wanapewa watu mliowarubuni?
 
Hicho chanzo cha hiyo habari sina imani nacho. Hiyo ni habati ya kusadikika tu inaonesha ni jinsigani CDM inavyo tapatapa

Kitoabu

Hapa ni kutumia akili kidogo tuuu...., Chadema ina mkono mrefu sana kwa sasa hata wewe unajua, subiri kitambo....., mimi nadhani CCM wajielekeze kuwaletea watu maendeleo, wananchi watawaelewa, lakini kwa mtindo huu Kitoabu hatufika
 
Mwigulu nchemba hizo siasa za kitoto anazoendesha zitammaliza kisiasa ndani ya ccm na nje ya ccm.Na aelewe hakuna siri chini ya jua siku si nyingi kila kitu kitakuwa wazi,huo mchezo watu wenye busara wa ccm wamekaa pembeni kwa kuwa wanajua mwisho wake ni mbaya kuliko mwigulu anavyofikiri.na hii njia anayotumia ili cdm ifutwe aelewe itasababisha vurugu maandamo na uasi mpaka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
 
Mwigulu Nchemba aka Osama bin Laden wa TZ ataumbuka sana na ufadhili wake wa Ugaidi. Halafu kuonyesha alivyo ziro kichwani anatoa ufadhili wa fedha kwa kutumia Mpesa ambayo inaweza kuwa traced na mtu yeyote.
Huyu sio kiongozi wa kutegemewa tena kama anaweza kuandaa mipango michafu hivyo dhidi ya raia mwenzie wa nchi hii hata kama wanatofautiana itikadi.
Una ushahidi na unacho kinena?
 
Kama kuna ukweli inasikitisha,maana juhudi hizi na pesa hizo zingesaidia hata kununua panadol kwa ajili ya dispensari moja.
 
Back
Top Bottom