Waanzilishi wa kipindi cha Futuhi!

Teko

JF-Expert Member
Jul 3, 2010
230
61
wanajamvi ,kwa wale wapenzi wa kipindi cha vichekesho cha Futuhi kinachorushwa na star tv,ningependa kujua kama kuna yeyote anayefahamu kuhusu wale waanzilishi wa kipindi hicho! Maana ni wiki kadhaa sasa naona wahusika wengi ni wageni tu na wale waanzilishi hawaonekani tena!
 
mwenyewe nimesikitika sana hasa yule msukuma simuoni tena, sijui ndo mambo ya mizeg'we kina zembwera out
 
Mie nimesikia kwamba jamaa wanalipwa kwa mbinde pale Star maana eti wanapewa laki moja moja tu kwa kazi yote ile wanayoifanya kwa mwezi mzima. Sasa pesa hiyo mbuzi haiwezi kumfanya mtu aweze ku-sustain maisha yake. Na pia nasikia pamoja na kwamba Bwana Dialo mwenyewe ndio alikuwa nyuma ya kuanzisha kikundi hicho na kuwatengea usafiri maalu wa kuwapeleka kurekodi, lakini shuguli ya kurekodi kwao huwa ni mbinde kwa sasa kiasi kwamba ukichanganya na matatizo ya fedha kiduchu na umaarufu walionao wanaona hakuna kitu bora kukaa mtaani. Ndio sababu hata waandishi mahiri kwenye TV hii nao walishakimbia kwa sana tu kutokana na hali ngumu, fuatilia utabaini ukweli wa haya mambo.
 
Ni kweli FUTUHI ilikuwa juu sana, mie nilimpenda yule Muha na Nshomire, sasa utamu umeisha. Ama kweli Strtv mmetema bazoka kwa karanga za kuonjeshwa
Nasikia mmetangaza nafasi za waigizaji wa vichekesho, mtupe na taarifa basi ya waanzilishi wa FUTUHI kuondoka kwenu
 
Tatizo la Wasanii kudharauliwa linaendelea kuwakumba hata wakiiletea mafanikio TV station, wamiliki wanadhani mtu yeyote anaweza kuchekesha! I no longer watch futuhi!
 
Nadhani ni matatizo yaleyale kama ya Ze Komedi pale EATV..................
 
ni kweli wale waigizaji walioachwa walikuwa wazuri sana kuliko wa sasa. hasa yule aliyekuwa anaigiza ulevi au msukuma
 
Hizi TV zetu nadhani malipo ni ya wasiwasi sana. Hivi kuna mtu anaweza kuwa na idea TVs zipi zinaopngoza kwa malipo hapa Tz?
 
Wale jamaa waliipandisha sana chati startv katika tasinia ya mambo ya comedy sasa hakuna mvuto kabisa.Star tv kwisha habari yake.
 
Back
Top Bottom