Waangalia Movie naombeni msaada wenu

Martin Kemosabe

Senior Member
Jan 28, 2020
168
225
Kuna movie niliangalia miaka kidogo imepita ila jina siikumbuki, naomba nisimulie kidogo story kisha kwa atakaeweza ifahamu naomba anisaidie kukumbuka jina la movie.

Story inaanza (ntasimulia nilipoikutia tu) kwahiyo mtaniwia radhi kama nitakuwa nimejichanganya changanya.

Kuna mdada mmoja alikuwa yupo na simu yake akawa ameingia chumbani kwake anatafuta nguo ya kuvaa, wakati anachagua chagua nguo ikaingia message saa hiyo mkononi kashika nguo, kusoma ile message akakuta ameambiwa (hilo gauni lizuri livae litakupendeza) yule dada akawa anashangaa sana akaangalia huku na kule hamna mtu.

Baadaye akam-text yule aliemtumia message kumuuliza wewe nani? Sijui alijibiwa au lah sikumbuki, basi dada akavaa ile nguo, alipomaliza kuvaa akavaa na viatu mara message ikaingia tena kwenda kusoma akakuta yule mtu alomsifia saivi anamsifia tena kuwa kapendeza sana sana, basi yule dada akawa anashangaa sana mpaka hapo hajui anaemtumia message na wala hamuoni anaemtumia message.

Maisha ya yule dada yaliendelea vile vile kuchati na yule mtu sijui waliishia wapi ilikuaje na mwisho ikaendaje, naombeni msaada wenu wapenda movie wote msaada wenu unahitajika hapa.

NOTE: Sio Bongo Movie
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,433
2,000
Hiyo muvi inataka kufanana na muvi ya 2018 inaitwa Anonymous. Jamaa alikua anachati na mtu akawa anamueleza mengi kuhusu yeye. Akamwambia nenda barazani rafiki yako anachepuka na dem wako. Jamaa kuchunguza akagundua ni kweli, aliwapa kifinyo..aliwatesa sana hadi kuwaua maana alikua ameenda kutembea kwa huyo rafiki yao..rafiki nae alikua na demu.

Yule aliyekua anachati nae ndio alimshauri awaue..halafu akamwitia polisi
 

Martin Kemosabe

Senior Member
Jan 28, 2020
168
225
Hiyo muvi inataka kufanana na muvi ya 2018 inaitwa Anonymous.. Jamaa alikua anachati na mtu akawa anamueleza mengi kuhusu yeye..Akamwambia nenda barazani rafiki yako anachepuka na dem wako. Jamaa kuchunguza akagundua ni kweli, aliwapa kifinyo..aliwatesa sana hadi kuwaua maana alikua ameenda kutembea kwa huyo rafiki yao..rafiki nae alikua na demu.

Yule aliyekua anachati nae ndio alimshauri awaue..halafu akamwitia polisi
kwenye hii movie nayoiulizia mdada ndio alikua akichatishwa na mtu asiemjua
 

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,267
2,000
Mkuu huyo sio Maureen kwenye
'Personal Shoper'?
Screenshot_2020-02-10-19-24-27.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom