Kilongwe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 423
- 116
Ukitaka kuinyima nchi maendeo, basi wanyime watu wale maarifa na ukitaka kuipa nchi maendeleo basi wape watu wake maarifa. Nchi yenye watu wenye maarifa, sio tu wataweza kutumia maarifa yao kwenye kuijenga nchi bali pia wataweza kuyatumia kupigana na wavamizi wasiowatakia mema.
Nilipofika China, kitu kilichonishangaza ni kuona kila sehemu kuna vitabu, na vingi kati ya hivi ni vya kwao wenyewe. Hii sio tu inawawezesha kupunguza gharama za usomaji, bali pia inawafanya watu wa chini kabisa kuwa na ujuzi na uwezo wa kufanya kazi za kawaida (cheap labor) na hii ndio secret ya China. Jamaa wamelocalise kila kitu chao, leo hii sisi hata historia ya nchi yetu tunasubiri kuandikiwa na wazungu.
Katika kulitambua hilo, kama walivyosema wahenga, zuri chukua na baya waachie wenyewe, ndio sababu niliwashauri wenzangu tukaanzisha AfroIT. Lengo lake ni kuwa na elimu na maarifa kwa kishwahili, kuanzia makala za taarifa na zile za ujuzi wa mafundisho. AfroIT si tovutii ya biashara na itaendelea kuwa hivihivi kwa miaka yote ya uwepo wake ingawa tunatarajia kukua zaidi na zaidi kulingana na michango ya wanajamii. Hivyo hatutotarajia kuwalipa waandishi, ni kazi ya kujitolea kwa 100%, hivyo ni kwa wale tu walio tanguliza uzalendo kwanza na wana wasaa wa kufanya hivyo.
Hivyo basi, tunakukaribisha wewe mwanajamii kushare kwa uchache wake chochote kile ulicho nacho ambacho unaona kwa namna moja au nyingine kitanufaisha jamii kwenye nyanja ya ICT.
Kushiriki uandishi, tuma makala kwenda nyonim@afroit.com
AfroIT Maarifa:
Mwisho: Tupo njiani katika kukamilisha AfroIT Maarifa.Hii ni kitu kama Wikipedia(au Baidu Sayansi) ambayo italenga sana Afrika ya Mashariki (Lugha mama itakuwa ni Kiswahili),AfroIT Maarifa itakuwa na kila kitu,sio tu ICT bali hata mambo ya Afya,mazingira,mechanics nk ambapo waandishi na members wote wa AfroIT watakuwa na uwezo wa kuchangia makala,kuhariri nk. Hivyo tushirikiane pamoja.
Siku si nyingi tutaanzisha kampeni hii ya kukusanya pesa kwa ajili ya hili, hivyo kama wewe ni programa, designer, mtaalamu wa project, uandishi au mtu ambaye unaona unaweza kuwa na mchango kwenye AfroIT Maarifa, usisite kuwasiliana naminyonim@afroit.com au simu namba +8615271818525
Nyoni Mkata
Founder
AfroIT Group