Waandishi wa Habari na Posho Zaidi ya Moja kwa Kazi ile ile! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa Habari na Posho Zaidi ya Moja kwa Kazi ile ile!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Oct 31, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakati vumbi la hoja kuhusu posho zaidi ya moja kwa kazi ile ile halijatua, niliangalia Star TV ambapo kulikuwa na mjadala kuhusu waandishi wa habari kulipwa posho hizo! Kwa haraka haraka nilipata mambo mawili makuu kwenye mjadala huo: 1. Je, mwandishi wa habari akilipwa posho na yule ambaye amemwalika kwa ajili ya kuandika habari kwa ajili ya tukio fulani (km kampeni za uchaguzi) ataandika kweli hata mabaya ya mlipa posho kama yapo? Kama sivyo, weledi (professionalism) uko wapi hapa? 2. Baadhi ya waandishi wa habari wanalipwa mishahara midogo na wengine hawalipwi (wanaishi kwa posho), je, wakiacha kupokea posho watajikimu namna gani? Naleta mjadala huu kwenu wadau kwa ajili ya brainstorming, nini kifanyike ili kuwanusuru waandishi wa habari na utumwa kwa wenye fedha?
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wadau tujadili kuhusu wadau wetu hawa muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu!
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Unazungumzia uweledi katika uandishi wa habari bongo!
  Inasikitisha sana jinsi hii taaluma imevamiwa na watu wa kila aina - vyuo vinaanzishwa kila kukicha... na kuzalisha waandishi kwa idadi kubwa bila kujali quality.Matokeo yake ni kujaza soko .... sasa hawa waandishi watafanyaje na huku wanahitaji kuishi? Wanageuka wabangaizaji kuvamia shughuli za watu ili wajipatie bahasha za khaki.

  Hivi MCT wana role yoyote katika kuweka standards na kuhakikisha hii aibu inapungua kama siyo kuisha kabisa?

  Binafsi huwa naona aibu kubwa kuona wenzetu hawa wanavyohanja kutafuta hizi posho ambazo huingilia katika uhuru wa uandishi na pia kuidororesha Media which is the 4th estate to ensure checks and balances katika utendaji wa dola na hata sekta binafsi.
   
 4. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #4
  Oct 31, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanalipwa mishahara midogo kwasababu ya kuandika mambo madogo madogo. Mfano unaandika taarifa kuhusu mabomu ya mbagala ina paragraph mbili hamna reference yoyote utaendelea kulipwa peanuts kila siku. Wafanye investigative reporting waandike mambo yenye uzito waweze kuthaminiwa na wamiliki wa magazeti. Mmiliki wa gazeti akiwa anamtegemea mwandishi hawezi kumlipa posho ndogo. Unajua sijawahi kuona mwandishi wa gazeti hapa Tanzania ameandika article inayo span zaidi ya ukurasa mmoja au gazeti moja. Lakini kwa wenzetu huko ulaya ni jambo la kawaida.

  Ushauri mwingine kwao kama waandishi, waandike vitabu.

  .
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ule muswada wa Sheria mpya ya habari sijui kama ume-address mambo ya weledi katika uandishi wa habari au wenyewe umejikita kwenye uhuru wa vyombo vya habari pekee? Hivi kuna definition wa "mwandishi wa habari?" Au kwa kuwa mtu ana cheti basi automatically anakuwa mwandishi wa habari hata kama kimaadili kwenye uandishi ni mbabaishaji?
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama mwandishi analipwa kulingana na uzito wa article aliyoandika na sio kulipwa mshahara basi waandishi wa habari ni vibarua na sio waajiriwa wa kudumu! Na kama ni vibarua suala la kulipwa posho mara mbili kwa kazi moja litahitaji greda kulitoa kwao!
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Pesa hizi mara nyingi zimekuwa ni kwa ajili ya kujenga urafiki kati ya wanasiasa au watendaji wa serikali na vyombo hivi, ambao ni wa kimaslahi.

  Hebu angalia baadhi ya magazeti ambayo yanajidai kuwa investigative. Chukuwa mfano wa Mwanahalisi, where is the news nowadays?

  Ni gazeti lililoonekana kama lina nguvu ya ki-investigative, sasa hivi halina cha kuandika siyo kwa sababu hakuna ya kuandika, lakini ni kwa sababu anayotaka kuandika yanakuwa mtaji toka kwa muathilika.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwenye hii taaluma kazi ipo! Tatizo jingine kubwa kuliko yote ni kwamba baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wanamiliki vyombo vya habari, sasa niambie kama hatavitumia kama rungu dhidi ya critics wake na mara nyingine kama sabuni ya kujisafishia! Kwa ujumla kaeneo haka ka uandishi wa habari kamekaa vibaya na udhibiti wake ni mgumu sana!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Buchanan,
  Kupokea takrima au posho katika uandishi wa habari ni kinyume cha maadili. Katika nchi zilizoendelea unapoajiriwa kazi na shirika la habari mojawapo ya mambo unayosaini ni kwamba hutapokea posho kutoka mtu au kampuni unayoripoti juu yake, lakini unaruhusiwa kumnunulia chai, au lunch source ya ripoti zako na ofisi yako itaku-reimburse. Ili tuwe na waandishi habari makini wanaozingatia weledi, mwajiri anapaswa kutenga kando fungu fulani la matumizi, kama vile hela za usafiri kwa waandishi wao wanaozurura mitaani kutafuta habari. Lakini iwe ni marufuku kupokea bahasha kutoka kwa mawaziri, wabunge, au kampuni ambazo zinaripotiwa katika vyombo vya habari. Ama sivyo tutaendelea kuwa na makanjanja tu na mamluki katika fani hii muhimu.
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Oct 31, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba bahasha za kaki zikipigwa marufuku watoto watakufa njaa! Na kama kuna mmiliki wa chombo cha habari na ni mwanasiasa udhibiti wake ukoje hapo?
   
 11. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  amna kibaya hapo kama mtu ana fanya kazi kama free-lance journalists, kibaya ni gazeti kupokea directly malipo kutoka kwa mtu kwa nia ya ku-mislead jamii. Hata hawa itakua ngumu mno kumu accuse mtu kwani watu wanaruhususa kuandika isipokua cha uongo.

  'Rupert Murdoch' amesaidia kuwa weka viongozi wengi madakarani through his media empire na viongozi wamemsaidia kuvunja sheria nyingi ili aweze expand.

  Hila mwandishi wa habari anao uhuru wa kuandika na kutetea anacho kiamini hata iwe ni kumpigia mtu debe. Ndio maana ya free speech, na malipo wao si wanasiasa hivyo uwezi kuwa ukumu.
   
Loading...