Waandishi wa habari mnatukosea

Waandishi wa habari mnatukosea

Hivi ili uwe muandishi wa habari, mtangazaji au mhariri unapaswa kupitia hatua zipi??

Wiki iliyopita king'amuzi chetu cha Azam kiliisha. Nikawasha redio kuisikiliza mechi ya Simba na Singida.
Mara nikasikia sauti ya mzee wangu ikinambia " tafuta kituo kingine, hao watangazaji stori ni nyingi". Nikabadili chap, nikafika kituo kingine, napo yalikuwa yaleyale.

Mtangazaji: Ni mechi nzuri ya kuvutia. Mpira unapigwa haswaaa au unasemaje mchambuzi wangu (YYY)

Mchambuzi: Exactly, Ni kweli mbungi linapigwa, exposure kubwa na confident ya wachezaji iko high hii inaonyesha samani ya ligi yetu. Ligi inawachezaji wengi experiencing ambao wamepata experienced kutokana na a alot of an international matches.(🤣🤣🤣🤣🤣🤣)

(Wakati wakiendelea na stori zao, na vingeleza vya uongo, mara tukasikia kelele kwa jirani. Tukaamini kuna tukio limetokea. Labda goli au mtu amekoswakoswa lakini sisi hatukujua lolote)

Ghafla tukasikia mtangazaji anasema " Singida wanapoteza nafasi ya wazi hapa, alikua Rupia, alipiga shuti kali sana lililipita mita chache tu, Camara alisimama akishangaa kama mbwa aliyepotea, anahema kwa kasi sana hapa.(🤣🤣🤣)

Kumbe ile redio tulikuwa tunasikiliza wengi, maana baada ya kauli ile ya mtangazaji tulicheka kwa pamoja watu wengi tuliokuwepo nyumbani. Baada ya hapo hatukuendelea na kuufatilia mpira, mada ikaanza.

Dadangu mmoja alisema hivi " bora hao wa mpira, wanapiga stori zao lakini ni za mpira huo huo, kuna hawa wa kusoma magazeti redioni asubuhi, ni makelele tuu" akatoa mfano

M1: Mwananchiiiiiiiiiiiiiiiii
M2:Unasema ??????
M1: Mwananchiiiiiiiiiiiiiii
M3: Gazeti la Mwananchi linasemaje?????
M1: Ujue wananchi wanaokaa pembezoni mwa mbuga wanapata changamoto nyingi sana.
M2: kwanin??
M1:Gazeti la mwananchi linasema. Wananchi Simiyu walalamikia tembo.
M3: Walalamikia tembo??? Tembo wakale wapi?? Kwani tembo wanalima?? Mimi ningekuwa tembo na ningesikia hizo tuhuma ningewafata hao watu wangenikoma.
(Waandishi wote wanacheka) wanaamia gazeti lingine.

Kuna gazeti moja kubwa kwenye ukurasa wa mbele liliandika IJP amefanya mabadiliko kikosi cha usalama barabarani, badala ya kusema IGP. Unajiuliza aliyeandika hivi ni nani?? Gazeti halina mhariri ?? Unabaki kushangaa.
Pascal Mayalla
 
Inawezekana changamoto kubwa ikawa elimu, na hasa elimu tu ya sekondari. Wengi ni wale four za mwisho then wanakimbilia vyuo vile vya D 4 kufata certificate ya Journalism
Niliwahi kumsikia mdau mmoja wa hayo mambo ya utangazaji akisema kwenye hizo ajira wao wanaangalia zaidi "kipaji binafsi" cha mhusika na "mapokeo ya wateja" (wasikilizaji) kwa huyo mtangazaji husika. maana yake staff anayeajiliwa ni yule wasikilizaji wanamwelewa na kumkubali, fullstop! hapo utaona hakuna ishu ya shule ya mhusika inaongelewa.

sasa hizi redio nyingi ni za burdani zaidi (kuliko uelimishaji) na wote tunajua wasikilizaji wake ni wa aina gani. kwahiyo tusilaumu tu, wasikilizaji wa redio hizo ndio wanaozalisha hao watangazaji wa hizo redio. maana yake km wewe sio wa huko (burdani) tafuta redio zinazofaa mwelekeo wako.

ila pia aliongea kuwa wengi wenye magamba wanaotoka mashuleni na vyuoni mara nyingi wanapwaya na kuachwa mbali na hao wenzao wa "vipaji binafsi" hasa kwa kuzingatia hivyo vipimo vya "kipaji binafsi" na "mapokeo ya wateja".
 
1000010562.jpg
 
Inawezekana changamoto kubwa ikawa elimu, na hasa elimu tu ya sekondari. Wengi ni wale four za mwisho then wanakimbilia vyuo vile vya D 4 kufata certificate ya Journalism
Umeongea vema kabisa
 
Kuna siku nilimsikia Baraka Mpenja anasema mapinduzi ya Zanzibar yaliongozwa na Mzee Karume 😀 nikasema hawa ndo aina ya waandishi wa habari tulio nao Tanzania.
 
Hivi ili uwe muandishi wa habari, mtangazaji au mhariri unapaswa kupitia hatua zipi??

Wiki iliyopita king'amuzi chetu cha Azam kiliisha. Nikawasha redio kuisikiliza mechi ya Simba na Singida.
Mara nikasikia sauti ya mzee wangu ikinambia " tafuta kituo kingine, hao watangazaji stori ni nyingi". Nikabadili chap, nikafika kituo kingine, napo yalikuwa yaleyale.

Mtangazaji: Ni mechi nzuri ya kuvutia. Mpira unapigwa haswaaa au unasemaje mchambuzi wangu (YYY)

Mchambuzi: Exactly, Ni kweli mbungi linapigwa, exposure kubwa na confident ya wachezaji iko high hii inaonyesha samani ya ligi yetu. Ligi inawachezaji wengi experiencing ambao wamepata experienced kutokana na a alot of an international matches.(🤣🤣🤣🤣🤣🤣)

(Wakati wakiendelea na stori zao, na vingeleza vya uongo, mara tukasikia kelele kwa jirani. Tukaamini kuna tukio limetokea. Labda goli au mtu amekoswakoswa lakini sisi hatukujua lolote)

Ghafla tukasikia mtangazaji anasema " Singida wanapoteza nafasi ya wazi hapa, alikua Rupia, alipiga shuti kali sana lililipita mita chache tu, Camara alisimama akishangaa kama mbwa aliyepotea, anahema kwa kasi sana hapa.(🤣🤣🤣)

Kumbe ile redio tulikuwa tunasikiliza wengi, maana baada ya kauli ile ya mtangazaji tulicheka kwa pamoja watu wengi tuliokuwepo nyumbani. Baada ya hapo hatukuendelea na kuufatilia mpira, mada ikaanza.

Dadangu mmoja alisema hivi " bora hao wa mpira, wanapiga stori zao lakini ni za mpira huo huo, kuna hawa wa kusoma magazeti redioni asubuhi, ni makelele tuu" akatoa mfano

M1: Mwananchiiiiiiiiiiiiiiiii
M2:Unasema ??????
M1: Mwananchiiiiiiiiiiiiiii
M3: Gazeti la Mwananchi linasemaje?????
M1: Ujue wananchi wanaokaa pembezoni mwa mbuga wanapata changamoto nyingi sana.
M2: kwanin??
M1:Gazeti la mwananchi linasema. Wananchi Simiyu walalamikia tembo.
M3: Walalamikia tembo??? Tembo wakale wapi?? Kwani tembo wanalima?? Mimi ningekuwa tembo na ningesikia hizo tuhuma ningewafata hao watu wangenikoma.
(Waandishi wote wanacheka) wanaamia gazeti lingine.

Kuna gazeti moja kubwa kwenye ukurasa wa mbele liliandika IJP amefanya mabadiliko kikosi cha usalama barabarani, badala ya kusema IGP. Unajiuliza aliyeandika hivi ni nani?? Gazeti halina mhariri ?? Unabaki kushangaa.
Mkuu fani ya uandishi wa habari imevamiwa ja wapuuzi, wahuni na makanjanja wasiokuwa na weledi wowote kwenye uandishi wa habari. Redio itaongozwa na akina Zembwela, Juma Lokole, na Mwijaku halafu utarajie maajabu? Never!
 
Siku hizi kusikiliza radio hapana bora uungane na akina Mama kuangalia tamthilia za Kibongo.
Kweli kabisa mkuu. Unaweza ukatafuta station ya kusikiliza ukafungua stations zaidi ya 30 usipate hata moja ya kusikiliza. Nchi ngumu sana hii.
 
Back
Top Bottom