Waandishi Clouds 360 wamshukia kama mwewe wakili Msando kwa kupotosha kuwa Arusha hali ni mbaya kwa Corona

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Watangazaji wa Clouds tv Sasali, Kabaye na Ngoma wamesema wakili msomi Albert Msando hana haki ya kuwasemea wananchi wa Arusha kuhusu Corona.

Ngoma amesema RC Gambo ndio anajua hali halisi ya mkoa wake, Msando anapaswa kuelezea waliofisadi mali za CCM waliowachunguza na siyo Corona. Amesisitiza kuwa wao kama waandishi wanaongozwa na miiko ya taaluma yao katika kuandika na kuripoti habari hivyo Msando asiwafundishe kazi.

Watangazaji hao nguli walikuwa wanaijadili clip iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha Msando akigawa Barakoa na vitakasa mikono kwa waandishi wa habari wa Arusha, na wamemkosoa kwa kugawa barakoa wakati yeye mwenyewe akiwa hajavaa.

Pia soma > Albert Msando ‘amwaga’ vifaa vya Corona kwa wanahabari Arusha, adai hali ni mbaya sana - JamiiForums

Chanzo: Clouds tv!
1588182883578.png
 
Clouds nilishawadharau siku nyingi,hawana tofauti na TBC,ukweli ni kwamba hali ni mbaya na tukitegemea serikali ituambie nini cha kufanya tutaendele kupoteza ndugu zetu,

Huyo mwenye mamlaka ya kutangaza mbona kakaa kimya?au anafikiri ukweli hatuujui huku mitaani,hovyo kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watangazaji wa Clouds tv Sasali, Kabaye na Ngoma wamesema wakili msomi Albert Msando hana haki ya kuwasemea wananchi wa Arusha kuhusu Corona.

Ngoma amesema RC Gambo ndio anajua hali halisi ya mkoa wake, Msando anapaswa kuelezea waliofisadi mali za CCM waliowachunguza na siyo Corona. Amesisitiza kuwa wao kama waandishi wanaongozwa na miiko ya taaluma yao katika kuandika na kuripoti habari hivyo Msando asiwafundishe kazi.

Watangazaji hao nguli walikuwa wanaijadili clip iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha Msando akigawa Barakoa na vitakasa mikono kwa waandishi wa habari wa Arusha, na wamemkosoa kwa kugawa barakoa wakati yeye mwenyewe akiwa hajavaa.

Pia soma > Albert Msando ‘amwaga’ vifaa vya Corona kwa wanahabari Arusha, adai hali ni mbaya sana - JamiiForums

Chanzo: Clouds tv!
Watangazaji Nguli!!!?
 
Back
Top Bottom