Wakili Albert Msando ashikiliwa na Polisi baada ya kutoa taarifa ya hali ya maambukizi ya Corona na kuhamasisha waandishi kuandika ukweli

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,568
2,000
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Koka Moita amesema Alberto Msando ameitwa kwa ajili ya Mahojiano ila ni mapema sana kusema ni mahojiano yanayohusu nini kwani hana taarifa kamili

Alipoulizwa kama kushikiliwa kwa Wakili Msando kunahusisha yale aliyoongea jana wakati wakati akikabidhi vifaa ya kujikinga na #COVID19, amesema hasema hana taarifa kamili na suala hiyo halijakaa sawa kuzungumzia

Aidha, amethibitisha kuwa Wakili Msando ameitwa Polisi kwa mdomo kama ambavyo alitumia yeye alitumia kuzungumza, na kuwa hakuna nguvu iliyotumika

Kamanda Moita amesema, “Kama ambavyo alitumia mdomo kuzungumza, na kuja Polisi pia imetumika kauli ya kumuita.” Amesema pia mahojiano yakikamilika atatoa taarifa

Jana wakati akigawa vifaa hivyo alisema “Ni kweli na niseme bila kuficha hali ni mbaya, kwa Arusha hali ni mbaya. Ndugu lazima mfike mahali muweke mguu chini mseme ukweli ili Wananchi, Serikali na kila anayehusika atambue tupo katika hali mbaya ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuchukua hatua.”

Aliongeza, “Mkirudi nyuma na kuogopa kusema, tutazikana. Hii ndio nafasi yenu, tusipozungumza, msipo andika na kusema ngoja tutoke tukatafute ukweli na tuuseme, basi huu ugonjwa hautaondoka kirahisi.”


Pia soma: Albert Msando ‘amwaga’ vifaa vya Corona kwa wanahabari Arusha, adai hali ni mbaya sana - JamiiForums


UPDATES
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita amesema wanamshikilia Wakili Albert Msando baada ya kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Serikali juu ya ugonjwa wa #COVID19

Amesema Msando amedai kuwa mkoani humo hali ya maambukizi ni mbaya ili hali yeye hana mamlaka hayo huku akiwataka waandishi wa habari wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa za ugonjwa huo

Ameongeza, "Hali hii ilitoa wakati mgumu kwa wananchi waliokuwa wanasikiliza na kauli hii aliitoa wakati anatoa vifaa vya kujikinga na #CoronaVirus katika eneo la Kaloleni katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari-Arusha"

Amemalizia "Serikali ilishatoa maelekezo kuwa mwenye mamlaka ya kutoa tarifa hizo ni Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Mganga Mkuu, hii kauli lazima iheshimiwe"
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,009
2,000
Huu ni ujinga wa kupitiliza
Mtakamata wangapi?
Kwa nini mnaficha takwimu inawasaidia nini?
Msando jamaa zako hao umenaswa ulikuwa mstari wa mbele kuwasimanga Chadema
Tukisema kijani ni lost case muwe mnaelewa
Pole kwa maswahibu wakili naniliii

Huyu kiukweli bado itikadi zake ni Chadema ....sema tu ile zengwe la money laundering lilimtisha , sasa angalia kajisahau kama yuko ccm
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,277
2,000
Waandishi watu wajanja sana!
Kamanda kaulizwa alichoiitiwa Msando kamanda kakataa kusema kwa sasa.
Kaulizwa njia iliyotumika kumuita/kumfikisha kituoni ndugu Msando hapo ndiyo kamanda kaingia mtegoni "Kama njia aliyotumia kuzungumza ...." kajikuta kajibu swali alilolikataa kujibu mwanzo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom